Makamba chunga sana, hili la viroba linakuondoa kwenye uwaziri maana umekurupuka sana

The retired soldier

Senior Member
Feb 26, 2017
104
218
Makamba umemshauri vibaya mheshimiwa Rais na Waziri mkuu. Na hii itakucost kwenye uwaziri..muda ni mwalimu mzuri sana.
Wewe na ofisi yako mlikuwa na agenda ya kupiga marufuku vifaa vya nylon na plastic but je utapata wapi substitute good ambayo haitoathiri mazingira. Karatasi unahitaji kuua misitu yote.


Suala la viroba.
Makamba na smartness yako yote haukufikilia vizuri pamoja na ofisi yako ambayo ni namba 2 Kwa ukubwa nchini....!! Haiwezekani katazo linatolewa mwezi wa februsri alafu mwezi machi unakamata watu wenye store ya viroba.. How come? Watu wanastock ya kutosha na wamelipia vat Kwa kuingiza mzigo sokoni..wafanyabiashara wakiwa serious wanakushitaki na ofis yako.!!
Kwanza ulibid utoe katazo la kuzalisha baada ya miezi sita then lifuate katazo la utumiaji na usambaji..!!

Makamba dawati lako unashake kijana mwenzangu. Alafu ivi serikali haitaki viroba Kwa sababu ya nylon inachafua mazingira au kwasababu ya afya...!! But makamba jua hata TBS walivithibitisha viroba hivyo!! Hata tfda pia. Je madhara ya viroba yanazidi ya Grant.. Na je wewe Januari unahusika na madhara ya viroba..wewe ni waziri wa afya? Pia makamba kumbuka hata usimamizi wa pombe na vileo siyo yako..sheria za vileo hizi zinasimamiwa na waziri Tamisemi. Kwann umekuwa front.!!

Cheap politics..unatafuta attention.

Makamba hili jambo si dogo...nakwambia si dogo..!! Haiwezekani mpige marufuku one month wakati watu wanastock. Umesababisha hasara na kifo kisicho na lazima..!! Tanzania ya kukomoana na siyo Viwanda..!! Humshauri Rais vizuri.

Tukutane bungeni..!! Makamba. Jiandae kuondoka. Makamba umeniangusha sana...Upo smart sana , kuhitaji cheap popularity km hii.sitisha zoezi Mara 1. Washauri wa Rais mnamwangusha sana Rais.

Dawati lako linavitu vingi sana very potential..!! Ebu firikia Kwa climate change hii na mvua zisizo tabilika.., je wewe kwa kushirikiana na waziri wa kilimo, mnamikakati gani au adaptation measures gani mnazozifanya kusaidia kilimo.
Wasaidizi wa Rais mnafanya mambo mpate umaarufu wa kisiasa.

Nimeamini Leo kumbe common sense is not soo common.

Pole mheshimiwa Rais huna washauri..!!
Another bashite movie
 
Kusema Ukweli Hiki Kitu kimenisikitisha sana..

Hivi hawa watu wamesoma wapi(kama ni kweli elimu inafungua ubongo).?

Watu weshalipia kodi kisha mnakuja mnakamata bidhaa zilizo na thamani ya mil.600.?????kweli.!!!!!!

Nilishangazwa sana na waziri mkuu kuhusika kwenye hili kwasbabu nilikuwa namuona na busara sana.!

Haihitaji Ufaulu Mtihani wa darasa la 4 kujua kwamba unatakiwa utangaze Production isitishwe ndani ya muda fulani,Kisha uwape muda wafanya biashara kuwa ndani ya muda fulani stock zao wahakikishe wanazimaliza .
 
Kuna mmoja kaona mwenzake anatajwa mno magazetini yeye akakurupuka na kusema atawataja mashoga na wakutane central.

Huyu bwana yeye kaja na hili.

Enzi za utoto tuliamini kuvaa miwani ni ishara ya usomi, kumbe miwani ni kwakua una shida ya macho na unaweza ukawa umeathiri hata ubongo wenyewe.
 
Kwakweli JPM kakosa mawaziri.
Huyu February ndio kabisaa hamsaidii Rais,bali ana mwangusha.Vifungashio vya plastik kwenye pombe lingepewa muda wa kutosha kuwawezesha wafanyabiashara wajipange.Kama ni madhara ya pombe,watu walianzia kwenye gongo.
 
Kiukweli mimi sinywi pombe na niko kinyume nayo ila pinga uongo na unafiki hata kama unakusaidia wewe,TBS wameidhinisha kuwa pombe haina madhara iwe kwa maslahi ya nchi au kwa maslahi ya wana TBS ila tunaangalia umuhimu wa chombo kama TBS nchini,Haya kama vile haitoshi serikali imesha lamba kodi hapo,watu wenye mitaji yao mikubwa wameleta mzigo leo mwezi mmoja tu mnakuja kuwavamia watu kwenye store zao na kukamata mzigo,hivi mzigo wa 1bilion unawezaje kuisha kwa miezi 2?
Huu ni uonevu,serikali na pamoja na raia,kila mtu akiwa anakuja na matamko na anataka yafanyiwe implementation harakaili tuu kumsuuza Mkuu,this is not fair
 
Haiwezekani bidhaa ipigwe ban ndani ya mwezi 1 ..tunaviongozi wasiofikiria vizuri..unapiga marufuku then 1 month unafatilia hadi stock tena wengine wameshalipa kodi
 
Wakati wa Mchakato wa Urais ndani ya ccm 2015 January Makamba katika sera zake alianisha vyanzo vipya muhimu vya kukusanya na kuongeza pato la Taifa.Ameamua kuacha kutumia ubunifu wake kumshauri Rais badala yake anashiriki ktk sera za kulirudisha nyuma Taifa.
Mwambie Mkuu aache kupambana na Upinzani ili apate mda wa kujenga uchumi imara wa Taifa na Watanzania wengi Wameishachoka Vituko,matamko n.k
 
Wapeleke risiti kuwa walinunua kabla ya tangazo kama kweli unataka uwasaidie kulalamika. Pia wamgerudisha waliponunua na kudai pesa walizokatwa. Viwanda ndio vingeisoma namba zaidi kiaina fulani kama pia hawakuacha kutengeneza baasa ya tamko.

Kuhusu maplastiki ni kweli yanachafua na kuharibu mazingira.
 
Wakati wa Mchakato wa Urais ndani ya ccm 2015 January Makamba katika sera zake alianisha vyanzo vipya muhimu vya kukusanya na kuongeza pato la Taifa.Ameamua kuacha kutumia ubunifu wake kumshauri Rais badala yake anashiriki ktk sera za kulirudisha nyuma Taifa.
Mwambie Mkuu aache kupambana na Upinzani ili apate mda wa kujenga uchumi imara wa Taifa na Watanzania wengi Wameishachoka Vituko,matamko n.k
Wakati wa Mchakato wa Urais ndani ya ccm 2015 January Makamba katika sera zake alianisha vyanzo vipya muhimu vya kukusanya na kuongeza pato la Taifa.Ameamua kuacha kutumia ubunifu wake kumshauri Rais badala yake anashiriki ktk sera za kulirudisha nyuma Taifa.
Mwambie Mkuu aache kupambana na Upinzani ili apate mda wa kujenga uchumi imara wa Taifa na Watanzania wengi Wameishachoka Vituko,matamko n.k
Hawa vijana siwaelewi kwakeli..inaitwa nitoke vp
 
Back
Top Bottom