Makampuni 27 ya Uchimbaji Tanzanite Arusha, Manyara na K'Njaro kufutiwa leseni kwa Ukwepaji Kodi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Jumla ya Kampuni 27 zinazojihusisha na uchimbaji wa madini ya Tanzanite Mkoani Arusha zitanyang'anywa leseni kwa sababu ya kushindwa kulipa kodi.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama kwa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Amos Makalla amebainisha kuwa uchunguzi unaoendelea unaonyesha kuwa makampuni ya uchimbaji madini yanahusika sana na wizi ukwepaji kodi.

Kamati hiyo ilikutana kuanzia tarehe 10 mwezi Disemba mpaka tarehe 17 kuongelea suala hili.

Makalla amesema kuna wachimbaji takribani 5,000 wanajihusisha na uchimbaji wa Tanzanite na madini mengine ya rangi. Amesema wachimbaji hao wanahusishwa na ukwepaji mkubwa wa kodi wa bilioni.

Amesema kuwa makampuni mengi yanapata faida kubwa lakini hayalipi kodi, alisema Makalla.

Kufuatia hali hiyo mamlaka za mikoa husika zimetoa muda mpaka Januari 5, makampuni yote kuweka vitabu vya mahesabu sawa na kulipa kodi zilizokwepwa.

Muda huo mpaka Januari 5 pia wamepewa raia wa kigeni waliovamia kwenye machimbo na kujihusisha na shughuli za uchimbaji bila kuwa na vibali. Amewataja Raia hao wa kigeni kuwa ni wale wanaotokea nchi za India, Congo na Kenya.

Wiki iliyopita Mfanyabiashara mwenye asili ya India alikamatwa katika Uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) akijaribu kutorosha madini ya Tanzanite yenye thamani ya Dola laki Tatu.
 
Good nyuzi Tanzanite africa ya BABA MENGI haitakosa maana huyu jamaa amekuwa mbabaishaji , kampuni imeanza 2006 lakini mpaka sasa eti wao wanajifanya ni wachimbaji wadogo waodogi ili wasilipe kodi na kulipa watu kama vibarua huku wakivuna kilo za Tanzanite na kwenda kuzifanyia labling INDIA
 
Hizi habari ni chungu kwa Chadema maana hizo kampuni nyingi ni za wafuasi wa Chadema Arusha kweli kukamua majipu siyo kazi ndogo.
 
Hizi habari ni chungu kwa Chadema maana hizo kampuni nyingi ni za wafuasi wa Chadema Arusha kweli kukamua majipu siyo kazi ndogo.

Cant you write without mentioning CHADEMA OR Hon. Mbowe just for once in your life?
 
Hao ndiyo wafadhili wakubwa wa Lema.
Basi tena ndiyo imekula kwao hapa kazi tu.

Si uwa tunaambiwa Arusha kumejaa mabilionea wa madini sasa inakuaje wanakwepa kodi.

Huu uzi uwezi kuwaona wafuasi wa Chadema..Ahahahhaha
 
Good nyuzi Tanzanite africa ya BABA MENGI haitakosa maana huyu jamaa amekuwa mbabaishaji , kampuni imeanza 2006 lakini mpaka sasa eti wao wanajifanya ni wachimbaji wadogo waodogi ili wasilipe kodi na kulipa watu kama vibarua huku wakivuna kilo za Tanzanite na kwenda kuzifanyia labling INDIA

Tumshukuru Mungu kwa kutuletea Prof. Muhongo.

Atawadhibiti wakwepa kodi, tutaifaidi wote keki ya taifa siyo kuliwa na "wazawa" wachache.
 
Makamanda kumekucha tena huko Arusha watu wanakwepa kodi tushirikiane kuisaidia serikali yetu kuwafichua wakwepa kodi adui wa Tanzania ni Watanzania wenyewe.
 
Makamanda kumekucha tena huko Arusha watu wanakwepa kodi tushirikiane kuisaidia serikali yetu kuwafichua wakwepa kodi adui wa Tanzania ni Watanzania wenyewe.
Makontena vipi mmeshalipia.
 
To the political forum you want us to write it?

Which forum is this? is it not political forum? you can convey your message and reach out without mentioning those things, when you keep mentioning all those things in almost every post it shows that you have your own problem connected to what you mention and not otherwise. Lets be critical and discuss issues and not people it wont lead us anywhere as a nation
 
Here they discussed only politicians, as the spirit is hurting very sorry mentioned Mbowe.
 
Nyumbu wa lumumba bana,Mnarukaruka kama maharage makavu, Lema, chadema inawaumiza sana ee, ile list ya wauza unga bado mzee wa msoga ameikali, wamiliki wa makontena nao hawajulikani hayo hamyaoni. Njooni na ushahidi kwamba wanakwepa kodi sio kuja na maneno matupu, mmenyang'anya mzungu tanzanite one kwa wivu wa kipuuzi leo imewadodea, na bado LEMA ataendele kuwa mbunge wa Arusha hata mfenge migodi yore ya tanzanite.#LemaforArusha.
 
Hakika Mabillionaire wa Arusha wote chaliiiii...makamanda chaliii
 
Hizi habari ni chungu kwa Chadema maana hizo kampuni nyingi ni za wafuasi wa Chadema Arusha kweli kukamua majipu siyo kazi ndogo.
Mwaka huu futari mtazitafunia msoga na kwa dr dau usije ukajisahau ukaenda ikulu na ndizi kama ulivyokuwa unafanya miaka kumi iliyopita utatolewa puta mpaka huo msuli unaovyaa uvuke
 
Hizi habari ni chungu kwa Chadema maana hizo kampuni nyingi ni za wafuasi wa Chadema Arusha kweli kukamua majipu siyo kazi ndogo.
Ritz weka vielelezo kusuport post yako, hakuna cha kujificha mwenye jipu akiwa ccm, cdm,act nk lazima akamuliwe.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom