Makala amfunika Murad | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makala amfunika Murad

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Jan 18, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yule kijana msomi mchakapakazi, Amosi Makala amefanikiwa mpaka sasa kumzidi kete mpinzani wake Suleman Sadiq "Murad". Bwana Makala ambaye amefanikiwa kujijengea jina Mvomero kutokana na uadilifu wake wa kupinga ufisadi katika viwanda miwa vya Mtibwa ambao unamuhusisha pia Rais Mstaafu Benjamini Mkapa. Tofauti na mwenzake Murad, Amos Makala amekuwa akisifiwa kote vijijini kutokana na kuwa upande wa wananchi, anaeleza mchambuzi wa masuala ya kisiasa.

  Hadi sasa, vita ya wazi katika majimbo ya ubunge imeanza kujitokeza katika jimbo la Mvomero, Mkoani Morogoro ambalo linaongozwa na Suleiman Sadiq 'Murad'. Katika jimbo hilo, msuguano wa wazi, unaonekana kuwa umeanza baina ya Murad na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UV-CCM) Amos Makala(Kwa sasa ni Mweka hazina wa chama hicho) ambaye alibwagwa mwaka 2005 kwa kura 540. Ukweli wa hilo umejitokeza katika ziara ya hivi karibuni aliyoifanya Makala katika maeneo mbalimbali ya nchi, ikiwemo jimbo la Mvomero. Hata hivyo, wakati Makala akieleza kufanya ziara kwa lengo la kuimarisha chama, Murad amekuwa akilalamika ziara hiyo kwa maelezo kuwa kiongozi huyo wa UV-CCM aliingia jimboni humo na kuitisha vikao vya vijana bila wenyeji kujua. Makala aliiambia Mwananchi Jumapili wiki hii kwamba, hakuvamia Mvomero kama anavyovumishiwa na wabaya wake, bali alikwenda kama sehemu ya kuimarisha chama na kusisitiza kuwa kamwe Mvomero haiwezi kuwa kisiwa. "Nilikwenda Mvomero, lakini Murad akasema nimevamia jimboni kwake, sikuvamia, nilitoa taarifa, Mvomero haiwezi kuwa kisiwa, Murad anaogopa kivuli cha uchaguzi," alisema Makala akifafanua kuhusu shutuma hizo. Hata hivyo, Murad naye kama ishara ya kujibu mapigo aliliambia Mwananchi Jumapili kwa njia ya simu jana, kwamba kwa sasa hahitaji malumbano na Makala kwani amekwisha kulifikisha suala kwa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC). Lakini Murad alithibitisha kauli yake kwamba Makala alifika katika jimbo hilo bila viongozi wengine kufahamu na kutamba kwamba yeye anatekeleza ilani ya chama kwa kaulimbiu ya nguvu, kasi na ari mpya na wala haogopi kivuli cha uchaguzi kwani hadi sasa ni mbunge na ana imani kuwa atashinda tena mwaka 2010. "Lakini labda nikueleze, sasa hivi sihitaji malumbano, hili suala nimesha likabidhi katika Halmashauri Kuu, sasa hivi natekeleza ilani kwa kasi," alisema Murad katika mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi Jumapili.

  .....ndiyohiyo
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Makalla asubiri ngumi tu toka kwa Murad...
   
 3. share

  share JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2008
  Messages: 2,293
  Likes Received: 2,277
  Trophy Points: 280
  Murad Sadiq, Mtanzania mwenye asili ya kiasia, hana jipya kwa maendeleo ya jimbo la uchaguzi la Mvomero. Alichaguliwa kutokana na ulaghai uliozoeleka wa kutumia biashara zake za maduka ya vifaa vya ujenzi kuwadaganya wapiga kura. Waasia wamekuwa wataalamu sana wa mbinu hizo ili kupata nguvu za kisiasa kupitia ubunge zinazowasaidia kulinda ufisadi wao kwa gharama za jasho la Watanzania. Ni kwa mbinu hizi, Murad mara baada ya kupata ubunge (1995) amekuwa tajiri wa kutupwa. Ameanzisha mabus ya Sadiq (Dar - Moro - Turiani), amejenga vituo vya mafuta kama uyoga, supermarkets, kufisadi mradi wa taifa wa miti ya mitiki jimboni kwake Mtibwa, kujiingiza kinyemela katika umilikaji wa kiwanda cha sukari cha Mtibwa ambacho awali kilikuwa mali ya serikali (inasemekana kimeuzwa kwa bei chee kwa Super Doll huku Mkapa akisaidikiwa kuwa mmoja wa wamiliki), amemsaidia fisadi Mkapa kupata mashamba makubwa ya miwa ya sukari eneo la Dizungu karibu na hospitali ya Chazi jimboni kwake Mvomero, amemsaidia fisadi Sumaye kupata mashamba makubwa kutoka ardhi ya vijiji jimboni kwake mvomero, amenunua magari makubwa ya mafuta kifisadifisadi. Huyu muasia anaokota utajiri wote huu kutoka mikononi mwa mwa watanzania huku akiwamwagia peremende wavujajasho kwenye ardhi yao wenyewe. Kitaaluma ni mpumbavu kabisa. Amemaliza form four Forest Hill Secondary School kwa kufeli masomo yote. F F F F F F masomo yote. Hivyo hana cheti cha form four. Lakini kutokana na ufisadi wake inawezekana sasa hivi akawa na cheti hizo kwa kununua. Murad anasinzia tu bungeni maana hana uwezo wa kuelewa mijadala ya kiakili inayozungumzwa bungeni. Imefika wakati wananchi wa Mvomero kuzinduka usingizini. Wasiwape utajiri wao waasia kwa kudanganywa na peremende. Tuiokoe nchi yetu na manyang'au. Mafisadi yanaifuata sana kauli aliyoitoa Sumaye mahali fulani (nadhani Mwanza - sina uhakika) kuwa "ukitaka mambo yako ya biashara yakunyookee, jiunge na CCM ".
   
 4. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,659
  Likes Received: 21,876
  Trophy Points: 280
  Wote hawana Nyimbo ni Ubabaishaji Jazz Band.....
   
 5. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Safi sana. Ndio maana mimi nampigia debe Amos Makala, kijana msafi msomi asiye na kashfa yoyote. Yeye ndiye awe mbunge wa Mvomero badala ya fisadi Murad swahiba wa Mkapa. Amos Makala anawashughulikia vilivyo kwa ari,nguvu na kasi mpya

  ......ndiyohiyo
   
 6. A

  AndrewMwanga Member

  #6
  Jan 18, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hakuna mtu mwenye jimbo au ambaye amezaliwa nalo, ila kama Makala amefanya ziara hizo kwa lengo la kukiimarisha chama ni jambo la kupongezwa na hasa kama amefanya hivyo sehemu zingine sioni sababu ya Murad kulalamika.

  Yeye ni mbunge wa jimbo hilo na kama alitekeleza ahadi zake kwa wananchi wa jimbo lake kwa kutekeleza kikamilifu ilani ya uchaguzi ya ccm (2005-10), wananci wa jimbo la mvumero watakuwa mashahidi na watamrudisha tena kumaliza aliyoyaanza lakini kama ni kinyume hatakuwa na jipya bali wananchi wasipumbazwe ila watumia kura zao vyema kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

  "Lets become the change thats we wants to see in the world"
   
  Last edited: Jan 18, 2009
 7. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0

  Tutamshangaa atakayempinga Kikwete...

  2008-05-13 09:02:05
  Na Mashaka Mgeta


  Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kitashangaa kama atatokea mwanachama wa kupambana na Rais Jakaya Kikwete, katika uteuzi wa kugombea urais mwaka 2010.

  Kauli hiyo imekuja huku kukiwa na tetesi za kuwapo viongozi waandamizi, wanaojiandaa kuchukua fomu, ili wateuliwe kuwania nafasi hiyo ya juu katika uongozi wa nchi.

  Baadhi ya vyombo vya habari, vilikariri vyanzo vyao mbalimbali hivi karibuni, vikidai kuwa miongoni mwa wana-CCM hao wanaouataka urais kabla Kikwete hajamaliza kipindi cha pili, walishiriki katika kinyang`iro cha kuwania kuteuliwa na chama hicho mwaka 2005.

  Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha wa CCM, Bw. Amos Makala, alisema chama hicho kimejiwekea utaratibu wa Rais aliyepo madarakani, kutumikia vipindi viwili, hivyo Rais Kikwete, atagombea tena urais mwaka 2010.

  ``Nitamshangaa mwanachama atakayejitokeza kushindana na Rais Kikwete kuwania uteuzi wa kugombea urais mwaka 2010, kwa sababu tuna utamaduni wetu uliojenga mazoea, kwamba Rais atatumikia vipindi viwili,`` alisema.

  Bw. Makala, alikuwa akihojiwa katika kipindi cha midani za siasa na uchumi kilichorushwa hewani na kituo cha luninga cha Star TV mwishoni mwa wiki iliyopita.

  Licha ya kuwepo utaratibu huo ambaao kimsingi haupo kikatiba, kwa mujibu wa Bw. Makala, aliyewahi kuwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Dk. Ghalib Bilal, alichukua fomu za kuwania Urais wa visiwa hivyo mwaka 2005.

  Wakati Dk. Bilal akichukua fomu hizo, Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar, alikuwa anaingia katika awamu ya pili ya uongozi wake.

  Hata hivyo, jina la Dk. Bilal, liliondolewa katika vikao vya juu vya uteuzi katika CCM, vilivyofanyika mjini Dodoma, hivyo kuliwezesha jina la Rais Karume kupita peke yake.

  Bw. Makala, alidai kwamba utaratibu wa kumwachia Rais kuongoza kwa vipindi vinavyotambuliwa kikatiba, unachangia kuimarisha utulivu ndani ya chama na serikali yake, hali inayopaswa kuigwa na mataifa mengine, ikiwemo Zimbabwe.

  Taifa hilo mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo na Uchumi Kusini mwa Afrika (SADC), linakabiliwa na mzozo wa kisiasa, uliotokana na Uchaguzi Mkuu ambao hata hivyo, mshindi wa urais bado hajapatikana.

  Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo, anashutumiwa na baadhi ya watu, taasisi za kijamii na mataifa, akidaiwa kung`ang`ania madarakani.

  Hata hivyo, Bw. Makala, aliunga mkono sera ya kurejesha ardhi kwa wazawa, na kutoridhishwa na mpango wa kuinyima misaada nchi hiyo.

  Alifananisha hatua ya kuinyima Zimbabwe misaada na kuhoji kasi ndogo ya maendeleo yake kuwa sawa na kumfungia mtu mawe miguuni na kumtaka akimbie.

  Kwa upande mwingine, Bw. Makala, alisema CCM kupitia awamu ya tatu ya mpango wa uboreshaji chama, inaendelea kujiimarisha katika ngazi za chini kwenye jamii, hali inayoweka mazingira bora ya kushinda chaguzi za mwakani na 2010.

  Uchaguzi wa serikali za vitongoji, vijiji na mitaa utafanyika mwaka ujao wakati Uchaguzi Mkuu wa Rais na wabunge utafanyika mwaka 2010.

  SOURCE: Nipashe
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  hivi kampeni kumbe ndo zimeshaanza??
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Asha Abdala,

  Kama unajua siasa za TZ, hivi kweli unafikiri kuna mwanasiasa mwandamizi wa serikali ya TZ atachukua forms kumpinga JK ndani ya CCM?

  Mambo mengine naona ni njia tu ya kuuza magazeti. Nikumbushe mwaka kesho kama hilo
  litatokea na nitajifungia JF kwa miezi kadhaa.
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Afadhali Mkuu umeliona hili. Hawa wote ni wababaishaji. hata huyo makala naye anatumia rasilimali alizonazo kama alivyofanya Muradi, akishapata naye atawageuka wananchin kama alivyofanya Murad
   
 11. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Shibuda: Nitamng’oa JK 2010
  na Martin Malera  MBUNGE wa Maswa (CCM), John Magale Shibuda, ameibuka na kutangaza msimamo wake kwamba ifikapo mwaka 2010, anakusudia kuchukua fomu ya kuwania kiti cha urais, kinachoshikiliwa na Rais Jakaya Kikwete kwa sasa na kwamba ana uwezo wa kumng’oa madarakani.

  Shibuda alisema hayo jana wakati akitoa maoni yake kuhusiana na uamuzi wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC), kukata jina lake katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa na Mkoa wa Shinyanga.

  Mbunge huyo, ambaye aliwahi kuwania nafasi hiyo mwaka 2005 na kuzidiwa na Rais Kikwete, alisema sababu, nia na uwezo wa kuomba nafasi hiyo anayo kwani hakuna mwenye hatimiliki ya urais.

  Uamuzi huo wa Shibuda kutangaza kuwania kiti hicho 2010 utazua mjadala na pengine kumgharimu kutokana na mazoea yasiyo ya kikatiba na utamaduni wa miaka mingi wa ndani ya chama hicho wa kumuachia rais aliye madarakani kuongoza kwa mihula miwili mfululizo.

  Akizungumza kwa kujiamini, Shibuda alisema: “Potelea mbali, liwalo na liwe, nimechoka kuwa mfungwa wa kisiasa ndani ya CCM wakati nina uwezo wa kuwaongoza Watanzania.”

  Alisisitiza kuwa ameamua kugombea urais kwa madai kuwa nafasi pekee anayoweza kugombea bila jina lake kukatwa ni urais na ubunge, lakini nafasi zingine jina lake limekuwa likikatwa na vikao vya juu vya chama bila sababu za msingi.

  “Hao wanaokata jina langu bila sababu ni akina nani? Na wana sababu zipi za msingi? Sasa nimechoka, nimekuwa mfungwa wa kisiasa ndani ya chama kwa muda mrefu, ni wakati wangu kusema basi inatosha, sitakubali kuimba wimbo wa ‘Ndiyo Mzee’ maana kugombana na sheikh, si kugombana na Waislamu au msahafu na kugombana na Kardinali Pengo si kugombana na Wakristo au Biblia,” alisema Shibuda.

  “Najua watasema mengi, najua watalikata jina langu, maana nimekuwa mfungwa wa kisiasa ndani ya CCM, kila ninapogombea, ukiuliza unaambiwa uamuzi wa chama, hii maana yake nini?” alihoji Shibuda.

  Kwa mujibu wa Shibuda, CCM haiwezi kuongozwa kwa kauli ya ndiyo mzee bila kuhoji sababu za maamuzi za vikao vya juu kwa lengo la kujenga ustawi wa chama.

  “Mimi sikubali kuwa kipandio cha wengine kisiasa, kama kila wakati jina langu linakatwa, si niambiwe basi, lakini haiwezekani kila ninapogombea, jina linakatwa, hakuna sababu, urais, jina linapitishwa basi, ni bora niwanie urais ifikapo 2010,” alisisitiza Shibuda.

  Akizungumzia uamuzi wa NEC kukata jina lake, Nimrod Mkono, pamoja na waombaji wengine, Shibuda alisema haiingii akilini kwa mtu aliyekuwa na sifa ya kuwania urais kama yeye, akose sifa ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi taifa na Mwenyekiti wa Wazazi mkoa.

  “Hivi mdogo wangu, mwaka 2005 chama kilinipitisha kwamba nina sifa ya kuwania urais, lakini leo kwa sifa zilezile naomba kugombea uenyekiti wa wazazi taifa na Mkoa wa Shinyanga, jina linakatwa, sina sifa. Hii maana yake nini? Sasa siwezi kuendelea kufanywa kipandio cha watu kisiasa na kubaki tukiabudu falsafa ya ndiyo mzee,” alisema Shibuda.

  Akizungumzia hatua ya Shibuda kutangaza kuwania urais mwaka 2010, Katibu Mkuu, Yusufu Makamba, kwanza alieleza kushangazwa kwake na hatua ya mbunge huyo na kuhoji endapo alikuwa katika hali ya kawaida.

  “Hao ndio aina ya viongozi tulionao ndani ya CCM, nyie andikeni asikike na jamii imjue, lakini binafsi sina la kusema kwa sababu utaratibu wa chama uko wazi na mbunge huyo anaujua vizuri,” alisema Makamba.

  Hata hivyo, hatua ya Shibuda, huenda ikamgharimu kisiasa ndani ya chama hicho kutokana na utaratibu usio rasmi waliojiwekea wa kutoruhusu mgombea kujitokeza kupingana na rais aliyopo madarakani ili amalize vipindi vyake viwili vya uongozi.

  Mwaka 2010, Kikwete atakuwa anamaliza awamu yake ya kwanza ya uongozi wa miaka mitano na anatarajia kuendelea na awamu nyingine ya miaka mitano ijayo na katika kipindi hicho, haruhusiwi mgombea mwingine kujitokeza.

  Endapo Shibuda atachukua fomu, itakuwa ni mara ya pili kwani mara ya kwanza katika awamu ya kwanza ya utawala wake, Rais mstaafu Benjamin Mkapa, aliwahi kupata mpinzani, hali iliyozua mjadala mkubwa nchini.

  Hali kama hiyo pia ilishawahi kujitokeza visiwani Zanzibar ambapo wakati Rais Amani Abeid Karume alipotakiwa kuchukua fomu peke yake ili kumaliza awamu ya pili ya uongozi, Dk. Mohamed Billal alijitokeza naye kuchukua fomu na kumzidi kwa kura Rais Karume, lakini baadaye aliombwa kuondoa jina lake alipofika mjini Dodoma kwenye vikao vya juu vya chama.

  Jina la Shibuda limekuwa likikatwa mara kadhaa au kuwekewa alama ndogo kuanzia mwaka 1998 ambapo jina lake lilifutwa alipowania nafasi ya Mwenyekiti wa Wazazi Taifa, iliyochukuliwa na Idd Simba.

  Mwaka 2002, akiwa mmoja wapiga debe wa mgombea mmoja, alilazimishwa kushushwa kwenye treni wakati akiwa na wajumbe wa NEC kwenda mkoani Dodoma kwa madai kuwa alikuwa akifanya kampeni za kuwaangusha baadhi ya vigogo.

  Nafasi pekee alizogombea mwaka 2005 na kurejeshewa jina lake ni urais na ubunge.

  Waliopitishwa kuwania nafasi ya mwenyekiti taifa na hivyo kumwezesha mshindi kuingia ndani ya vikao vya Kamati Kuu (CC) ni Alhaji Abdallah Bulembo, Athuman Juma Mhina na Esther Nyawazwa, wakati waliopitishwa kuwania umakamu ni Khamis Suleiman Bad, Haidar Haji Abdallah na Dogo Idd Madrouk.

  Mkoani Shinyanga waliopitishwa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa Wazazi ni Vestus Ngasa Lukango, Asha Ramadhani Kanyongela na Bernad Maduhu Itendele.
   
 12. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Uteuzi mgombea urais CCM 2010: Kanuni zitazua mtafaruku?

