Makamba ni mwanasiasa aliyejaa chuki na fitina | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba ni mwanasiasa aliyejaa chuki na fitina

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Luteni, Oct 26, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama wewe ni mfuatiliaji wa siasa za Tanzania nafikiri utakubaliana nami nitakachokisema. Kitendo cha hivi karibuni cha Makamba kukimbilia upesi upesi kwenye tukio la mauaji ya Maswa na kusema anauhakika Shibuda amehusika ni cha kusikitisha sana. Vilevile kitendo chake cha kufika Maswa na kumtembelea mgombea CCM na kumwacha wa Chadema Shibuda aliyekuwa anashikiliwa pia na polisi akiwa mahabusu zinadhihilisha kuwa Makamba ana siasa za fitina ugomvi na kisasi na bado ana fikra za kuona upinzani ni uadui. Inawezekana kabisa maneno yanayosikika mitaani kuwa matukio mbalimbali ya vurugu za kisiasa yanayotokea sehemu mbalimbali (Arusha, Moshi, Tarime, Musoma, Mwanza, Busanda nk) huwa yamepangwa au kupewa baraka na Makamba, na inawezekana kabisa hata tukio la Maswa lilipangwa na Makamba ili kumchafua Shibuda mpango ambao umeshindwa kufanikiwa. Niko tayari kusahihishwa.
   
 2. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,500
  Likes Received: 2,743
  Trophy Points: 280

  Hivi Makamba ana elimu gani??
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,602
  Likes Received: 4,716
  Trophy Points: 280
  Ngumbaru+Ndumba=Katibu Mkuu CCM
   
 4. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Luteni ulichoeleza ni 100% kwani hata wanachama wachache wa CCM walio waaminifu na kumfahamu Makamba kwa muda mrefu wamekuwa wakieleza wazi kuwa Mzee huyu anakipoteza chama na hafai kuwa katibu mkuu, kinyume na mawazo yao mkuu JK aliyeshika mpini ndio kwanza anazidi kumkumbatia kwani ndie ndondocha wake ambaye anaweza fanya kazi naye kuliko wengine, angalizo moja hapa muhimu ni kwamba mzee huyu yupo karibu sana na anashirikiana vizuri sana na mafisadi kama kiunganishi kwa mkulu
   
 5. S

  SUWI JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  I agree with you, halafu ana kisasi pia.... Kitendo cha Shibuda kuhama CCM kilimuuma sana siku zote alikuwa natafuta sababu. Vurugu za Maswa anahusika asilimia mia moja. Sijui amepata faida gani kwa kifo cha huyo Mtz!!!! Watu wengine wana roho za uuaji!!! I hate!!!
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh!umesema ukweli kabisa,ile kasi yake kufika eneo la tukio inatia shaka.Huyu ni mfano ya wazee wasiyokuwa na busara!!hapa ule usemi wa kiswahili unaosema "wazee wana busara" hapa unagonga ukuta,huyu mzee hana kitu kabisa kichwani mwake.Anachofanya ni zaidi ya siasa!
   
 7. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Makamba ametokea mkoa wa Tanga ambapo mamake Jk ndipo alipotokea, ili kuimarisha familia hizi mbili wakaamua kugawana madaraka ndani ya CCM na kufanya ni chama chao, wakawaingiza na watoto wao ili wadumu nacho milele.

  La hasha hawakujua kuwa wao ndio chanzo cha mpasuko na ndio hitimisho la utawala dhalimu, machozi na vilio vya waTz vipo mikononi mwao. Itakapotimu saa 12 jioni tarehe 31 Oktoba watatahayuri kuona kombe limewaachia bumbuwazi.

  Ni masikitiko, huzuni na majonzi kwa mafisadi wachache ila ni furaha ya kudumu kwa wazalendo wapenda maendeleo kwa ujumla.

  Tumia kura yako kufanya mabadiliko.
  Haiitaji zindiko wala tambiko.
  Ni busara ya werevu kuwakata kidevu.
  Shime kituoni tuwatokomezee kusioni.
  KURA yako ni yako, mabadiliko ni ya UMMA.
   
 8. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,205
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Mkuu uliyosema ni sahihi kabisa. Makamba amechukua ukatibu mkuu kwa wakati muafaka kwani amefanikisha kwa kiwango kikubwa kukishusha chama cha ccm kuzima. Na ni furaha ya kila mwanamageuzi.
   
 9. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  darasa la nne la mkoloni + jeshi
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nina wasiwasi hata wazee wengi kutojihusisha na kampeni kumesababishwa na Makamba hana busara ya kushirikisha ana ile kasumba ya 'divide and rule' wazee wamechukizwa na matamshi yake mfano kuwaita 'wahuni' bila kujali michango waliyotoa kwa taifa. Kama ni mpasuko wa chama Makamba anahusika sana, endapo chama kitatokea kugawanyika nitakuwa wa kwanza kumnyooshea kidole.
   
 11. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wacheni propaganda za kipuuzi!!! Huyu ni katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na kaenda Maswa ktk kampeni za chama chake, nyinyi Chadema munalilia kwanini hakwenda kumjulia hali mgombea wenu wa ubunge shibuda!!!! Sasa aache kwenda kumuona mgombea wao wa CCM aende kumuona wa Chadema!!! UPUUZI HUU!!!

  Kwani shibuda bado yuko CCM? Na kwanini katibu wenu mkuu wa Chadema asiende kumjulia hali Shibuda ila munamuomba Makamba akamjulie hali? Katibu mkuu wa Chadema yuko wapi? Hivi Chadema mbona mumekuwa kama vitoto vidogo vinavyolilia pipi?

