Makaidi ajitolea kunusuru 'ndoa' ya Zitto, CHADEMA

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,143
Katika ukurasa wa kwanza wa gazeti la Mwananchi la leo,kuna habari isemayo "Makaidi ajitolea kunusuru ndoa ya Zitto,CHADEMA". Kwenye habari hiyo inayoandikwa katika kurasa za 1 na 4, Mwenyekiti huyo mwenza wa UKAWA na NLD Emmanuel Makaidi amekaririwa akidai kuwa Zitto alimuomba kumpatanisha na Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe. Makaidi amedai kuwa sasa yu tayari kuanza kazi aliyoombwa na Zitto kwakuwa Mbowe anaingilika na ni mtu makini,safi na muungwana.

Lakini,Zitto alipoulizwa kuhuu hilo alikana na kusema kuwa kama kuna haja ya kufanya hivyo atakaa na Mbowe na kuyamaliza. Pia Zitto amesema kuwa asilazimiswe kuingia UKAWA kwa njia ya CHADEMA tu kwakuwa aweza kuingia UKAWA kupitia CUF,NCCR-Mageuzi au ACT-Tanzania. Alisema "Huyu mzee ni mtu ninayemheshimu sana na juhudi zake ni nzuri,lakini sijawahi kuzungumza naye kuhusu kupatanishwa na chama changu,sisi wenyewe tuna uwezo kukaa wawili na kuyamaliza,jitihada zake kwasasa hazijahitajika"

Baada ya kukana kumuomba Makaidi, Makaidi amesema " amekana huyu Bwana,haa! Tulikutana pale kantini Bungeni,aweza kukutajia namashhidiwaliokuwapo,laini mimi nilikuwa nafuatilia jinsi ykumuingia huyoBwana mkubwa wa CHADEMA na sasa naona inawezekana."

Lengo ni zuri. Lakini mkweli ni nani?
=======================

Naamini makaidi yuko kweli ila huyu bbwana mkubwa zitto anaona akikubali ataonekana desparate sana na anathani itamshushia hadhi. Tatizo la zitto ameshajiona mtu wa maana sana ni better kuliko wengine. Mimi nathani anajua hata kama akienda hicho chama alichokianzisha cha ACTS hatafanikiwa kama angekaa chadema. Kujenga chama si kazi nyepesi.

Huyu zitto ni matatizo ready to happen tu hata kwa CHADEMA hata UKAWA. Kwaxushauri huyu bwana mzitto aachwe aende zake huko atakapo. Tuone atafika wapi na uchu wake wa madaraka. WATU WALIO PROUD NI HATARI SANA.
 
zitto ndiye mkweli Kwa ni swala lake linalomuhusu moja Kwa moja.
 
ZZK anatamani kurudi CHADEMA, tatizo anawaza kwamba atamuambia nini 'muasisi' wa ACT Nyakarungu ?
 
.... Mzee Makaidi Hawezi Kusema Uongo, Zitto Siku Zote Huwa Ni Kigeugeu, Haaminiki Hata Kidogo, Si Mnakumbuka Alivyounga Mkono Hoja Ya Chenge Na Kuwaacha Wenzake Njia Panda, Huku Kafulila Akibaki Anapayuka Tu Akisema "Hata Wewe, Hata Wewe....
 
namkubali sana zitto lakini namwogopa, kiburi na kujitukuza vinamharibu
 
Upatanishi wa namna hii hufanywa kwa siri kubwa. Sasa kama Makaidi aliombwana Zittona kukubali kuwa mpatanishi anini aede kwenye magazeti kutangaza? Nafikiri Makaidi anatafuta publicity tu hapa.
 
.... Mzee Makaidi Hawezi Kusema Uongo, Zitto Siku Zote Huwa Ni Kigeugeu, Haaminiki Hata Kidogo, Si Mnakumbuka Alivyounga Mkono Hoja Ya Chenge Na Kuwaacha Wenzake Njia Panda, Huku Kafulila Akibaki Anapayuka Tu Akisema "Hata Wewe, Hata Wewe....
Mzee Makaidi ni mtu muongo sana, ni mzee mmoja mp.umbavu na wa ovyo kweli huyo mzee hupenda kuingilia mambo yasiomuhusu, matatizo ya CDM yanamhusu nini yeye.

