Makampuni ya ujenzi wa makazi

Makampuni ya ujenzi wa makazi

Kwa ukosefu huu wa kazi na kipato, heri tuishi kama tunavyoishi. Mtu anapata hela kununua unga nusu na matembele, apate hela ya kupanga apartment! Tanzania yetu hakuna kipato cha uhakika cha watu kuishi kwenye apartment. Zilizopo kwa sasa zinakosa wanunuzi na wapangaji. Heri tuishi kwenye mabonde yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwajui wabongo. ..kwa tabia zao wanaona shida kukaa kwenye apartment.

Utakuta anaishi na bata. ..kuko gorofani bata watapandaje.

Kibustani cha tembele anakiweka wapi.

Kwani hapa bustani iko wapi? Na hata bata wake hapa atamjua ni yupi?
302f6d1cff18ddef2b674966256d3790.jpg
 
Kwa ukosefu huu wa kazi na kipato, heri tuishi kama tunavyoishi. Mtu anapata hela kununua unga nusu na matembele, apate hela ya kupanga apartment! Tanzania yetu hakuna kipato cha uhakika cha watu kuishi kwenye apartment. Zilizopo kwa sasa zinakosa wanunuzi na wapangaji. Heri tuishi kwenye mabonde yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Huko kwenye mabonde mnalipa ngapi mkuu. Mimi niko kwenye nyumba lakini siwaelewi wanaokodi. Wanalipa zaidi ya kulipa mkopo wa nyumba. Na kila mwaka kodi yao inapanda wakati mwenye nyumba kila mwaka deni lake linapungua.

Si uchawi ni mahesabu tu mkuu.
 
wapo mkuu una nunua land na ku design nyumba yako na unamwachia mpenzi huku wewe uk

Ni nadra sana labda uwe muwekezaji wa ardhi. Kuhusu kudizaini nyumba yako unaweza kumalizana na kontrakta. Inategemea eneo na utawala wa serikali za mitaa.
 
Sijawahi kusikia mtu Marekani kanunua kiwanja cha kujenga nyumba. Kwanza kuna majimbo mengine viwanja ni mali ya serikali. Nyumba yako kiwanja cha serikali. Utatia akili hapo.
ikiwa hivyo tz utashangaa ukiwa upinzani tu,serikali inakupokonya kiwanja inakuacha na nyumba yako.Tz tukubali bado saaaaana,nyie tuishi tu
 
Sheria zibadilishwe kama zinavyobadilishwa za madini. Wajenzi wa kiholela wanaidhulumu serikali kipato kushinda Acacia.

Elewa makampuni ya ujenzi hulipishwa kodi kwa mabilioni. Kina mzee Asumani wakijenga nyumba hawalipi kodi yeyote. Hata hela hawaweki benki.

Mwenye jumba la kupangisha ana kodi mbili. Kodi ya jengo lenyewe na kodi ya biashara ya kupangisha jengo kubwa kama hili.
Kwa sasa hivi kina mama Kaundime wakikusanya kodi ya pango hawailipii kodi yeyote.
05a797a10ca238eca8e12c3bbc901579.jpg
 
Unaongelea maisha ya magharibi ukilingamisha na Tanzania
Hivi unadhani ni rahisi kiasi hiko mtu wa kawaida akakope nyumba kisa tu imejengwa tabata

Tanzania mtu yuko radhi akakae bagamoyo imradi tu asisumbuliwe na mwenye nyumba
Anaweza akanunua pia endapo nyumba hizo zitakakuwa zinauzwa kwa bei nafuu
 
Marekani ukipangisha nyumba yako halafu ukae kimya usiwambie watu bado mwisho wa mwaka utapata barua kutoka halmashauri ya mji inasema inaonekana wewe umepangisha nyumba yako kwa hiyo tunakudai kodi ya kupangisha nyumba kiasi kadhaa wanakuandikia.
 
Ii point nzuri sana kinachofanyika sasa ivi ni nhc kutuuzia nyumba kwa bei ya juu,ili linatokana na kukosa ushindani,...ila ili lilitakiwa lifanyike apo kigamboni sasa sijui ni lipi lilitokea

Sent from my SM-G950FD using JamiiForums mobile app
 
2bd03fa89410c1fc750c64f056d1ea28.jpg



Katika nchi zilizoendelea miji hujengwa na makampuni ya ujenzi.

