Makada wa CCM wawatisha mahakimu na kufunga mahakama

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
22,378
19,216
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mahakama wilayani Bunda zimeshindwa kufanya kazi baada ya makada wa CCM wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi kuwatisha mahakimu wanaohudumu ktk mahakama hizo.

Mahakimu hao wameogopa kufungua mahakama na kuwahudumia wananchi baada ya kupokea vitisho vya kuuawa na watuhumiwa hao wa ufisadi. Kabla ya kuamua kusitisha huduma kwa wananchi, mahakimu hao walifanyiwa vurugu wakiwa mahakamani na kuponea chupuchupu kuumizwa.

Mahakimu wote mkoani Mara wameapa kuwaunga mkono wenzao na wanataka uchunguzi ufanyike ili kuwakamata na kuwachukulia hatua makada hao; na pia wameomba mahakimu wapewe ulinzi wa polisi vinginevyo hawatafanya kazi ng'o.

Mtuhumiwa mkuu katika kadhia hii ya vitisho kwa mahakimu ni mbunge (ambaye hakutajwa jina) akishirikiana na makada kadhaa wa CCM wanaotuhumiwa kwa tuhuma za ufisadi.


Source
: ITV

MAONI YANGU:
Naona sasa makada hawa wamefika hatua mbaya sana. Kitendo cha mafisadi kuwatisha mahakimu ni cha hatari sana. Tunapaswa kuwalaani watu hawa.
 
CCM sasa wamefika kiwango cha juu kabisa cha UFISADI hadi kufikia hatua ya kuwazuia mahakimu kufanya kazi zao. Ee Mungu tuondolee ukoo huu panya katika utawala wa nchi hii. Amina.
 
Chama bado kimeshika hatamu, CCM ndiyo wenye serikali ndugu, ukitaka mafanikio haramu jiunge na ccm, haguswi mtu hapo.
 
Uzushi tu, na siku hizi mmegundua mbinu nyingine ya kuandika source za uongo. Na bahati mbaya mods hawafuatilii.
 
Uzushi tu, na siku hizi mmegundua mbinu nyingine ya kuandika source za uongo. Na bahati mbaya mods hawafuatilii.

kama unataka ushahidi nenda ITV wakupe video waliyorekodi kwenye taarifa ya habari ya saa 2 usiku jana. Mimi nimetazama tu sikufanikiwa kurekodi ushahidi. Kama utaona vipi nenda mahakamani mimi nitakuja kutoa ushahidi huko. taarifa ile ilitazamwa na dunia nzima, haina ubishi. Kama unadhani mods hawajafuatilia, wasaidie wewe. Nenda kaombe mkanda ITV, si unajua ofisi zao zilipo?
 
maCCM yanajua yanaongoza maiti ndio maana hayana wasiwasi wowote.
 
Uzushi tu, na siku hizi mmegundua mbinu nyingine ya kuandika source za uongo. Na bahati mbaya mods hawafuatilii.

ITV ni source ya uongo? Kumbe source ya ukweli ni TBCCM na Redio Uhuru tu? Wewe si bure, kama hujaumuwa DENGUE utakuwa UMEROGWA!
 
kuna siku serikali hii ya CCM itakuja kufuta mahakama zote nchini ili waendelee kufanya UFISADI bila kushitakiwa.
 
Back
Top Bottom