Sent from my SM-G800H using Tapatalk
 
Katika yote haya kitu kilichomtoa Zitto jeuri na mbwembwe zake si kingine bali ni UKAWA kusema kweli huu ndio umekuwa mwiba mkali kwake na wengine kadhaa halafu ile ACT yake ikaanza kukata roho kabla haijazaliwa,waasisi wakawatolea uvivu kina Mwigamba na Mkumbo.
Zitto akaona hana pakutokea mbele ya UKAWA hana jinsi ya kwenda NCCR Mageuzi wala CUF achilia mbali Chadema,na kwa kina Mwampamba na Shonza wakuu wa kaya wasingemhitaji kazi yao aliyopewa kashindwa kuitimiza, sasa kabaki katikati kama ulimi juu meno chini meno.
Nawashauri Chadema wasijisumbue naye tena vinginevyo watajutia uamzi wao.
 
Kwa takwimu zilizopo ni kuwa Zitto ana mgogoro na taasisi iliyokatika mfumo wa chama cha siasa. Taasisi hiyo inaitwa CHADEMA. Kupatanishwa Zitto na Mbowe hilo nalisikia leo , sikujua kama wana mgogoro.

==================================================================================
Mwenyekiti huyo mwenza wa UKAWA na NLD Emmanuel Makaidi amekaririwa akidai kuwa Zitto alimuomba kumpatanisha na Mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe. Makaidi amedai kuwa sasa yu tayari kuanza kazi aliyoombwa na Zitto kwakuwa Mbowe anaingilika na ni mtu makini,safi na muungwana.

Lakini,Zitto alipoulizwa kuhuu hilo alikana na kusema kuwa kama kuna haja ya kufanya hivyo atakaa na Mbowe na kuyamaliza. Pia Zitto amesema kuwa asilazimiswe kuingia UKAWA kwa njia ya CHADEMA tu kwakuwa aweza kuingia UKAWA kupitia CUF,NCCR-Mageuzi au ACT-Tanzania. Alisema "Huyu mzee ni mtu ninayemheshimu sana na juhudi zake ni nzuri,lakini sijawahi kuzungumza naye kuhusu kupatanishwa na chama changu,sisi wenyewe tuna uwezo kukaa wawili na kuyamaliza,jitihada zake kwasasa hazijahitajika"
 
Makaidi nae kama ni kweli busara ilimpotoka, huwezi kuombwa kusuluhisha kwa siri alafu wewe ukaenda kutaarifu vyombo vya habari ata kabla hujaanza usuluhishi na pia huwezi kutangaza jambo kama hilo bila ruhusa ya aliyekuomba usuluhishi, huu ni upungufu wa busara tu.

Kwa umri wake alipaswa ajue kuwa wakati wa kuongea na vyomba vya habari ulipaswa uwe ni wakati wa kutangazwa kamaliza upatanisho, sio ata kabla hajaonana na mhusika mwingine wewe umewahi kwenye vyombo vya habari.Ni kama vile nae Makaidi anatafuta umaarufu kupitia hilo.Ata ningekuwa mimi ningemkana tu na kumuondoa kabisa kwenye watu wanaopasa kufanya usuluhishi.
 
Upatanishi wa namna hii hufanywa kwa siri kubwa. Sasa kama Makaidi aliombwana Zittona kukubali kuwa mpatanishi anini aede kwenye magazeti kutangaza? Nafikiri Makaidi anatafuta publicity tu hapa.

Nashukuru umeliona hilo pia, Mzee Makaidi hapa kaaibisha wazee, alikuwa na haraka gani ya kuwahi kwenye vyombo vya habari ata kabla hajaonana na Mbowe?je aliruhusiwa na Zitto kutangaza kwenye vyombo vya habari?

Lakini pia sehemu yenyewe walipokutana, mgahawa wa bunge, inahashiria kuwa zilikuwa ni story zisizo rasmi, sasa Mzee akatoka nazo kama zilivyo kwenye vyombo vya habari.
 
Mzee Makaidi ni mtu muongo sana, ni mzee mmoja mp.umbavu na wa ovyo kweli huyo mzee hupenda kuingilia mambo yasiomuhusu, matatizo ya CDM yanamhusu nini yeye.

Sent from my SM-G800H using Tapatalk
sema uwezavyo, zitto haeleweki japo ni mwanasiasa mzuri!
 
Kweli mkuu mzee makaidi kakosea sana, kama Zitto aliweza kumfata kwa siri basi na sio magazetini basi Mzee makaidi naye ilimpasa kuendesha reconciliation kwa siri na sio kwa njia kama hii ya magazetini, Matokeo ya upatanisho ndiyo yalitakiwa yawe magazetini na sio mchakato. OVER
 
Last edited by a moderator:
CHADEMA SIO MBOWE, amekihujumu chama sio MBOWE hata iweje ZZK hatumtaki CDM. Kama wanapatanishwa ni kwenye dili zao zingine kama zipo sio kuhusu CDM
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…