GE2025 Makada wanne wajitokeza kumrithi Ndugai

GE2025 Makada wanne wajitokeza kumrithi Ndugai

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Wagombea 24 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamechukua fomu kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea ubunge wa Jimbo la Kongwa, kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge mstaafu na Mbunge wa jimbo hilo, Hayati Job Ndugai. Tukio hilo limefanyika jana, Agosti 12, 2025.

Hatua hiyo inafuatia uamuzi wa CCM kuanza upya mchakato wa kujaza nafasi hiyo, baada ya Hayati Ndugai kuibuka mshindi kwenye kura za maoni zilizopigwa Agosti 4, 2025, ambapo alipata kura 5,690 na kuwashinda wagombea wengine tisa waliopitishwa na vikao vya juu vya uteuzi wa chama.

Soma pia: Kumbukumbu alizoacha hayati Ndugai ni lile Soko la Ndugai na Mtaa wa Salasala kwa Ndugai

Screenshot 2025-08-13 013420.png


Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala, amesema kati ya wagombea 24 waliochukua fomu, watatu ni wanawake na 21 ni wanaume.

“Wale wote tisa waliopitishwa na Kamati Kuu ya CCM Taifa pamoja na Hayati Ndugai wamechukua fomu. Pia, tunazo sura mpya 10 katika idadi hiyo,” amesema Mkaugala.
CCM Wilaya ya Kongwa ilitangaza kuanza upya mchakato wa kuchukua fomu Agosti 11, 2025, mara baada ya kumalizika kwa shughuli za maziko ya Hayati Ndugai.

Chanzo: Nipashe digital
 
Naomba kufahamu kifungu katika kanuni za utaratibu wa kura za maoni ccm..kurudiwa inapotokea mmoja wa watia nia waliopitishwa anapofariki..
 
Siku chache baada ya kuzikwa kwa aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Kongwa, Hayati Job Yustino Ndugai, mchakato wa kisiasa wa kujaza nafasi ya ubunge wa jimbo hilo umeanza upya kwa kasi

Mnamo Siku ya jana Agosti 12, 2025, jumla ya wanachama 24 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walichukua fomu kuomba ridhaa ya chama kugombea nafasi hiyo. Kati yao, watatu ni wanawake na 21 ni wanaume

Takwimu hizo zimetolewa na Katibu wa CCM Wilaya ya Kongwa, Joyce Mkaugala, ambaye amebainisha kuwa waombaji hao wanajumuisha wagombea tisa waliopitishwa awali na Kamati Kuu ya CCM Taifa pamoja na Hayati Ndugai, sambamba na sura mpya 10 zilizojitokeza katika kinyang’anyiro hicho

Soma pia: GE2025 - Kifo cha Ndugai Charudisha Mchakato wa Kura za Maoni Jimbo la Kongwa; Fomu kuchukuliwa leo Jumanne Agosti 12, 2025

Hatua ya CCM kuanzisha mchakato mpya imekuja kufuatia kifo cha ghafla cha Hayati Ndugai, kilichotokea muda mfupi baada ya kushinda kura za maoni za chama mnamo Agosti 4, 2025, ambapo alipata kura 5,690 na kuwashinda wapinzani tisa waliokuwa wameteuliwa kushiriki hatua hiyo. Baada ya maziko yake yaliyofanyika Agosti 10, 2025, CCM Wilaya ya Kongwa ilitangaza rasmi kuanza kuchukua fomu kuanzia Agosti 11, 2025

Job Yustino Ndugai alihudumu kama Mbunge wa Kongwa kwa muda wa zaidi ya miongo miwili, akiwa pia Spika wa Bunge la 11 (2015–2022)

Alijulikana kwa msimamo thabiti wa kulinda kanuni za Bunge na kuhimiza nidhamu kwa wabunge. Kabla ya kuwa Spika, alishika nafasi ya Naibu Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2010 hadi 2015

Katika kipindi cha uongozi wake, Ndugai alihusishwa na juhudi za kuimarisha utendaji wa Bunge na kuendeleza shughuli za maendeleo katika jimbo lake, hususan sekta za elimu, miundombinu, na maji.

Mchakato wa uteuzi wa mgombea atakayewakilisha CCM katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa utahusisha hatua kadhaa, kuanzia kuchukua na kurudisha fomu, usaili, kura za maoni ndani ya chama, hadi uteuzi wa mwisho na Kamati Kuu ya CCM Taifa

Chanzo: Manara TV
 
Wazalendo na wapenda maendeleo wanataka Sana kuitumikia nchi yao, kila la heri kwao!!
 
Maisha yanaendelea huku duniani, na maisha pia yanaendelea huko kaburini.

Cheo chako tayari watu wanakitaka tena kwa wingi wanakigombania, inawezekana pia wajane wamepata wafariji ndugu, jamaa na marafiki, Mali zako pia zimeshaanza kupigiwa hesabu nk.

Somo, tuishi kwa wema na haki huku tukimtii na kumcha Mwenyezi Mungu maana maisha ya duniani ni mafupi na ubatili mtupu.

ndani ya mitaa ya Kabul Afghanistan.
 
Atakaeshinda apewe na ile fimbo aliyokua anatembeaga nayo
 
Back
Top Bottom