Makamba amkoromea Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makamba amkoromea Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 24, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,602
  Trophy Points: 280
  CCM yamgeuka Lowassa
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 23rd December 2010

  Habari Leo

  [​IMG]
  Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa.

  MGOGORO wa kisiasa wa kuhusu uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha, unaweza kuzaa mpasuko siyo tu kwa wakazi wa Arusha, bali hata kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya Katibu Mkuu wake, Yusuf Makamba, kutofautiana na mmoja wa makada wake maarufu, Edward Lowassa.

  Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Makamba akionesha kutofurahishwa na kauli
  ya Lowassa ya kutaka mgogoro huo wa umeya wa Arusha umalizwe kwa amani kwa kuzikutanisha pande zinazohusika, alisema taarifa ya Lowassa iliyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari jana, imemshitua sana.

  Pamoja na kuzungumzia amani, Lowassa pia alisisitiza wahusika kuelimishana ili kuunusuru mji huo wa Arusha na Taifa kwa ujumla, usitumbukie katika ghasia.

  Lowassa alivitaka vyama hivyo kukaa meza moja kumaliza vurugu zilizotokana na uchaguzi wa
  kumpata meya wa jiji hilo ambapo iliripotiwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alisababisha vurugu na kukamatwa na polisi ambapo baadaye aliachiwa.

  Jana, baadhi ya magazeti yalimnukuu Lowassa akisema juzi katika mkutano mjini Arumeru kuwa, “leo nimekuta Mji wa Arusha ukiwa umezingirwa na askari Polisi na sehemu zingine kulikuwa na gari la maji ya kuwasha kwa ajili yakulinda usalama wa mji na watu wake.

  “Hali hii imetokana na uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, nawaomba viongozi wa vyama
  vinavyovutana, wakae haraka ili kuondoa hali hii ili Arusha isije kuwa kama Ivory Coast…Arusha ni yetu sote.” Alisema.

  Hata hivyo Makamba kutokana na taarifa za vyombo vya habari alisema:“Nimeshitushwa sana na taarifa hiyo, nimeshituka kwa vile namjua vizuri Mheshimiwa Lowassa.

  Ni kiongozi makini, hakurupuki, ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na anazijua sana taratibu za Chama.

  Hawezi kukikemea Chama chake kupitia magazetini. “Anapo mahali pa kukikosoa kama kimekosea. Ni katika vikao. Nadhani amenukuliwa vibaya.”

  Makamba alisema vurugu zinazoendelea Arusha haziwahusu na wanaopaswa kukemewa kwa kutaka kuigeuza Arusha kuwa Ivory Coast, siyo CCM kwani wao wanaamini uchaguzi uliendeshwa vizuri na mgombea wa chama chao ndiye Meya wa Arusha kwa sasa.

  Makamba alisema hoja ya Lowassa kuwataka wakae meza moja na Chadema, haina msingi ambapo alisisitiza “hatuna ugomvi na Chadema na mgombea wetu ameshinda, upande usioridhika na matokeo unapaswa kuyapinga kwa mujibu wa taratibu zilizopo.”

  Alisema uchaguzi huo haukusimamiwa na CCM, bali Mkurugenzi wa Jiji la Arusha hivyo kasoro kama zipo, CCM haipaswi kulaumiwa, akifafanua kuwa “upande ambao hauridhiki na matokeo hayo, unapaswa kuyapinga kwa mujibu wa taratibu zilizopo.”

  Lakini akizungumza kwa simu jana jioni kutoka nyumbani kwake Monduli, Lowassa alisema hajayaona magazeti ya jana yalivyoandika, lakini alichokisema juzi ni kwamba vyama husika vikae na kuzungumza namna ya kumaliza tofauti zao kwa sababu vurugu hazina maslahi kwa Arusha na Taifa kwa ujumla.

  “Niko Monduli, sijaona magazeti ya leo (jana), lakini nilichokisema juzi ni kwamba vyama husika, vikae na kuzungumza kwa nia ya kumaliza tofauti zao. Sijamkemea mtu, sijasema nani mshindi, nani ameshindwa. Nimetoa ushauri, kwa sababu sitaki amani ivurugwe,” alisema Lowassa.

  Alisema katika ushauri wake, hakutaja jina la chama chochote, na anaweza kuwa amenukuliwa
  vibaya, lakini la msingi alilosisitiza ni kuwa suala la kuelimishana.

  “Pengine hawajui utaratibu, ni suala la kuelimishana. Tusipigane mitaani, tuwaelimishe wenzetu. Nisingependa kuona Arusha inakuwa na vurugu, tunahitaji mji wetu uwe na amani,” alifafanua Mbunge huyo wa Monduli.

  Chadema juzi iliandaa maandamano na vijana wa chama hicho kuingia mitaani na kulifanya Jeshi la Polisi kuingilia kati na kuwatawanya kwa maji ya kuwasha.

   
 2. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,770
  Likes Received: 2,043
  Trophy Points: 280
  Uyu makamba ovyoo eh?
   
 3. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni wazi kuwa hao polisi wanafuata maagizo ya Makamba!!
   
 4. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwani makamba anajali hata tukiuana?nilishawambia tuwapuuze viongozi ambao sio future,wameshaishi over 80% ya maisha yao hawana cha kupoteza
   
 5. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,838
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  Mhe. Lowasa ana hoja ya msingi
   
 6. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  hli jamaa sometimes huwa linafikiria sana.
  "Hali hii imetokana na uchaguzi uliomalizika hivi karibuni, nawaomba viongozi wa vyama
  vinavyovutana, wakae haraka ili kuondoa hali hii ili Arusha isije kuwa kama Ivory Coast…Arusha ni yetu sote." Alisema."Niko Monduli, sijaona magazeti ya leo (jana), lakini nilichokisema juzi ni kwamba vyama husika, vikae na kuzungumza kwa nia ya kumaliza tofauti zao. Sijamkemea mtu, sijasema nani mshindi, nani ameshindwa. Nimetoa ushauri, kwa sababu sitaki amani ivurugwe," alisema Lowassa. "Pengine hawajui utaratibu, ni suala la kuelimishana. Tusipigane mitaani, tuwaelimishe wenzetu. Nisingependa kuona Arusha inakuwa na vurugu, tunahitaji mji wetu uwe na amani," alifafanua Mbunge huyo wa Monduli.   
 7. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  I hate Makamba doesn't care what is happening ni kiongozi lakini wakumpuuza, bado ana dreams za chama kimoja matukio haya yote Arusha, Mwanza, Kigoma, Mbeya nk injinia ni yeye, ndiyo kwa chama chake atakifurahisha lakini kitaifa anaharibu.
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Lowasa ndiye kinara katika vurugu zote hizi Arusha. Bila shaka ndiyo maana hata kauli zake zimemshitua sana Makamba.
   
 9. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Sikujua kwamba Lowasa kichwani kwake huwa kuna hoja constructive kidogo sometimes..Lakini huyu clown Makamba sielewi kwanini bado ni katibu mkuu wa CCM..hata kama mnaibia watz, CCM tafuteni mtu smart awe face of the party..mtachekwa wajameni.
   
 10. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,838
  Likes Received: 2,000
  Trophy Points: 280
  sio kweli aisee
   
 11. Tambara Bovu

  Tambara Bovu JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 19, 2007
  Messages: 586
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  yaani hapo nakubaliana nawe kabisaa mkuu.halafu huyu makamba sijui anamatatizo gani.hivi amesoma hadi darasa la ngapi?nahisi soon ntahitaji profile yake maana anayofanya hayaendani na umri na uzoefu wake.
   
 12. e

  ejogo JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 19, 2009
  Messages: 994
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  makamba ataacha lini upuuzi!!
   
 13. c

  carefree JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Makamba sasa anaishi miaka ya ziada hivyo anachuki, wivu na uwezo wake kufikiri umepotea kwa hy haoni madhara ya watu kupoteza maisha wala haimuumi ,
  angekuwa baba yake ningemkana hadharani baba hana busara hata ya kuchunga kuku
   
 14. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #14
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,827
  Likes Received: 10,128
  Trophy Points: 280
  Nashukuru sikua na baba borgus kama huyu...yaani nani kakemewa hapo na hata kama Lowasa kakemea kwani si ni kweli CCM walicheza rafu?

  akifa Lowasa (Mungu aepushie mbali) nipo tayari japo kidogo kusema kua marehemu alikua mtu mzuri lakini huyo mwenye kisukari chake....mmmh wapi!

  Niliskia watu wenye kisukari wana maatatizo ya kichwa hasa kisukari kikiwa severe, ni sawa kwa Makamba?
   
 15. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Makamba ana hasira mwanae January kakosa uwaziri kwahiyo hatumii tena kichwa chake kufikiri bali maungo yake mengine ya mwili wake!!
   
 16. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Makamba na Lowasa wanjua exactly kinachoendelea Arusha
  Makamba ni hayawani na hiyo ndio type ya viongozi 'makini' kwa CCm
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Ana maslahi ya msingi. Hana hoja. Ukisikia Lowassa anasema kuondoa mpasuko ujue ni kichekesho sana, yeye through CCM mtandao alikuwa architect wa mpasuko, sasa umeanza kumtafuna ndio anaona haja ya kukaa meza moja. Na kukaa huko anakokuzungumza ni kuwa aweze kurubuni pande mbili kwa maslahi yake binafsi.

  Hona ni kwamba Arusha inatakiwa kuwa shwari, haitakiwi kuwa battle ground ya mafahari ndani ya CCM. Kumsikiliza Lowassa ni kuanza kurudisha matatizo.
   
 18. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 896
  Trophy Points: 280
  Lowasa aka Senator wa Arusha.

  Lowasa could make a great leader if he could stay away from theives (Indians and Iranians).

  Sasa wamemtia gundu tu.

  Anadharaulika hata na Makamba.

  Pole EL.

  Una hela lakini hauheshimiki tena.
   
 19. w

  wikolo JF-Expert Member

  #19
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 801
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa nini viongozi wetu si watu wa kusimamia ukweli? Kwani kuna shida gani ukisema mkurugenzi kavunja kanuni na hivyo meya aliyepatikana si halali bila kujali chama alichotoka? Ina maana mzee wetu huyu yeye anaona ni sawa uovu ufanyike kwa vile tu unakinufaisha chama chake? Haingii akilini kwa mtu yeyote mwenye fikra sahihi na kwa hali hii,wanakotupeleka si kwema. Ni bora hata wangekuwa wanakaa kimya kuliko hivi wanavyotufanyia.
   
 20. Diehard

  Diehard JF-Expert Member

  #20
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 370
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Unamaananisha nini kuhusu january maana ndo baba hivyo, sasa naamini January alilelewa na familia ya Mh Shelukindo, lakini tabia za baba yake zitamfika uzeeni yaani hapinduki kwenye hizo tabia uzeeni
   
Loading...