Makamba funga dampo la maji chai Arusha Taswira mbaya kwa mji wa Arusha.

kijenge

Senior Member
Mar 9, 2012
179
164
Kuna wakati walikuwa wanawasha moto moshi unatanda barabara yote ya Moshi Arusha hadi gari zinashindwa kupita,na moshi kujaa kwenye maeneo ya makazi ya wawekezaji doli.Mkurugenzi amekuwa anafuatwa kuelezewa anajibu nimewaambiwa wasichome moto bila kujali kuna harufu mbaya sana na wanatupa uchafu hadi barabarani kama nilivyoona kwenye picha,Mkurugenzi huenda anamaslahi binafsi tumemlalamikia hadi tumechoka
 
Na linazidi kuwa kubwa kila uchao kwa kuwa siku za karibuni serikali za mtaa wamekataza ktumia mashimo ya taka (hata kwa wale tunaoishi nje ya jiji/migombani) na badala yake wametulazimisha kufukukia mashimo ya taka na kututaka tulipia gharama za gari la kusombea taka ambalo lilipita mara moja tu.

Ni zaidi ya mwezi sasa halijapita na hakuna taarifa yeyote. Gari naliona maeneo ya Shangarai spana mkononi kutwa/kuchwa likitengenezwa (gari lenyewe ni taka pia!!).

Linafanya kazi saa ngapi wahusika wanalo jibu.
 
Ha ha haaaaa. Umenichekesha sana mkuu kuhusu hilo gari la taka. Ki ukweli kwa hali ilivyo sasa pale hapakaliki. Harufu mtindo mmoja hata kama ni mpitaji tu, na haka kamvua kamepita basi imekuwa ndio balaa yani.

Watu wanatupa taka hadi barabarani, hamna mtu anashuka kule chini kwa ajili ya kumwaga taka aisee. Nimepita hapo leo hadi kero yani hiyo harufu. Nawaza wale waheshimiwa wa usalama barabarani wanawezaje kukaa pale?. Kwanini wasisogezewe kituo cha kukagulia magari mbali na pale?.
 
Back
Top Bottom