  Shibuda kama aliwachochea mashabiki wake wamuue dereva wa CCM na yeye kukamatwa kwa kuhusika na mauaji hayo inakuwaje tena munataka Makamba akamjulie haliShibuda gerezani?

  Mimi na hakika huyu Shibuda anamkono ktk mauaji haya ya dereva wa CCM hivyo jeshi la Polisi limkamate na kumfikisha mahakamani kujibu kesi ya mauaji!!!
   
 12. P

  Paul S.S Verified User

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu mimi nadhani uwe wakwanza kumshukuru kukigawa chama iwe baraka kwa wapinzani
   
 13. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Matamshi yako ni mwendelezo wa siasa za fitina ninazozizungumzia.
   
 14. P

  Paul S.S Verified User

  #14
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Wakuu msihoji sana elimu za watu hasa kwa mtu kama katibu mkuu wa chama, na hakika wakikuhoji elimu ya mgombea mwenza wa Dr Slaa wa ukweli utapata kigugumizi
  Unajua mantiki nzima ya hii hoja haina kichwa wala miguu, sana sana inaonyesha mtoa hoja ndio ana chuki binafsi, makamba kweli amefanya mengi ya ajabu ajabu, lakini katika hili Mzee wa watu amefanya kitendo cha kiungwana na pia kuzingatia alama za nyakati, unadhani ni watu wangapi wa huko wataguswa na ujio wa Katibu mkuu wa chama ktk msiba, wakati CHADEMA hata kutoa tamko tu imekuwa shida
   
 15. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,655
  Likes Received: 21,868
  Trophy Points: 280
  Makamba ana elements zote za watu washirikina.
   
 16. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  ana pihechi dii ya theology
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,602
  Likes Received: 4,716
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe na Mbatia mko pamoja?
   
 18. S

  Selemani JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 26, 2006
  Messages: 871
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mzee inavyoonekana ukilala usiku unamuota Luteni yaani. Hamna hamu naye. And you add your conspiracy theories just to find a scapegoat kwa uhanithi wenu mliofanya huko Maswa.

  When u throw allegations kama hizo, u better have evidence to back it up Chief. Otherwise it is idiotic for us discuss your baseless allegations kutoka "maneno yanayosikika mtaani".

  Look, I know for a fact that Makamba is incredibly effective, na ndio maana haipiti siku bila nyie kuanzisha thread mbili, tatu kumdiscuss mtu ambaye mnasema hana elimu, na ni mropokaji. Why wasting time then kumuongelea? If he is clue less as you are all suggesting, then why spending threads, and threads discussing him and his children?
   
 19. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Originally posted by Zubeda
  Wacheni propaganda za kipuuzi!!! Huyu ni katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi na kaenda Maswa ktk kampeni za chama chake, nyinyi Chadema munalilia kwanini hakwenda kumjulia hali mgombea wenu wa ubunge shibuda!!!! Sasa aache kwenda kumuona mgombea wao wa CCM aende kumuona wa Chadema!!! UPUUZI HUU!!!

  Kwani shibuda bado yuko CCM? Na kwanini katibu wenu mkuu wa Chadema asiende kumjulia hali Shibuda ila munamuomba Makamba akamjulie hali? Katibu mkuu wa Chadema yuko wapi? Hivi Chadema mbona mumekuwa kama vitoto vidogo vinavyolilia pipi?

  Shibuda kama aliwachochea mashabiki wake wamuue dereva wa CCM na yeye kukamatwa kwa kuhusika na mauaji hayo inakuwaje tena munataka Makamba akamjulie haliShibuda gerezani?

  Mimi na hakika huyu Shibuda anamkono ktk mauaji haya ya dereva wa CCM hivyo jeshi la Polisi limkamate na kumfikisha mahakamani kujibu kesi ya mauaji!!!


  Yaani wewe ndiyo bure kabisa!siasa siyo uadui elimika,acha kuwa mjinga kiasi hicho!!kichefuchefu!!!!!!!!!!!!!!1
   
 20. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #20
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mi nadhani mda mwingine elimu si chochote ktk siasa kwani ni viongozi wangapi wenye elimu kumpita sokoine lakini hatuone wakifanyacho? Zaidi ya kuudanya umma kwa matakwa binafsi,angalia mikataba iliyosainiwa juu ya madini na rasilimali zetu nyingine ni hao hao viongozi wenye elimu ya juu ndio wametufikisha hapa tulipo,malalamiko na kilio juu ya matumizi mabaya ya elimu walizonazo,
  kuhusiana na mzee wa tanga ni kwa kuwa si mzee mwenye kupanga mambo yake yakapangika,ni mzee wa kuongea na kunukuu vitabu vya dini pasipo kujua hata mwisho wa kunukuu nini kitatokea,angalia swala la nape.mzee wa tanga aliapa kuwa mpaka mungu hata msameheekijana nape,lakini sasa nape ni mkuu wa wilaya,angalia kwa bashee mzee wa tanga alidiliki kusema kuwa kijana si raia mbele ya vyombo vya habari,lakini sasa bashee ni raia tena mwema.nadhani ni swala la busala lenye msukumo wa umri ndilo analokosa mzee wa tanga na ndio maana baadhi ya vinguke ktk chama chetu ccm hawamwitaji mzee wa tanga
  mapinduzi daima​
   
Loading...