Makamba achaguliwa kuwa Katibu mkuu CCM

WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM

Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu Yussuf R. Makamba
.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
Ndugu Jaka Mwambi
.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz
.
Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM Taifa
Ndugu Rostam Aziz
.
Katibu wa Organaizesheni wa CCM Taifa
Ndugu Kidawa Hamid
.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa
Ndugu Aggrey Mwanri.

Katibu wa ISiasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM Taifa
Dr. Asha Rose Migiro.
 
Pamoja na kwamba tunaweza kukubaliana au kutokubaliana na ufanisi wa kazi za wateuliwa lakini ukweli unabaki kuwa hii ni issue ya kichama zaidi na ningependa kuchukua muda huu kumpongeza Mzee Makamba kwa kuendelea kuaminiwa na kupewa madaraka makubwa. Natumaini utaendelea vizuri kuwasimamia viongozi wa serikali katika utekelezaji wa sera zako. Pia nadhani hili liwe fundisho kwa vyama vya upinzani kwamba wanahitaji kuiga CCM kwa kubadilisha viongozi baada ya muda fulani na kuja na mipango mizuri. Mimi nikiwa siyo mwanachama wa CCM nadhani sina haki ya kumlaumu Mzee JK kwa uteuzi wake, BWM alifanya hivyo hivyo alipopewa rungu, JK amembakisha mtu mmoja BWM aliwaondoa wote. Kazi kwenu wana CCM tunataka kazi sasa, au kuna kitu kingine tusubiri? Lipumba, Mrema, Seif, Mbowe, muda umefika na ninyi kuwaachia watu wengine.
 
Katika Vyama vyote najua vinaweza kufanya mageuzi ila sema hawana wanasiasa real ila waganga njaa .Chadema nahdani wamesha fanya mabadiliko maana alikuwa Mtei akaja Mbowe na alikuwa Kabourou akaja Slaa .Sidhani kama kuna la kusema kwa Chadema .Shida ya vyama vtetu vya Siasa chama ni mtu na ni instituation ndiyo shida na hapa ndipo CCM wanapo fanikiwa .NCCR they did well .Alikuwa Marando akaja Mbatia na baadaya Mrema na sasa naamini NCCR wana Katibu mkuu mpya .Upinzani wakifanikiwa kuwaondoa Mrema na TLP yale na CUF kukubali mabadiliko patakuwa na mwelekeo zaidi .

Ila sikubaliani na hoja yako kwamba kwa kuwa CCM wamefanya mabadilijo basi na Vyama vyingine vifuate hapana .Nakubali hoja ya uongozi wa kweli kwamba Chama kikishindwa ama kuingia kashfa basi kiongozi aliyehusika ajiuzuri kutoa nafasi hili ndilo naomba ambalo si hata Serikali ya CCM inaliweza .
 
Kila chama kina Katiba yake na kina taratibu za chaguzi.

Mabadiliko ndani ya chama hayafungamani au hayana uhusiano na mbadiliko ya chama kingine.

Kama Katiba au Taratibu za CCM zinavyowapa mamlaka ya kuongoza kwa miaka kumi au kila mabadiliko ya rais yanapofanyika, vyama vingine vina utaratibu wao hata kama ni kubakia mwenyekiti kwa miaka 20 ilimradi wanachama na kamati kuu inaridhia.

Mfano mimi nafahamu Chadema hutoa nafasi kwa mtu ye yote kugombea Uenyekiti na siyo kamati kumsimamisha mtu. Mwanachama ye yote hai anaruhusiwa na wanachama ndiyo kupitia kamati ya chama ndiyo wana nafasi ya mwisho kwa kuwapigia kura walioomba kugombea uongozi ndani ya chama.

nadhani tatizo kubwa kwa taifa la Tanzania ni kwamba tumelelewa katika mazingira na imani ya kuwa Chama Tawala ndicho BABA, MAMA, na NDUGU

********
Maisha Safari ndefu, kutembea usichoke.
 
Aljazeera
Karibu mzee!
Nadhani jambo la muhimu kwa wapinzani ni kuchukua mawazo na kuyafanyia kazi siyo kuyapinga. Sijasema na wao wafanye uchaguzi inabidi wajifunze mbinu ya kubadilisha watu, kwenye siasa hata kama mtu ni mchapakazi kiasi gani inafika wakati watu wanamchoka. Mrema na Lipumba wa '95 siyo huyu wa leo. Viongozi wa chama siyo mwenyekiti tu ni viongozi wote.
Ili chama kiingie madarakani lazima kipate baraka ya wananchi ambao ndiyo wapiga kura. Na wananchi wenyewe ndiyo sisi, tunawambia viongozi wenu wamechoka wanahitaji damu mpya mnadai mna utaratibu wenu, fine, kaeni na utaratibu wenu.
Siku zote najiuliza lengo la vyama hivyi vya upinzani ni nini hasa. Labda kuongoza ahela.
 
Wazee, ukweli ni kwamba JK katika CCM ameweka viongozi anaoweza kuwaburuta, anaoweza kuwaambia ruka juu! wakauliza urefu gani mzee! Haya ndiyo mambo aliyokuwa akiyafanya Foreign, alifikia mahali mpaka posting za nje alikuwa involved, sasa anataka kuamua hata katibu wa kijiji awe nani,

Mangula alichaguliwa na Mwalimu na wala sio Mkapa, na ndio maana mara nyingi Mangula alikuwa akigomea maamuzi mengi ya uabbe wa Mkapa, sasa hiyo ni hadithi maana unafikiri Makamba atamgomea JK? Kitu kimoja cha muhimu ni kwamba kumbe sometimes JK akionywa husikia, maana miezi miwili iliyopita nilisema kuwa mzee mmoja wa CCM alimuonya JK, kuwaweka mbali Mtandao na CCM na amefanya kweli, sasa swali ni kwamba je Mtandao kina Nchimbi, Membe, Ditopile, watakubali kumpa Makamba nafasi afanye kazi yake?

Hapa ndugu zangu kuna kitendwili kikubwa tena sana, maana behind huu uchaguzi nina-smell a betrayal mbele ya safari, hawa Mtandao ni lazima hawakuridhika na huu uchaguzi, kwa sababu ni clear kuwa hapa ni nani anayetayarishiwa kuwa rais 2015, je watakubali? Anyway hayo ni mawazo yangu binafsi, isipokuwa huu uchaguzi ni typical JK kutaka kuamua kila kitu mwenyewe bila ya kushirikisha mtu!
 
Ni kweli Kabisa 99% kuwa Mangula aliwekwa na Nyerere. Akina Butiku walipiga sana Kampeni wakati huo.

Siku moja before tuliijua kuwa Mangula angeteuliwa kuwa Katibu Mkuu huko Dodoma.

Kwa mtizamo wangu ninadhani amefanya kazi nzuri ya chama hadi sasa(anaoneka siyo mwenye tamaa na mali ! ila sina uhakika na hili). Mwaka jana tulimsikia akisema chama hakitakubali viongozi wenye "element" ya udikiteta na hapa alimaanisha maamuzi ya kimabavu ya ....


Mzee ES au mr FD, CCM ina mpango gani wa kuanzisha angalua malipo hata ya sh 30000/= kwa mwezi kwa viongozi wake wa ngazi ya shina?

Maana wenyeviti wa CCM na pia viongozi wa serikali wa ngazi za shina hawalipwi MISHAHARA JE NI KWELI CCM HAINA UWEZO WA KUWALIPA MISHAHARA HAO WATU? ruzuku yake kubwa ya kila mwezi inaliwa na akina nani tu? MAANA INAPOFIKA WAKATI WA UCHAGUZI VIONGOZI WA SHINA HUWA WANAFANIKISHA SANA USHINDI WA CCM LAKINI CHA AJABU BAADA YA HAPO HUACHWA MIDOMO MITUPU.

Ni imani yangu kuwa wakilipwa mishahara watatenda kazi kwa haki badala ya kuanza kuwasumbua wanachi kila mtu anapoenda ofisini mara utsikia njoo na karatasi yako ili tukuandikie au njoo na sh 1000 nk.
Mimi ninaamini wakilipwa mishahara itasaidia sana kupunguza uonevu na unyanyasaji wanachi vijijini.

Ningelipenda kusikia ni jinsi gani JK analifanyia kazi hili suala pia Kama unaongea na JM tunataka kusikia maoni yake juu ya hili. Ni kwa nini wenyeviti wa shina wa serikali na wa CCM hawalipwi mishahara? CCM ina hela nyingi si kweli kwamba haina uwezo wa kuwalipa mishahara watumishi wake wa ngazi za chini bali ni tamaa ya wachache tu kuendela kutafuna fedha za chama wao wenyewe?

Akina Makamba tafadhali lifanyieni kazi hili tatizo.
 
Mkira,

Mawazo mazuri, ni kweli hao watu hawalipwi, sijajua sababu, ila naweza kujaribu kutoa sababu. Maana haikuandikwa kwenye katiba sababu za kutowalipa.

Kwa kawaida Katibu ndie mtendaji, anapaswa kulipwa, ndani ya chama chetu CCM ngazi ya chini ya katibu kuwepo ofisini saa zote za kazi ni KATA. kwahiyo katibu kata anakuwepo ofisini muda wote wa kazi. Baada ya hiyo ngazi kuna TAWI (katibu wake halipwi) kisha kuna SHINA.
Utaona umeongelea chini sana na frequency ya mikutano sio mingi na hata kazi sio nyingi. Kwa maoni yangu hali iendelee hivihivi. Hela zipo ila UTARATIBU wa kukusanya toka vyanzo vya mapato na utumiaji ndio sio mzuri.

Ngoja nitajaribu kuongelea wazo lako kwenye vikao nisikie wengine wanasemaje!

Kidumu Chama cha mapinduzi!
 
Last edited by a moderator:
Mimik badala ya kulia na uteuzi ama kufanay chaguzi za vyama ninataka kuona vyama vinapungua na tunakuwa na vyama ambavyo wananchi wataviamini na kufanya navyo kazi .Najua CCM haitapenda kuona Upinzani unakwua na nguvu lakini si kwa manufaa ya vyama bali ni manufaa ya Tanzania na Taifa .Chaguzi ni kitu kidogo sana mimi issue kwangu ni kupunguza vyama na kuwa na vyama hata 3 vyema maana na mwelekeo it will make sense .
 
Mzee Mkira,

Mzee FD anayo majibu ote ya maswali yako, na pia heshima juu maana maneno mengi ni mazito!

Mzee Muggy,

Hakuna la kuongeza, isipokuwa tu ni jukumu la vyama vyenyewe kupungua CCM haitafanya hilo kwani uwingi wao ni furaha ya CCM, ukweli ni kwamba tunahitaji kuwa na vyama viwili tu CCM na Upinzani, halafu may be when the time is ready Indapendent Candidate, ispokuwa tena kabla ya kuruhusu Independent Candidate, lazima kuwepo na mabadiliko ya katiba ama sivyo yatakuwa yale yale tu CCM wataigeuza hiyo element ya I ndependent Candidate kwa manufaa yao,

Kama walivyofanya on vyama vingi, sasa upinzani wasirudie kosa tena la kuingia kichwa kichwa ni afadhali wagomee kuliko kuwemo tu, wananchi wamechoka na kuburutwa kama wajinga na kukosa pa kukimbilia!
 
Mzee Es
Point noted .Nakubaliana nawe kwamba Katiba inawaua wapinzani na no one is talking or even thinking of Katiba changing why is that ? Ni muda huu wanao wa kutosha wa kulia na Katiba kama kweli JK ni msikivu na mpenda Tanzania he will push and back the call for the Const changes .Naona wapinzani wanajikita kuona JK anafanay nini badala ya kujiandaa sasa na kuanzia na Katiba .They must sit down and think na kuingian kudai Katiba Mpya .Mzee Es Mnyika akipita hapa basi naamini ataenda kumwambia Mbowe na waanze madai haya .
 
Tatizo siyo Katiba! Waswahili wanasema "Papa mkaange kwa mafuta yake". Kama wapinzani wangeamua kutumia Katiba iliyopo ili kuwanikisha kisiasa wangeweza kufanya hivyo. Katiba iliyopo inawanufaisha CCM kwa sababu wameweza kuitumia vilivyo kujikita madarakani. Je wapinzani wangeweza kuitumia Katiba hiyo vipi?

Jibu ni rahisi! Bunge, Bunge, Bunge..... Kosa kubwa walilolifanya ni kuwekeza fedha nyingi kwenye kiti cha Urais badala ya kujikita kwenye majimbo. Wapinzani hawataweza kuibadili Katiba kwa kupiga kelele kwenye semina na warsha! Njia pekee ya wao kuweza kuibadili Katiba au kufanya mabadiliko ya sheria ni kuanzia Bungeni. Kwa maoni yangu, Wapinzani wana nafasi mbili za kuchukua Bunge, kwanza ni 2010 ambao wadhamiria kuchukua viti angalau 100 na 2015 ambapo wadhamiria kuongeza viti vingine 50 - viti 150 ni sawa na asilimia 53 ya viti vyote ni zaidi ya theluthi moja!

Ni lazima wabadili mkakati!! Kwanza waungane siyo kama shirikisho bali kuua na kuvizika vyama vyao vya sasa na kuja na chama kimoja. Mambo ya shirikisho kama Narc hayawezekani Tanzania. Wakiungana basi wanaweza kupata nafasi ya kujenga imani ya Watanzania kuwa wapinzania siyo wachekeshaji!! Nilitamani kuona Bunge la kina Mrema, Seif, Lipumba, Mbatia n.k... Hilo lingekuwa Bunge lenye joto...... But then, what would I know?
 
Wazee, thanks for great contributions.

Mnalionaje hili la JK kupata kura zote isipokuwa moja tu? does it mean kwamba wajumbe wote isipokuwa mmoja tu wapo happy na mabadiliko ambayo mwenyekiti atayafanya (dalili zipo) hata kama yatawahathiri?

Naamini kuwa kuna wajumbe walikuwa na informations za mabadiliko ya sekretarieti ya CCM Taifa kabla hata ya mkutano wa Dodoma, sasa hao wajumbe na wanaowaunga mkono (ambao kwa akili za kawaida wasingependa jamaa zao watolewe) hawakuwa na habari kweli, au wanaamini labda Mzee JK hatawatupa kabisa, ila atawatafutia sehemu nyingine?

Kama kweli wajumbe walipiga kura kwa mapenzi yao bila sababu nyingine..., then wananchi hawana budi kuamini kuwa makundi ndani ya CCM yameshazikwa. Kama CCM imerudi kuwa moja kwelikweli basi ipo kazi kubwa sana tena sana ya kujenga upinzani wakuhakikisha ''tembo CCM halali usingizi" kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla.
 
Amani na matatizo ya CCM, siku zote yanategemea mtu mmoja tu naye ni JM, as long as walioko kwenye power wako naye sawa hakuna tatizo na to the suprise of wajumbe wote safari hii alikuwa ANATAKA KUTOKA!, hiyo ikaleta a big confussion kwa wenye power kuwa WHY? Kwanini anataka kutoka now? Wenye power wakakataa kata kata! Maana huwezi kumuamini huyu mzee anataka kufanya nini next? I found this to be very interesting kwa hawa Mtandao ambao walikuwa siku zote wananlilia kuwa hafai na ni mzee na atoke,

Katika kikao kilichopita cha NEC wajumbe wengi walimjia juu JK kuhusu kundi lake la Mtandao, na akapewa one condition kupigiwa kura ya mwenyekiti kama atawaweka kando Mtandao ndani ya CCM, kwa hiyo hilo ndilo lililomsaidia, na litakalomsaidia from now on kwenda mbele,

Sasa tatizo la JK ni Mtandao wenzake maana hawakuridhika na huu uchaguzi na ninajua kuwa watamtesa sana Makamba na wenziwe, anyway mwakani ataingia EL kwenye makamu, ambaye sasa hivi yuko katika mazoezi makubwa ya kujitayarisha, lakini swali ni kwamba ataweza? Ataweza ule mchezo wa anayetoka wa kwenda kuishi kijijini miezi miwili kupiga kambi ya uchaguzi kwa kulala kwenye madarasa ya shule za msingi, huku amechukua magunia ya mchele na maharage, mpaka kuona ushindi wa jimbo unapatikana ndio arudi mjini?

Kwa upinzani mamba yanaendelea kuwa yale yale, tena sasa ndio balaa maana Jk na kundi lake wanaamini sana siasa ya hela zao kwa hiyo wapinzani wajiangalie sana safari hii maana wote watanunuliwa!
 
Mzee Mwanakijiji,

RA ndiye aliyekua na ndiye anye-run mambo yote ya pesa toka uchaguzi wa rais, na pia wakati wa ubunge kuna wabunge kadhaa ambao hawakuwa Mtandao, lakini Mtandao walikuwa wanawahitaji ni yeye RA ndiye aliyekuwa ana-supply takrima! Sasa kwa sababu hizo hakukuwa na tatizo la yeye kuchukua hiyo nafasi ambayo ukweli ni low-profile within CCM,

Yeye alichoogopa kuwa waziri ni makelele ya wananchi na the fact kwamba mpaka kufikia uchaguzi wa rais mambo yake mengi yalikuwa wazi, na ukweli kwamba ni Mu-Iran ilikuwa inawapa homa wafadhili wetu wa West na they it clear kwa BM na JK mwishoni kwamba wasingependa huyu awemo, na juzi alipokuwa US JK alionywa na wakubwa kuhusu Iran na terrorism, na kuambiwa aisaidie US kuwafuatilia hawa wtu wa Middle East walioko hapa bongo, kwa hiyo ni wafadhili ndio waliomkwamisha kuwa waziri lakini hata hivyo akawazunguka na kumuweka mistress wake,

Uwaziri hakunyimwa ila aliogopa the West, haweki hazina ila anatumia hela zake kui-run CCM, huo ndio ukweli!
 