  2008-09-24 08:51:18
  Na Ani Jozeni


  Minong`ono imeanza katika ngazi tofauti za CCM kuhusu uwezekano wa watu wengine kuchukua fomu kutaka kugombea kuteuliwa na chama kuwa washika bendera yake uchaguzi mkuu ujao.

  Katuni moja hivi karibuni ilimchora kipanya akimuuliza JK kama ana habari kuwa wapo wana-CCM wanataka kuchukua fomu, halafu JK anajibu `you think so? Sidhani.`

  Jibu hilo la katuni linatosheleza mantiki halisi, suala hilo liko katika fikra tu.

  Kuna aina fulani ya uchangamfu sasa hivi kuhusu wakinzani kadhaa wa JK kuchukua fomu, kutokana na kuelemewa na matatizo ya aina tofauti, na pia kutokana na fikra ya kawaida tu kuwa wana uhuru wa kufanya hivyo.

  Hali hiyo imekuwepo miaka yote kuanzia pale uchaguzi wa vyama vingi ulipoingia na kutoa changamoto ya demokrasia ndani ya CCM yenyewe, hivyo inaweza kuonekana kama kuchukua fomu kushindana na JK ni sehemu ya ukuaji huo wa demokrasia. Katika hali halisi suala ni tofauti - ni kama uasi dhidi ya JK.

  Hivyo suala linalohitaji mjadala lina pande mbili, kwanza ni misukosuko ya hivi sasa na kama inaweza kuleta `uasi` dhidi ya JK, yaani watu mashuhuri kadhaa wajitokeze kuchukua fomu dhidi yake, na uongozi wa juu wa CCM ugawanyike kuhusu kuwadhibiti.

  Ni wazi kuwa hapa yapo masuala mawili, kuwa siyo tu kwamba yuko mtu fulani anaweza kutaka kushindana na JK katika uteuzi kutokana na `kukithiri kwa rushwa` au sababu nyingine, ila pia kama uongozi wa chama utagawanyika kuhusu suala hilo.

  Kinachohitaji kufafanuliwa hapa ni kuwa ngazi zote mbili haziwezekani au hazitakuwepo, kwanza ndani ya CCM kwenyewe ionekane kuwa JK ameshindwa kazi kiasi ambacho hata ndani ya ngazi za juu kama Kamati Kuu na Halmashauri Kuu theluthi ya wajumbe wamtake mtu mwingine.

  Na inabidi kwanza ifikie hapo ili suala la kujadili kutenguliwa kanuni kuwa rais aliyeko madarakani hapati mpinzani katika kuingia muhula wake wa pili zibadilishwe.

  Kwa maana hiyo suala kama hilo haliwezi kuzuka ndani ya CCM, na kwa vile haliwezi kuzuka, haliwezi vile vile \"kutafutiwa`` kanuni.

  Makamu wa mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, ni mtaalamu wa suala la kanuni kuwa inabidi ziendane na uelekeo wa chama, kwa maana ya katiba na miongozo ya uthabiti wa chama kwa jumla, na siyo tu kwa vile uko upande wa maoni ndani ya chama unaosema kuna haja ya kubadili au kufafanua kanuni.

  Mwaka 1978 mwezi Machi, akiwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM, alipokea ombi la maandamano ya Umoja wa Vijana tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuhusu wabunge kupewa `gratuity` (kiinua mgongo) cha sh. elfu 40 (karibu sawa na milioni 20 sasa).

  Alikataa ombi hilo akisema yako maandamano ya aina tatu ambayo chama kinayatambua, yaani yale ya kitaifa, ya makundi kwa mwito wa kitaifa, au itikio maalum.

  Hili la mwisho linahusu suala linalotambuliwa kitaifa kwa mfano kuna haja ya maandamano kupinga kitu fulani kwa mwitikio wa kitaifa, na siyo pale kunafumuka kundi fulani la watu wapange maandamano yasiyofahamika kitaifa, yaani siyo itikio.

