Makampuni ya simu yameongeza gharama za makato katika huduma za kifedha, Serikali iingilie kati unyonyaji huu

Scars

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
44,314
105,143
Jana usiku nimetumiwa meseji majira ya SAA 4 kuwa ifikapo saa 6 usiku kutakuwa na maboresho kwa upande wa Tigo Pesa.

Nilitegemea kuona maboresho ya sasa yatakuwa yanamnufaisha mwananchi na sio ukandamizaji ambao umekuwa ukiwadidimiza wananchi

Hapo awali kabla ya update ya jana ilikuwa ili upate sh.10000 utakatwa 1400, kwenye 20000 walikata 1700, na kwenye 50000 walikata 2650

Angalia hii statistics baada ya maboresho ya jana. Ili upate 10000 utakatwa 1450 (hapa wameongeza 50)

Ili upate 20000 utakatwa 1750 (150 imeongezeka) halafu kwenye 50000 utakatwa 2700

Nakumbuka mwaka 2015 makato ya huduma za kipesa kwenye mitandao karibia yote ilikuwa na mienendo mizuri ambayo kila mwananchi aliweza kui-afford

Kwenye shilingi 10000 walikuwa wanakata 800 lakini haya maboresho ya jana ni kisanga aisee
 
Haya makampuni yanatumia gharama kubwa sana kutangaza huduma mbovu. Oligopoly na duopoly theories haziwasaidii.
Mitandao yote hovyo, udhibiti hovyo.
 
Hata hivyo tunalalamikia tu kwenye mitandao hakuna wa kukusikiliza, nchi za ukanda wa Afrika mashariki wananchi wake hawana uhamuzi zaidi ya kuongea na kuandika sana.

Hata zile taasisi za watetezi wa watumiaji viongozi wake wanasoma haya yote wakifunguka wanaitwa wanapewa bahasha na kusema tunafanyia kazi au pia wanaogopa 😷!
 
Mkuu cheki vizur wameongeza shs 50/= na sio 150/= Kingine hamia kwenye mobile banks.
Hapana mi ndio nimekosea kuandika, hapo awali ilikua 700 ila baada ya maboresho imekua 750
 
Hayo makampuni ya simu utayoonea bure wenyewe wanapokea maagizo kutoka BOT

Hata riba za mikopo ya Bank wananchi wanalalamika kuwa ni kubwa lakini ukweli ni kwamba Bank zinafuata maelekezo kutoka BOT

BOT ndio mchawi wetu
TBS

TANZANIA BADO SANA
 
Haya makampuni yanatumia gharama kubwa sana kutangaza huduma mbovu. Oligopoly na duopoly theories haziwasaidii.
Mitandao yote hovyo, udhibiti hovyo
Nashangaa sana serikali inawakalia kimya hawa manyemela. Nashindwa Kuwatofautisha na wale wa ile pesa tuna kwenye namba hii
 
Kutoa bank ndo nuksi... Wanakamua ka mashetani.

Hawafai.
Daah inakua ka' hakuna pakukimbilia. Lakini juzi hapo nimeskia WhatsApp wametangaza kuweka huduma za kibank ambapo hakutakua na makato yeyote ile
 
Hata hivyo tunalalamikia tu kwenye mitandao hakuna wa kukusikiliza, nchi za ukanda wa Afrika mashariki wananchi wake hawana uhamuzi zaidi ya kuongea na kuandika sana.

Hata zile taasisi za watetezi wa watumiaji viongozi wake wanasoma haya yote wakifunguka wanaitwa wanapewa bahasha na kusema tunafanyia kazi au pia wanaogopa 😷!
Nikwasababu nchi yetu haijali kero zetu, nakumbuka kipindi ambacho dangote alileta cement yake akitaka iuzwe kwa shilingi 5000 lakini serikali ikamkatalia kua lazima auze kwa bei ambayo wengine wanauza.
 
Scars,
Kwahiyo tukimbile Airtel sio? Basi sawa, nikikuwa siweki na kutoa pesa kwa mtandao wowote zaidi ya tigo, ila kwa sasa naenda airtel. Ninachohisi ni kwamba kila Kampuni ya simu imeombwa ichangie pesa za Uchaguzi, hivyo hata wakipandisha serikali itakaa kimya tu.
 
Back
Top Bottom