Ndoa kati ya Kampuni za Mawasiliano na Serikali kuhusu tozo ni kichomi kwa Wananchi

Nawaandikieli

Member
Aug 20, 2021
9
2
Ndoa kati ya kampuni za mitandao ya simu na serikali inayohusu tozo kwenye miamala mbalimbali inayofanywa kwa njia ya simu, pamoja na ndoa kati ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) zimekuwa ni ndoa kichomi kwa wananchi kutokana na mlundikano wa kodi anazokutananazo Mwananchi katika kila shughuli anayoifanya moja kwa moja ili kujipatia kipato ama katika huduma za kijamii kama usafiri, maji, nishati ya gesi manunuzi ya bidhaa mbalimbali za dukani na sokoni kama mahitaji muhimu ya kila siku.

Nia na madhumuni ya ndoa hizo ni kuiwezesha serikali kukusanya mapato kwa ajili ya maendeleo, lakini kwa mtazamo wangu mwananchi huyu anakamuliwa pakubwa mno ikilinganishwa na kipato chake ambacho nacho kina makato pia. Nashauri serikali kupitia Wizara ya Aridhi kuona namna ya kurasimisha makazi ili kuweza kupata idadi kamili ya zipi ni nyumba za makazi na zipi ni nyumba za biashara. Ni kiasi kikubwa cha pesa kinapotea kwa kutorasmisha nyumba hizo. Kuliko kusumbuka na shilingi 1000 kwenye kila mita ya umeme kila mwezi, kuna uwezekano mkubwa wa kupada pesa zaidi kwa kutambua nyumba za biashara na kuzitoza kodi za biashara.

1629459935889.png
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom