Makadirio ya mapato ya Askofu Gwajima

Makadirio ya mapato ya Askofu Gwajima

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,618
Wanabodi,

Kama ni kweli Ngwajima ana waumini wasiopungua elfu sabini na wanaenda kanisani mara mbili kwa wiki basi Ngwajima anaingiza zaidi ya bilioni tatu kwa mwaka (makadirio ya chini kabisa)

NI HIVI:
Tufanye kila muumini wake hutoa sadaka ya sh. 500 tu-hiyo ni flat rate, ina include waliotoa elfu kumi, waliotoa sh mia na wasio toa kabisa.

Hivyo basi kwa siku moja kwa waumini 70,000 wakitoa sh 500 ni sawa na sh milioni 35. Kwa wiki wanaenda mara mbili hivyo ni sawa na sh milioni 70.

Kama kwa wiki anaingiza milioni 70, je kwa mwezi anaingiza kiasi gani? Uki cross multiplication utapata milioni 280

Kama kwa mwezi anaingiza milioni 280, je kwa mwaka anaingiza kiasi gani? uki cross tena multiplication utapata bilioni 3 na milioni 360. Sasa piga hesabu kwa miaka yote aliyotoa huduma ameingiza sh ngapi?

Kwa mantiki hiyo pesa aliyonunulia Hummer aliipata ndani ya mwezi mmoja tu.

Achilia mbali fungu la kumi na pesa mbali mbali anazopewa kama zawadi, hapo tumepiga hesabu ya sadaka tu.

NAMALIZIA, Biblia inasema "vya madhabahuni vitaliwa na wamadhabahuni" full stop.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)
 
Last edited by a moderator:
Watu wanaacha kupga mahesabu ya TRA jinsi yanavoliwa na maCCM mnakuja na vijihesabu vya kataasis ambako hata hakatugusi wengine, acheni majungu nyiny, lete hesabu zenye maslahi mapana ya nchi bwana mnaboa sana
 
Kweli mkuu haya makitu ya ccm ni baraaa

swissme
 
Huyu mhuni mambo ya Mungu muachie Mungu mwenyewe.Vihesabu gani unapiga wewe mapato ya kumtolea Mungu?Hata zinge kuwa nyingi au chache kiasi gani mtu anatoa kutokana na Mungu alivyo mbariki.Na mwakilishi wa Mungu ndiyo hao watumishi.Wanao toa unafikiri wajinga sana na wewe ubaki kuwa una akili?Nina hakika wewe ni mbumbu wa mambo ya Mungu.Wengi wa watoaji huja makanisani wakiwa hohe hahe halafu wanabarikiwa na kuinuka na kisha nao humtolea Mungu.Wao wanajua siri hiyo we hujui.
 
Bado huja pigia hesabu za mawasilisho ya sadaka za matawi ya chini!
 
unahis umegusa hisia za watu hapo ?

hzi bando zinazopatikana maeneo ya chuo bora zifutwe tuu , umeona sasa matokeo yake watu wanakuja kuandika sh. ndogo za gwajima unaacha kuzunfumzia tegeta escrow, epa, ....

kwel maisha bila unafki hayaendi
 
kumbe jamaa haliibi bana.
si ajenge kanisa sasa
 
Tuwekee na makadirio ya matumizi a.k.a gharama za uendeshaji.
 
Hata kama bilioni 203 sasa wewe zinakuhusu nini? Wewe unakosali mnapata sh. Ngapi?
 
hizi imani zingine nazo inawezekana zikawa ni vichaka vya wezi tu.
(ewe Mungu tuepushie mbali)

Wanabodi,

Kama ni kweli Ngwajima ana waumini wasiopungua elfu sabini na wanaenda kanisani mara mbili kwa wiki basi Ngwajima anaingiza zaidi ya bilioni tatu kwa mwaka (makadirio ya chini kabisa)

NI HIVI:
Tufanye kila muumini wake hutoa sadaka ya sh. 500 tu-hiyo ni flat rate, ina include waliotoa elfu kumi, waliotoa sh mia na wasio toa kabisa.

Hivyo basi kwa siku moja kwa waumini 70,000 wakitoa sh 500 ni sawa na sh milioni 35. Kwa wiki wanaenda mara mbili hivyo ni sawa na sh milioni 70.

Kama kwa wiki anaingiza milioni 70, je kwa mwezi anaingiza kiasi gani? Uki cross multiplication utapata milioni 280

Kama kwa mwezi anaingiza milioni 280, je kwa mwaka anaingiza kiasi gani? uki cross tena multiplication utapata bilioni 3 na milioni 360. Sasa piga hesabu kwa miaka yote aliyotoa huduma ameingiza sh ngapi?

Kwa mantiki hiyo pesa aliyonunulia Hummer aliipata ndani ya mwezi mmoja tu.

Achilia mbali fungu la kumi na pesa mbali mbali anazopewa kama zawadi, hapo tumepiga hesabu ya sadaka tu.

NAMALIZIA, Biblia inasema "vya madhabahuni vitaliwa na wamadhabahuni" full stop.

Posted by: MCHUNGUZI HURU (Associate Professor)
 
Thread ya kipuuzi sana! Mambo ya mapato ya TRA tunayaacha, tunajadili ya Gwajima! Ndio maana tutaendelea kuliwa tu, maana hakuna namna!
 
Back
Top Bottom