  Hivyo hapakuwa na `category\' (fungu) la aina ya maandamano waliyokuwa wanataka kufanya Umoja wa Vijana wa tawi la Mlimani na kwa maana hiyo ilibidi ombi hilo likataliwe.

  Licha ya kuwa sasa mantiki ya siasa ni tofauti kidogo, suala hilo la `fungu` la kanuni bado lipo.

  Kwa maana hiyo, inawezekana kabisa kusema kuwa hapatakuwa na hoja ya kubadili kanuni za uchaguzi katika CCM ili JK ashindanishwe na huyu au yule kwa sababu ya kile kinachodhaniwa ni udhaifu katika utendaji.

  La kwanza katika kuainisha hilo ni kuwa udhaifu huo unaonekana kwa dhati zaidi kwa wapinzani kuliko ndani ya CCM, ambako maelezo aliyotoa JK katika hotuba yake yalikidhi hisia na matazamio ya wengi, au kuondoa wasiwasi pale hata wakereketwa walipoanza kuwa na wasiwasi.

  Licha ya masuala magumu bado kuwepo, si rahisi kumkejeli JK ndani ya CCM, sasa.

  Licha ya mafanikio ya kuwavuta wana-CCM nyuma yake, kuna suala rahisi tu la mtazamo wa kawaida wa kisiasa katika tawala yoyote ndani ya nchi, na si Afrika peke yake, kuwa utawala uliopo ndiyo `makutano` ya fikra na malengo ya makundi tofauti yanapokutana.

  Haiwezekani kuanzisha upya makutano hayo kuhusu sera na nini kinatakiwa kufanyika bila kufikia tamati halisi ya awamu hii, ambayo ina maana ya uchaguzi mkuu wa 2015.

  Pale ndipo dukuduku zote CCM zitatolewa, si kuhukumu uongozi uliopo ila katika kupambanua uelekeo wa CCM kwa uchaguzi huo, na awamu mpya.

  Hivyo ni wazi kuwa msukumo unaoanza kuhusu uwezekano wa kuchukua fomu katika CCM kwa uteuzi wa jina la mgombea urais mwaka 2010 ni dhaifu, kwani unalenga lile suala la mgombea binafsi, lakini kwa haya.

  Kila mtu anajua hakuna mgombea binafsi anayeweza kushindana na CCM na hata upinzani, kwa rekodi iliyopo katika nchi kama Marekani, ambapo wagombea binafsi siku zote wapo.

  Pamoja na kwamba uamuzi mahakamani kuwa kuwazuia ni kukiuka misingi ya katiba (na siyo katiba yenyewe, kwani sheria ya uchaguzi ilitungwa kwa kuzingatia katiba) upo na bado serikali haijatoa pingamizi la maana mahakamani, fomu CCM ni bora zaidi.

  Tayari kuna dalili kuwa baadhi ya wanachama wa chama hicho wanaweza kuchukua fomu za kugombea urais mwaka 2010 ingawa Katibu Mwenezi, John Chiligati amesikika hivi karibuni akisema kuwa chama hicho kitamshangaa mwanachama yeyote atakayefanya hivyo kwa kuwa licha ya katiba kutoeleza chochote kuhusu jambo hilo.

  Baadhi ya wanachama wa CCM waliwahi kuchukua fomu kushindana na marais walioko madarakani mfano Dk. Mohamed Gharib Bilal dhidi ya Karume mwaka 2005 na marehemu Musasa Sabi Munasa dhidi ya Mkapa mwaka 2000, lakini chama kikawazuia.

  Kwa mantiki ya kisiasa, kutazamia kuwa JK atakuwa ameshindwa kuvuta wana-CCM nyuma yake kiasi cha kukimbiwa na hata theluthi ya wajumbe wa mkutano mkuu ni kosa, kwani itabidi anayedhani hivyo aeleze ni hisia gani mbadala zitakazowaunganisha wana-CCM.

