Makampuni ya Kigeni Hayalipi Kodi ya Mapato? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makampuni ya Kigeni Hayalipi Kodi ya Mapato?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DSN, Apr 17, 2011.

 1. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Nimekuwa nikijiuliza mbona makampuni mengi ya kizalendo hayabadilishi majina kama yanavyofanya makampuni mengi ya kigeni yanayoendesha shughuli zake hapa nchini.Nimegundua makampuni mengi ya kigeni ni wakimbiaji wakubwa wa kulipa kodi [Tax evador].Makampuni hayo yanakimbia kulipa kodi kwa kuyafanya makampuni hayo yaonekane kama yamepata wamilki wapya,ama wakati mwingine yanajitetea kuwa hawa kutengeneza faida kipindi kilichopita.

  Nani yuko ndani ya seriklali yetu ambae kazi yake kubwa ni kuakiki kwa ukweli makampuni haya ya kigeni hayatutendei michezo michafu ya kibiashara ya kubadili umilki wa kampuni.?

  Natamani kujua ni jukumu la nani kujua kampuni gani imezalisha nini, imepata faida kiasi gani, na imelipa kodi kiasi gani?

  zamani nilikua naona milki ya makampuni machache haswa ya migodini yakipenda kubadili umilki wa kampuni moja kwenda nyingine tena wakati mwingine bila kuiambia Serikali. Lakini mchezo huo umeingia mpaka makampuni ya kawaida ya uzalishaji na utoaji wa huduma.

  Ni Jukumu la nani kuona Watanzania hawaibiwi?
   
 2. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Japo hakuna ugunduzi wowote uliofanya na kudai umegundua, ngoja nikushauri! Iwajibishe serikali ndio imeshidwa majukumu yake! Kampuni ni za hao hao viongoz mafisadi, walitunga sheria za kodi zenye kuruhusu upenyo wa kukwepa! Wanacho fanya ni ''tax avoidance, sio evasion''
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Jomba habari ndio hyo hawalipi hata sent, iwe voda na wezake tz kwa huu mfumo ni shamba la bibi
   
 4. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni kwamba tunaibiwa laskini si kwenye kubadili majina ya makampuni, nitaelezea vile nijuavyo
  1. Kwanza uuzwaji wa kampuni huwa unaambatana na uhamishwaji wa hisa, kuna kodi za kulipa wakati wa kuhamisha hisa bila kulipa kodi hizo uuzaji huo unakuwa haujakamilika
  2. Kile tulichozea kukiita tax holiday ukweli ni kwamba hakipo katika mtazamo ambao wengi wanafikiri - yani kampuni kufanya kazi kwa miaka labda minne halafu wanauza kampuni kisha mmiliki mpya naye hupata hiyo tax holiday, ukweli ni kwamba kilichopo ni investment allowance ambayo hata mnunuzi ili anunue biashara hiyo atahitaji kujua kilichowekezwa kwa usahihi na anapokea kijiti pale mwenzake alipoishia kwakuwa sio uwekezaji mpya.
  3. Umesema pia ni kwanini makampuni ya kwetu ya wazawa hayanunuliwi au kubadilishwa majina, hiyo inatokana na ukweli kwamba makampuni yanayokuwa kwenye nafasi kubwa ya kununuliwa kwenye uwanja wa kimataifa ni yale tu yanayofanya shughuli zake kimataifa na mitandao yao ya kibiashara pia niya kimataifa, cha msingi ni tra kuwa macho na kukusanya kodi pale inapostahili kwa manufaa ya wananchi.
  4. Swala la kampuni kupata faida au hasara hilo lipo ndani ya uwezo wa tra, kuna wasomi wapo huko tatizo ni ufisadi uliokubuhu katika nchi yetu, ukweli ni kwamba hao wataalamu wakiamua kufanya kazi kwa uthabiti kodi itakusanywa - labda Tanzania ianzishe sheria ya kuua hadharani mafisadi na wala rushwa na itekelezwe kwa vvitendo ndipo utaona mageuzi makubwa katika idara hizi za ukusanyaji wa mapato
   
 5. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Wanayofanya ni Tax Avoidance sio Tax Avasion.
  Tax avoidance inafuata sheria zote za nchi, Google mwaka jana wame-avoid zaidi ya $3 BILLION in Taxes kwa kuhamisha profits zao Ireland na Bermuda ambapo hakuna Tax. GE baada ya kupata $14 BILLION profit wamelipa $0 (Zero) Taxes Marekani.
   
 6. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tutafika kwa hili la makampuni kukwepa kodi alihitaji ugunduzi wala utafiti wowote kwa Mtanzania, kujua kuwa tunaibiwa.Kaa chini na Watanzania wanaofanya kazi uhasibu [Accountancy] katika mashirika binafsi ya kigeni yanayotoa huduma na yanayoendesha shughuli za uzalishaji fanya nao mazungumzo ya kawaida utakayo yasikia ni vichekesho na maumivu ya mjamzito.

  Wafanyakazi wa idara hizi mauzo, uhasibu na uzarishaji [Sales, Accountancy na Production] wanajua kiwango gani haya makampuni yanaingiza pesa na gharama kiasi gani yamatumia kwenye uzarishaji. Wengi wanaangaikia mkate wa watoto wao wanajua lakini wafanye nini?Hata kama wanajua mfumo wetu sio shirikishi [Supportive] kuhakikisha mtoa taarifa hadhuriki na wao wapewa taarifa za ukwepaji wa kodi kodi. Pia hawajui hata pakuanzia na hata wakati mwingine hata wazo la kuhusisha ukwepaji huo wa kodi ile ni anaibiwa yeye kama mtanzania japo ni mwajiriwa bado halipo.
   
 7. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Hii sio haki, iweje wao wasamehewe? Mbona cc tukianzisha biashara hatupewi hiyo tax holiday? Shamba la bb
   
Loading...