Makamba: Uongozi ni koti la kuazima

Makamba: Uongozi ni koti la kuazima

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,162
Reaction score
162,594
Gazeti la Mwannchi la leo Disemba 30,2017, limeandika au kwa lugha nyingine limenukuu tweet ya jana ya Waziri wa Muungano na Mazingira, bwana January Makamba.

Tweet husika inasomeka:

"Uongozi ni koti la kuazima.Kuna wakati utarudisha tu.Kama ulikuwa unawakoga nalo watu,likirudi unaadhirika."

Makamba amekiri kuwa hiyo tweet ni yake baada ya kuulizwa na gazeti la mwananchi.

My take:

Mwisho wa siku kila mtu mtumuona adui au mpiga dili kumbe maadui na wapiga dili ni nyinyi wenyewe na kikundi chenu cha watu wachache.
 
Karibu tena kwenye kuanzisha uzi
Naona la Kabobe mliyemtuma limewatokea puani.. eeeeh

Ni kiongozi na hayo ni mawazo yake yeye alivyotaka kuona hayo.
 
Hao mwananchi wanajua jinsi ambavyo chadema hufarijiwa na tweet za aina hiyo ndio maana wameileta kama ilivyo laiti ungekuwa unafatilia ungeenda kwenye account ya J Makamba uone alikuwa anaongea na nani na kwanini alisema hivyo?

Hiyo tweet alikuwa ana mjibu mchngiaji fulani kwenye twitter aliye muuliza mbona yeye aonekana kama ni kiongozi?

Kwakuwa Chadema mnaugonjwa wa kusahau na mnahitaji faraja basi mtaanza kumuita Kamanda teh teh teh.......
 
basi kuna jamaa kaazima koti amesahahu kuwa ni la kuazima_mkumbusheni
Wengine huwa ni wagumu mno kurudisha koti la watu hadi waporwe kwa nguvu!! Kuna jirani yetu pale karibu na ferry ameshaanza kushona sehemu zilikuwa na vifungo!! Yaani badala ya vifungo yeye anashona kabisa,anadai eti vifungo vinamchelewesha kufungua na kufunga,sasa siku atakayotakiwa kuvua sijui itakuwaje! Na anasema kuwa koti alienda kuazima mwenyewe kwa hiyo hakuna wa kumpangia jinsi ya kulivaa!! Hajaribiwi!
 
Hao mwananchi wanajua jinsi ambavyo chadema hufarijiwa na tweet za aina hiyo ndio maana wameileta kama ilivyo laiti ungekuwa unafatilia ungeenda kwenye account ya J Makamba uone alikuwa anaongea na nani na kwanini alisema hivyo?
Hiyo tweet alikuwa ana mjibu mchngiaji fulani kwenye twitter aliye muuliza mbona yeye aonekana kama ni kiongozi?
Kwakuwa Chadema mnaugonjwa wa kusahau na mnahitaji faraja basi mtaanza kumuita Kamanda teh teh teh.......
Mwananchi wamesema Makamba hakutaka kufafanua kauli yake hiyo zaidi ya kukiri kuwa iko kwenye akaunti yake.
 
January ana hasira sana mzee wa aliyevaa koti.Basi tu!
 
Wengine huwa ni wagumu mno kurudisha koti la watu hadi waporwe kwa nguvu!! Kuna jirani yetu pale karibu na ferry ameshaanza kushona sehemu zilikuwa na vifungo!! Yaani badala ya vifungo yeye anashona kabisa,anadai eti vifungo vinamchelewesha kufungua na kufunga,sasa siku atakayotakiwa kuvua sijui itakuwaje! Na anasema kuwa koti alienda kuazima mwenyewe kwa hiyo hakuna wa kumpangia jinsi ya kulivaa!! Hajaribiwi!
Heshima yako mkuu kwa lugha sahihi na maudhui mazuri,ila hyo jirani yenu haoni hata haya duh
 
Gazeti la Mwannchi la leo Disemba 30,2017, limeandika au kwa lugha nyingine limenukuu tweet ya jana ya Waziri wa Muungano na Mazingira, bwana January Makamba.

Tweet husika inasomeka:

"Uongozi ni koti la kuazima.Kuna wakati utarudisha tu.Kama ulikuwa unawakoga nalo watu,likirudi unaadhirika."

Makamba amekiri kuwa hiyo tweet ni yake baada ya kuulizwa na gazeti la mwananchi.

My take:

Mwisho wa siku kila mtu mtumuona adui au mpiga dili kumbe maadui na wapiga dili ni nyinyi wenyewe na kikundi chenu cha watu wachache.

mtamzidishia mafrustration

Mara "tubu"

Ohoo "hirizi kiunoni"

sasa na huyu kaja na yake eti koti LA kuazma
 
Mnaangaika sana, ila hamjui mna deal na mtu wa aina gani, zamu hii kila rangi mtaiona. Badala ya kwenda vijijini angalau mjaribu kutetea viti vya ubunge na udiwani 2020 vipatikane hata 10 tu,mpo mnahangaika na kauli za KAKOBE. Na viongozi wenu wamesanda wapo kimya, hizi siasa za matukio zitawafanya mpate wabunge 5 mwaka 2020 msiposhtuka mkaacha kucheza kila ngoma inayoletwa.
 
Karibu tena kwenye kuanzisha uzi
Naona la Kabobe mliyemtuma limewatokea puani.. eeeeh

Ni kiongozi na hayo ni mawazo yake yeye alivyotaka kuona hayo.
La Kakobe bado linaendelea kuwateseni, wala haliishi leo. halafu si unaona na akina Askofu Bagonza wanaendeleza hilo zali...
 
Back
Top Bottom