Moja ya shughuli zao ni kununua ardhi wakajenga kitongoji/mji wa kisasa. Chukulia eneo lote la Tabata lingekuwa limejengwa na kampuni ya ujenzi. Nyumba za kisasa na za mpangilio.

Na baadae kampuni hiyo huuza nyumba za eneo hilo au kuzikabidhi kwa mwenye mradi wake (mwekezaji)

Hivyo ndivyo miji inavyojengwa. Hakutakuwa na mfumuko wa bei za nyumba za ajabu ajabu. Watu wanaweza kupewa mikopo ya nyumba. Ukishindwa kulipa unatolewa tu hela yako uliyokwisha lipa hurudishiwi na nyumba anauziwa mtu mwingine.

Yafuatayo ni makampuni kumi kati ya mengi yanayoshughulika na ujenzi wa makazi ya wananchi nchini Marekani.

1. D.R Horton Inc.
2. Pulte Group (2013
3. Lennar Corp
4. Toll brothers Inc
5. Taylor Morrison Home
6. Hovnanian Enterprises.
7. KB Home
8. Ryland Homes
9. Standard Pacific corp
10. Meritage Homes

Mtu anitajie makampuni kumi ya ujenzi wa makazi (sio ya nyumba moja moja) yaliyopo Tanzania.

Inasikitisha sana viongozi wanaposafiri nje wanauona utaratibu lakini wanashindwa kuutekeleza Tanzania.

Hata ikibidi kuleta wawekezaji wa ujenzi wa miji. Watakuwa ni wa maana kuliko Acacia. Kwa sababu mwisho wa siku wawekezaji wa hivi wanatuachia miji ya kisasa.

Uwekezaji wa hivi utatoa ajira nyingi sana kwenye sekta ya ujenzi na usafi wa miji. Wawekezaji sio Tigo na Voda tu ambao tunawashukuru kwa kurahisisha mawasiliano lakini kwa upande mwingine wamebwetesha sana watanzania. Umbea umetawala kwenye instagram na Facebook. Kazi hakuna na wananchi wananyonywa sana visenti vyao kwenye mabando yasiyochacha na yanayochacha.
Nipe jibu yakinifu, hayo makampuni yanajenga hizo nyumba kwa hela toka wapi?
 
Point nzuri sana, ndivyo tunavyotakiwa kuishi. NHC wanafanya, kuna ile kampuni inajenga kwa ajili ya wafanyakazi wa serikali Watumishi Housing Corporation, WHC.

Kinachoumiza zaidi ni UMASIKINI uliokithiri wa walio wengi, watu wanaishi below poverty line < $1 per day, yaani chini ya Tsh. 2200/- kwa siku, wengi hawana ajira rasmi hivyo benki haziwezi kuwakopesha, kifupi hatukopesheki kwa sababu ya nature ya ajira zetu.

Kwa kuanzia, kungekuwa na sheria ngumu za ujenzi na umiliki wa ardhi, upimaji wa ardhi. Kuna nchi zinaruhusu individuals kujenga, hasa suburbs(nje ya mji), lakini sheria zake huwezi tu kujiamulia na fundi nyumba ikae unavyotaka, utafuata sheria za mipango miji na huwezi kufanya hata mobilization kama hujapata go ahead toka idara ya ardhi. Maana yake kuna sewage systems, drainage systems electric systems lazima ufuate sheria.

We could start implementing that, then haya ya mengine yatakuja baadae. Naamini baada ya miaka 200 ijayo, hizi nyumba zote/nyingi humu zitavunjwa ili kufuata mfumo rasmi wa ujenzi.

Nadhani serikali kupitia wizara ya ardhi kitengo cha mipango miji hasa ndio wameruhusu shant houses.
 
Mixed economy ufanye kuwa katika kila uwekezaji kuwa na nyumba 10-20 ambazo ni affordable homes maana yake zinakuwa subsidies na serikali kwa akili ya wasio na uwezo.
Huwezi kuweka watu wenye income sawa sehemu moja lazima unahitaji service providers kama cleaners, supermarket attendants au restaurant waiters.
Ikiwezekana kwa serikali kuwa na subsidy homes kwenye kila uwekezaji itakuwa ni jambo zuri lakini tunaposema neno ''affordable'' tunageneralize mnooo.Tumeshuhudia NHC wakijenga nyumba za gharama nafuu kisha kuuza kwa mil.50 mpk mil 88 sasa unajiuliza unafuu wake ni nini ???Je mtz wa kawaida anauwezo wa kuwa na hizo pesa kununua hiyo nyumba ???Okay poa anaunganishwa na benki apate mkopo...je ataweza kuservice huo mkopo kwa kipato chake au biashara aliyonayo kwa muda wote wa mkopo ??
Well niu ngumu ila Hatuna haja ya kungoja uwekezaji wa kutoka nje nadhani hawahawa NHC wangekuwa imara wangeweza kubadilisha taswira ya makazi kwa watz wengi wa hali ya kawaida.Wawe wabunifu na wajikite kwa watu wa kawaida masky scrapper sijui na mashopping malls/towns viwepo ila iwe ni baada ya kuwainua hawa wa kawaida.
 
