Makamba huyo Arusha sikiliza vituko vyake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba huyo Arusha sikiliza vituko vyake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, Oct 19, 2009.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Makamba akiri kuwepo kwa makundi ndani ya chama tawala

  Hemed Kivuyo, Arusha
  10/19/2009


  SIKU chache baada ya kudaiwa kuingia katika baadhi ya majimbo na kuendesha kampeni za kuwang'oa wabunge waliopo na kuwawekea mazingira ya ushindi watoto wake; Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba amekerwa na makundi yaliyomo ndani ya chama hicho katika mikoa mbalimbali, ukiwamo wa Arusha.

  Pamoja na hayo, Makamba pia aliwafananisha na watoto wadogo wanachama na viongozi wa chama hicho ambao wamehamia katika vyama vya upinzani kwa madai kuwa mtu mzima mwenye akili timamu hawezi kuhama CCM.

  Alisema kuwa pamoja na chama hicho kuonyesha dalili nzuri ya kushinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa, bado kuna tatizo la baadhi ya wagombea wanaoshindwa katika kura za maoni ambao huhamia katika kambi ya upinzani na kundi la wanachama.

  "Mimi naona kuwaita wazee wale waliohamia kambi ya upinzani siyo sahihi, bali ni kama watoto wadogo," alisema .

  Aliwataka viongozi wa chama hicho mkoani Arusha kuhakikisha wanamfukuza mwanachama yeyote anayeonyesha dalili za kukiasi chama hicho kwa kumnyang’anya kadi ya uwanachama mapema.

  "Kama kuna mtu mnaomuona ana dalili za kwenda upinzani na kutoa siri za chama, chukueni kadi mapema na aende huko anakotaka," alisema Makamba.

  Katika hatua nyingine, Makamba alisema kuwa chama hicho kitawalipa 'posho' mawakala wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu pamoja na kuwepo kwa mawakala wengi wa kusimamia kura kwa upande wa chama hicho.

  Makamba aliyasema hayo mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa wilaya, Jubilate Kileo wakati akimkaribisha kuzungumza na wanachama waliohudhuria katika mkutano huo.

  Ziara ya Makamba mkoani Arusha ambayo ina nia ya kukiongezea nguvu chama hicho katika uchaguzi wa serikali za mitaa, umeikuta CCM ikiwa katika hali mbaya baada ya wanachama kadhaa na viongozi kuhamia kambi ya upinzani.

  Pamoja na hayo pia chama hicho mkoani hapa kimegawanyika katika makundi mbalimbali ambayo huwaunga mkono baadhi ya viongozi na wengine wakiwapinga.

  Wakati huo huo, jana Makamba aliwatoa nje waandishi wa habari katika mkutano wake kwa madai kwamba wataandika 'madudu'.

  Hali hiyo ilitokea katika Ukumbi wa chama hicho mkoani hapa majira ya saa 5:55 asubuhi. Kabla ya hapo alitoa risala kwa waandishi hao kwa muda wa dakika 10 mbele ya viongozi na wanachama wa CCM huku akishangiliwa kwa nguvu wakisema: "Kidumu Chama Cha Mapinduzi".

  Makamba alifika katika ukumbi huo saa 4:22 asubuhi akiongozwa na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Batilda Buriani na mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Mkoa wa Arusha, Elishilia Kaaya na viongozi wengine wa mkoani hapa.

  Baada ya hapo Makamba ambaye wakati fulani alionekana kutabasamu, aliangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili vilivyopangwa kumpokea na kisha kuwagawiya wachezaji zawadi za fedha ambazo kiasi chake hakikufahamika. Makamba aliingia katika ukumbi huo saa 4:34 na viongozi kadhaa wa chama hicho walianza kusoma risala mbele yake na yeye aliitikia kwa kuwalaani waliokihama chama hicho.
   
 2. E

  Eddie JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mahakamba ndio nini? haraka za kishabiki tu!
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mahakamba umeona ni kitu pekee cha wewe kuacha kujadili yaliyomo ? Hapana mie si ushabiki ila utumbo wa Makamba kila kona na CCM yake ndiyo issue hapa .
   
 4. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ushabiki wa nini sasa?uwe una heshima kwa wakubwa wako sio ili mradi umekaa kwenye li desktop lako tena croned ianaanza kujibu tu vitu..sio lazima kila kitu uchangie
   
 5. E

  Eddie JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Koma we! mkubwa wangu nani? hunijui sikujui tuliza kitenesi hicho
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  ulivyo na akili za kitoto unatukana hapa...hayo ndo madhara ya kufungwa blog yenu ya ze utamu na kuruhusu ile sheria yenu kama walivofanya wenzako wa kenya huko london
   
 7. E

  Eddie JF-Expert Member

  #7
  Oct 20, 2009
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  We bwabwa Kituko, umri huo bado unafanya biashara hiyo tu? Food for thought: peleka sehemu nyingine hiyo biashara yako,hapa hailipi! simply u r barking a wrong tree!

  Vipi wewe unakuwa kama sio mjinga!
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Oct 20, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Hapa sina la nyongeza - Mwanga husafiri haraka zaidi kuliko sauti
   
 9. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #9
  Oct 20, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Cha zaidi sauti husafiri hata katika mada yabisi..... tofauti na mwanga..
   
Loading...