Makampuni ya simu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makampuni ya simu.

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Kivia, Dec 16, 2010.

 1. K

  Kivia JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Makampuni ya simu, yameshusha gharama saana za kupigia simu ndani ya mtandao na hata kwenda mitandao mingine. Ukifikiria kule tulipoanzia wakati vocha zinauzwa kwa Dollar na leo hii hadi zinatozwa kwa senti ni mabadiliko makubwa. JE HUDUMA HII INAWEZA KUWA YA BURE MIAKA IJAYO ??.
   
 2. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2010
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,121
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Bure? Sasa kampuni zitajiendesha vipi? Pia kushaka kwa bei ni kwa sababu ya competition kubwa sana, nadhani sooner or later kuna kampuni zitashindwa kukeep up na zitakufa au zitanunuliwa, hapo bei itapanda tena. Kwa wawazo yangu kuna wanaooperate at a loss ili kukamata market share.
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,927
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Katika kila shilingi mia moja unayotumia katika serikali inapata kodi ya karibia shilingi 30. Sasa wakati tariff ikiwa shilingi 5 kwa sekunde, ina maana serikali ilikuwa inapata shilingi 1.5 kwa sekunde. Kwa tariff za sasa za nusu shilingi ina maana serikali nayo inapata kodi ya senti 15 kwa katika sekunde ya maongezi. Sasa kama muda wa watu kutumia simu hautaongezeka elastically kuendana na kupungua kwa bei, unaweza kuona sio makampuni tu yatapoteza, hata mapato ya kodi kwa serikali yatapungua significantly.

  Hata hivyo kwa sie 'kunguru' vita vya 'panzi' ni neema kwetu!
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ilikuwa ni dollar, afu shilingi 360 kwa dakika, uwe umeongea sekunde moja au sekunde 59. Mpaka leo wengi bado wanaita vocah 'dola'.

  Ila message zilikuwaga bure (kwa voda ilipoanza)
   
 5. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280


  wacha ya pungue kwani sioni faida yake, serekali kila siku inakopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, kodi zetu wananywea chai na kupeleka viduku vyao nje ya nchi!
   
Loading...