Kwa Bongo haiwezekañi sababu mifumo ya takwimu haieleweki.

Hakuna mtu anajua mishahara na kipato kwa ujumla cha wananchi, mishahara bado ni duni sana, makampuni ya ujenzi hayako serious kwenye kazi majengo na ujenzi mwingi uko chini ya kiwango. Mfano kuna ghorofa inaitwa Uhuru heights ukifika floor ya nne nenda vyooni uone subastandard doors, sinks kila kitu mpaka milàngo. Au nssf mkapa tower nenda ground floor toilet hata taa zilishakufa kila kitu ni chini ya kiwango havina ubora.
Ardhi yetu nyingi haijapimwa na haina hati, Tamaduni za mtanzania hapendi kuishi kwenye jumuiya kama kota ni lazima zizingatiwe sababu watu wanapenda kufuatiliana maisha ya wenzao yasiowahusu.
Benki zetu zimeweka interest rate kubwa sana hivyo collateral down payment haiimiliki kwa mkopaji.
Urasimu kwenye mamlaka kurasimisha ujenzi mfano Building permit kuna bureaucracy, soil analysis inafanyika sehemu chache sana tanzania Bico na few approved consultancies.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eneo kama Kawe Tanganyika packers ground likipangwa vizuri tutajua kweli NHC wana uwezo kwenye sekta. Sioni sababu ya serikali kutokutenga stendi kubwa ya mabasi ya jiji na kwenda mikoani hapo kawe opposite na Feza schools. Wajenge Bus Terminal itakayo include rail terminal kama Mombasa. Full Automated systems hakuna mkatisha tiketi, una punch kadi tu haya mambo ya wauza mahindi,wapiga debe,madereva deiwaka kujaa vituoni tuyaonee aibu waswahili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cha muhimu kabisa ni kuwa na sheria imara za ujenzi. Real estate ni muhimili mkuu sana wa uchumi.

Wakati sheria zilipokuwa zinafuatwa miji kama Tanga na Dar ilijengwa kwa mpangilio mzuri sana.

Tanga ina barabara zimejipanga moja mpaka 21 baadae ndio yakatokea maeneo ya hovyo hovyo kama Kwanjeka.

Kwa Dar nyumba za Ilala, msimbazi kota, na Magomeni mapipa mpaka leo kuna sehemu mabaki ya lami ya mkoloni bado ipo.

Mikopo ya THB ilianza kutolewa zamani sana. Inahitaji marekebisho tu. Benki zinatakiwa kutoa mikopo kwa dhamana ya nyumba ambazo tayari zimejengwa katika kiwango kizuri na thamani inayoeleweka.

Tusiseme watanzania hawana uwezo wakati nyumba za Dar zimekuwa zikiuzwa milioni mia mbili mpaka milioni mia kwa muda mrefu sana.

Wafanyakazi wanapanga vyumba kwa kodi za milioni mbili.

Huko mabondeni watu hawapangi nyumba wanapanga chumba. Ina maana nyumba ya vyumba sita inaingiza zaidi ya laki mbili kwa mwezi.
 
Tofauti ni mwenzio wa Marekani anauziwa nyumba ina jiko, friji, microwave, carpet mpya na imefanyiwa inspection wewe unauziwa nyumba iko hivi:
fa2d0d0652bc536c04e2bceceb184c32.jpg
 
Nipe jibu yakinifu, hayo makampuni yanajenga hizo nyumba kwa hela toka wapi?

Ni pesa za kampuni. Mtu yeyote akiwa na mtaji anaweza kuanzisha kampuni ya ujenzi. Kumbuka wako kibiashara hawalipwi mishahara na serkali kama NHC.
 
Back
Top Bottom