FD na mzee ES asanteni kwa majibu yenu na pia ninashukuruni kwa kunielewa. Niliandika kwa haraka na nilikuwa ninamaanisha viongozi wa matawi lakini cha ajabu nikaandika viongozi wa shina! Hata hivyo wote hao wahalipwi kwa hiyo katibu mkuu mpya na na JK tafadhali watafute ufumbuzi wa hilo tatizo.
 
Huyu ndiye watu walimwita mwenye busara sana Makamba .Kawa kartib Mkuu kaonyesha his true colour .Je kwa maneno na dalili hizi kuna siasa Tanzania tena za Vyama vingi ama ndiyo mwisho wake ??

2006-06-28 18:46:36
Na Dominic Nkolimwa, Lumumba


Katibu Mkuu mpya wa CCM Luteni (Mstaafu) Yusuf Makamba amewaaga rasmi wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na kama kawaida yake amerusha vijembe vya lala salama kwa vyama vya upinzani.

Kwanza amewaambia wapinzani kwamba wasidhani Rais anaweza kuwapa nafasi yake ya Ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambayo iko wazi.

Akasema badala yake nafasi hiyo itakwenda kwa kada mzuri kutoka CCM.

’’Nawaambia wapinzani kuwa sasa chama kimepata watu, kama majibu ya kebehi na ngebe hapo ndio wamefika, na hata kama ni majibu ya ustaarabu, hapa yamejaa,’’ akarusha kijembe kingine.

Kana kwamba hiyo haitoshi, Mzee Makamba akawavunja mbavu meza kuu akiwemo Rais Kikwete kwa kusema ’’Wapinzani wakisema utajiju nasi tunawapa kubwa zaidi ya hiyo kwa kuwaambia utajiju mwenyewe na wenzako wote’’.

Aidha Mzee Makamba alimtoa wasiwasi mwenyekiti wake akisema asidhani kuwa kuwachagua kushika nafasi hizo alikosea, bali asubiri kazi, kwani timu imekamilika na hakuna mchezo.

’’Sisi si watu wa kukaa ofisini, sisi ni wanasiasa... kazi yetu kubwa ni kujenga chama, ofisi ni ya wanachama na wala si viongozi’’ akasema.

Akaongeza kuwa safari ya kukijenga chama imeanzia Dodoma dakika chache tu kabla ya kuchanguliwa kuwa viongozi wa chama.

Aidha, akawataka wakazi wa Jiji wasiwe na shaka wala kuhuzunika, kwani, yeye anaenda kwa baba kuwaandalia makao kwakuwa alitoka huko na sasa ni vema akirudi tena.

Akasema kuna baadhi ya watu wanadhani kuwa amepotezwa, lakini wanasahau kuwa alitoka katika chama na sasa anarudi katika chama.

’’Lakini nataka muwambie hao viongozi wa vyama vya upinzani kuwa wasiote kuwa huenda Rais akasahau na kuteua mkuu wa mkoa huu kutoka kwao, ni lazima awe kada wa chama na wala si vinginevyo,’’ akasema Luteni Makamba huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Luteni Makamba na sektarieti mpya ya chama hicho ambayo itaongozwa na yeye (Makamba) iliteuliwa na Halmashauri ya chama hicho Jumapili jioni wiki iliyopita ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Rais Kikwete kuzoa kura katika Mkutano Mkuu uliofanyika Chimwaga mjini humo.

Mzee Makamba alirusha madongo hayo ya lala salama wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba, Jijini.

Mkutano huo uliondaliwa na wanaCCM, ulikuwa ni sehemu ya makaribisho ya Mwenyekiti mpya wa CCM Rais Kikwete na timu yake mpya.


SOURCE: Alasiri
 
Takriban miaka mitano baadaye, CCM imenufaika nini chini ya uongozi wa jamaa huyu?
 
Back
Top Bottom