Samahani Ndg. zangu kwa uelewa wangu mdogo labda ni kwa uchache wa elimu niliojaaliwa, ila kwa mtazamo wangu VETA kutoa gawio kwa Serikali ni upopoma ulio pitiliza Katika kujipendekeza.
Nasema hivyo kwa sababu ninavyojua mimi ni kuwa VETA ni miongoni mwa taasisi chache za Serikali katika sector ya elimu zilizo pewa upendeleo kwa kupata fedha moja kwa moja kutoka Katika chanzo kikuu cha mapato ya Serikali ambacho ni kodi za wananchi kupitia TRA.
Lengo likiwa ni kukuza sector ya elimu ya kujitegemea na kutengeneza daraja kwa vijana walio kosa fursa za kuendelea na elimu ya kawaida
Sasa unaporudisha gawio serikalini kutokana na kile unachoona ni surplus ya mapato yako ambayo umepata kutoka katika mfereji wa mapato ya moja kwa moja kutoka Serikalini maana yake ni nini??? Basi bora wafute SDL isiwepo tujue moja
Tunasahau kuwa leo TRA inatumia resources za serekali Kuu kukusanya pesa kwa niaba ya VETA halafu kesho eti unatoa gawio Kurdisha Serikali Kuu huu si ni kama mchezo wa pata potea hii imekaaje jamani???
Hivi ni kwa kiwango gani cha elimu ya VETA kimekua kikubwa kiasi cha kutosheka na kurudisha pesa serikali kuu??? vifaa vyenyewe vya kufundishia ni majanga acheni hizo bana mnatuzingua sasa.
Kwa nini leo taasisi za elimu hawalipi SDL kwa wafanyakazi wanaoajiriwa na taasisi hizo??? Jamani mbona kama tunazidi kujipendekeza mpaka inafikia mahali unatoa gawio mfuko wa Kulia na kujiwekea mfuko wa kushoto ili iweje ???
Kujipendekeza kwa sataili hizi jamani kumezidi sana, inafikia mahali tunasahau mpaka dhamira za uhai wa taasisi zetu kwa kumfurahisha bwana yule, huku Sasa ni kuumizana
Haya tena nyinyi ndio mlioshika mpini si wachoma mahindi wacha tuwapigie makofi kwa upuuzi huu hakika huu ni upuuzi uliopitiliza
Mnyanyembe wa Mboka
Karibuni Mahindi ya kuchoma
Stendi Kuu Unyanyembeee!!!
View attachment 1289935
Sent using
Jamii Forums mobile app