Makame Mbarawa aiwakia ATCL

Haha..Hawa watu wanaumia sana precisionair kuruka kwa mafanikio. Wameiga sana vita kwa kila namna, sasa wameamua kabisa kununua ndege kwa akili zao. Shida ni ktk ajira, niliwaambia watu, kubagua kanda yenye mafanikio ni kujiumiza. Tatizo jingine ni utawala uliopo ndio kabisa,una hofu na kanda ya kaskazini, kila angle wanaogopa kivuli cha hawa jamaa. Ktk siasa wanaogopa watahujumiwa, ktk Ndege wanaogopa watahujumiwa eti precisionair itapewa chapuo, ktk mawasiliano hivyo hivyo.Mwisho wa siku ni kuweka watu wanaofanya maigizo kila angle. Hii nchi ipo siku itakabidhiwa kwa wachapa kazi kiroho safi, wabaguzi watakuwa chalii wenyewe.
 
Wazalendo tupi tena wengi tu tutazioanda. Nakumbuka niliwahi kufanya kazi navwaswed. Ole wako umkatie tiket nyingine zaisi ya Aitr Tanzania. Lakini waTanzania wenyewe kawana mwanzo mwisho dah.
Aisee ulikua usingizini?
 
Mnakosea sana kudhani mchawi ni hao sekta binafsi. Yaani serikali ina usalama wa taifa unadhani wasingejua wanahujumiwa?

Mashirika ya uma yanakufa kwa sababu mbili kuu. Mosi, serikali haipaswi kufanya biashara maana cha wote hakina mwenyewe (lack of ownership). Pili hakuna ile kujituma kupata faida sana kwa maana ruzuku itatutoa tukikwama au hakuna mshindani.

TANESCO haina mshindani toka sekta binafsi mbona iko hoi miaka yote kukimbilia kupandisha bei bila ya kuboresha huduma? Kutwa kucha inaliwa kila kona. Why? Cha wote hakina mwenyewe na hata iliwe vp kuna ruzuku kufidia hasara.

Tusipende kulaumu sekta binafsi wakati upuuzi unaondelea serikalini kuna mazuzu kazi kusifia tu. Mashangingi. Ndege. N.k.

Serikali kazi yake iweke mazingira wezeshi na sawa kwa sekta binafisi kushindana. Hapo sisi walaji ni full bata kuanzia ubora viwango bei upatikanaji uhakika thamani n.k.
 
Wazalendo tunasema hakuna sababu kununua midege kwa taslimu wakati kuna ya msingi kufanya. Shirika lifutwe tu au mtaji utaobaki baada ya madeni wawekeze precision.

Serikali hina haja kufanya biashara ya usafiri. Ni upuuzi tu huo. Wajifunze toka mataifa menginewe. Walioendelea (na pengine ndo maana wameendelea) hawana hayo mashirika. Swissair waliuza lao kitambo.

Wanaojikongoja wanang'ang'ania ufahari kuwa na ndege na kushindia hasara. Kenya SA Rwanda Misri n.k. wote hasara.

Na Magu badala hata ya kwenda kujifunza Ethiopia, anaenda kwa walioshindwa. Tangu waanze Rwandair hawajawahi kupata faida. It's time before hawajafunga virago na wataanza ATCL then Rwandair.

Kinachowashinda kuwekeza kwa Precision ni nini? Au hata Fastjet.
 
Bila IT na Marketing kushirikiana na kuweka mfumo friendly and Transparent,wapigaji wataendelea kupiga milele.
Zote hizo ni sawa na kufunga Ac chumbani ili utumie blanketi kama kwenye bongomuvi. Kisha unaanza kutafuta dobi mzuri kufua mablanketi na fundi mzuri kuhudumia Ac.

Hasara inaanziaga kwenye wazo halafu inatengeneza mfumo wa domino kwenye utendaji.
 
Wasitumie nguvu. Wawekeze kwenye anaeweza au waachane na kuendesha biashara ya ndege.

Kama ni kukuza utalii, nchi zenye utalii mkubwa sana wala serikali zao haziendeshi mashirika ya biashara ya ndege. Marekani, Ufaransa, ujerumani, n.k. Tuige walio mbele. Sio makapuku wenzetu.

Kuna shida kubwa sana kwenye mfumo wa mawazo wa wanaowashauri watawala. Wanawazia zama za ujima bado. Mara kulazmisha watu kupanda ndege na upuuzi mwingine mwingi tu.
 
Marketing department ifanyiwe kazi ikiwezekana ifumuliwe,kusiwepo na ufanyaji wa kazi kwa mazoea.
Guys... spare your efforts. Hakuna sababu ya msingi serikali kuwa na hilo shirika. Iwe usalama, utalii, n.k isipokua tu labda ufahari. Na hatujitaji ufahari kwa sasa
 
Taja sababu walau tatu tu za kwanini ni lazima kuwa na shirika la kibiashara la ndege linaloendeshwa na serikali
 
Japo umeiweka kiukabila ila nakuunga mkono kuna kihoro kikubwa kwa serikali kuipa flag Precision. Na kiko so unfounded. Sana sana na hearsays.

Kama ndivyo, watuokolee hasara (kupoteza kodi zetu kwa mishahara iso tija na ruzuku zisoisha) wafunge hiyo biashara na kupea private sector uwanja huru watoane jasho. Kwetu itakua faida tu.
 
yani watu wanavyolalamika mpaka naogopa kupanda, nimebook hii ndege lakini nilipoomba kucancel route nikaambiwa nitakatwa elf 50 kwa kichwa kwa route, nilibaki kama nimepigwa shot ya umeme
 
Ndugu zanguni ndege hazitaki mchezo...
Ni afadhali tusiwepo na shirika la aina hiyo kuliko yatokee kama ya ADAM AIR.
Ni busara watu wa NTSB waanze kufanya pre investigation ...kabla ya jambo litarajiwalo...Mungu aepushie mbali.
 
yani watu wanavyolalamika mpaka naogopa kupanda, nimebook hii ndege lakini nilipoomba kucancel route nikaambiwa nitakatwa elf 50 kwa kichwa kwa route, nilibaki kama nimepigwa shot ya umeme
Mkuu we si ulitaka Kwenda FastJet au Precision Air? Ndio wanaiandaa kuwa Monopoly polepole...
 
Mamilioni ya dola yamepotea kisiasa.
Magu ana vita na raia wake anataka maisha yao yawe magumu hapohapo anataka tumuungishe kwenye ndege zake, never.
Huweza kuwa na ugomvi na wateja halafu unategemea faida.
 
dah mi hiyo pesa ya ndege wangeipeleka kwa reli naona tungepata faida mara dufu tofaut na hy ndege maana hatuna hata kipato cha kupanda hzo ndege bali tungewachia sekta binafsi kujihusisha huko tu..sisi mwend wa kodi tuu
Reli nayo sio mchezo Mkuu; inatakiwa kujipanga hasa. Hiyo hela iliyonunulia ndege sijui hata kama ingetosha standard gauge ya reli kutoka Kituo cha Station - Dar hadi Pugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…