  Jawabu rahisi ni kuwa ni pale tu ambapo uongozi uliopo unafikia tamati ndiyo itawezekana kwa watu wengine kutoa taswira tofauti ya maongozi ya nchi na zikawa na uwezo wa `kuwakuna vichwa` wana-CCM kwa makundi makubwa, na siyo kabla.

  Akitaka `muhula wa tatu` atashindwa, siyo kuteuliwa tena 2010.

  Halafu tena kuna suala la kundi gani la watu ambao wanaona kuna stahili fulani ya wazi kutafuta jina la mgombea ambaye anaweza kusimama na JK akawa na nafasi kubwa ya kushinda, hivyo CCM ikawa na mgombea mbadala mwaka 2010.

  Chanzo kimoja lakini ni dhaifu ni yale makundi ya mwaka 2005 ambayo kwa jumla hayajavunjwa, lakini hayana fikra halisi ya maongozi gani yanatakiwa nchini, kiasi cha kujiamini kabisa kuanza kujishindanisha na JK.

  Wengi wanatanguliza tu nafasi zao au umaarufu wao, ambao kamwe hauwezi kuzidi umaarufu wa chama, kama yule kijana Nape Nnauye na wasindikizaji wake walivyoanza kutambua hivi karibuni.

  Chanzo kingine ambacho si dhaifu kiasi hicho lakini hakina uwezo wa kubadili lolote katika mikakati ya chama na kuungwa mkono JK sasa na hadi uteuzi wa mgombea 2010 ni kundi la akina Joseph Butiku, wanaotaka kurudi katika Azimio la Arusha.

  Hao angalau wana kianzio halisi kutafuta mgombea tofauti, kuwa `sababu wanayo, uwezo wa kutafuta mgombea tofauti wanao, na nia ya kufanya hivyo wanayo.`

  Tatizo ni kuwa hata inyeshe mvua ya mawe hawawezi kukiteka chama, na kabla ya muda wa uteuzi mwaka 2010 haujafika, mageuzi ya kuingia soko la pamoja Afrika Mashariki, na mkataba wa biashara huria na Umoja wa Ulaya vitatikisa misingi ya matazamio ya wahafidhina; kurudia Azimio mwaka 2010 kwa mantiki hiyo itakuwa kichekesho. Muda wake uliishia Butiama, majuzi.

  SOURCE: Nipashe
   
 13. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Dada Asha Abdala,

  Sawa endelea ku recycle hizo article mimi simo. Mbunge naye siku hizi ni kiongozi mwandamizi wa serikali?

  Usitegemee waziri kwenye serikali ya JK achukue form ya kumpinga JK mwaka 2010. Hilo sahau kabisa. Labda huwajui CCM wanavyofanya mambo yao. Labda atumwe na JK mwenyewe kama propaganda, vinginevyo hakuna waziri atakayempinga JK 2010.
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160

  Ulivyoanza tu, hapakuwa na haja ya kujua kakutuma nani!! Tusipoangalia hapa JF patakuwa kipimajoto cha CCM na wapambe wao... ni kweli Habari Ndiyo Hiyo!
   
 15. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2009
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyu Amos Makalla si ndio mshiriki mmoja wapo wa mradi wa KIFISADI wa jengo la UVCCM.... Na kumwaga ma signature yake ili kummilikisha haohao mnaowaita waasia, umiliki wa milele jengo lililojengwa kwa michango ya wavuja jasho!... Once FISADI, ALWAYS FISADI.
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thanks Sober,

  Huwa wanasema ukenda vagi la uswahilini weka mawe yako japo matatu mfukoni, watu wakimaliza ngumi ndio unatoa yako... Sasa wewe mbona yako umeanza kurusha hata mtaa wa vagi lenyewe bado?
   
 17. M

  Masatu JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumbe umemstukia eeh...
   
Loading...