Makada Mmekumbuka Shuka Wakati Jua Limechomoza

Chademakwanza

JF-Expert Member
Jun 11, 2014
6,346
1,871
Nchi hii imenichukua miaka 23 kuisoma tabia ya wanaccm ,kadri ya siku zilivyosonga ndipo nilipokubaliana na kauli ya Yesu kristo kuwa"ufalme hauwezi kujifitisha"

Wakati tunamwingiza Rais jk Madarakani tuliambiwa chaguo la Mungu,kijana na anajua shida za vijana na watanzania.

Kikwete aliingia na gia kali ya;

* kurudisha nyumba zetu za serikali zilizouzwa kipindi cha Mkapa,
* kuhakikisha anaunda baraza la Mawaziri litakaloendana na kasi,

* Anapambana na rushwa,na maeneo mengi kutaboresha

Kilichotokea tangu 2005-2015 watanzania wanajua.
Leo simchambui Mzee huyu,lakini nijikite kwenye Mada.

Ikiwa jumapili saa 8:10 Taasisi ya Mwalimu Nyerere ilikuwa na mdahalo pale Blue Pearl hotel,lengo ni kujadili maadili kuelekea uchaguzi mkuu,nilichoona si maadili bali ni mkakati wa wanufaika wa serikali hii kutetea kitumbua kilichokaribu kuingia mchanga.walitafuta figure people ili wasaidie kusherehesha safari ya kwenda Ikulu kwa watu walewale wanaoamini wao ni wajuvi kuliko wenzap,wenye hati miliki ya nini kifanyike nchi hii.


Kwa ukaribu Mzee Butiku alifafanua tu maana ya MAADILI kwa kutumia kamusi ya kiingereza na kiswahili akisema;
" accumulation defenciency and failure of democracy strategies of our problem,it involve
* failure to respect UN charter
* failure to respect AU constitution ethics
* failure to rrspect our Nation Constitution

The result is
- use of force
-impunity
-Exclusion
- Gender
- Marginalization
- Massive civil war
Aidha akasema,Mwalimu Nyerere alituandikia vitabu hivi "Tujisahihishe,Utawala wa chama kimoja nk.


Mjadala ulisimama baada ya Polepole kusimama kutoa mada yeye akajita kusema haya"

Niliwaonya ccm ikiwa watachagua fisadi nitazunguka nchi nzima kusema ccm isichaguliwe"

Lakini akasema pia akiwa ndani ya katiba alisema Maslahi binafsi,nayavyama yalishinikiza mambo tuliyoyaona,miongoni mwao ninawajua( japo hakututajia)

Inaonesha Polepole anatupa ujumbe kuwa ccm imewang'oa mafisadi sasa ipo salama( japokuwa wote waliogombea nafasi ya urais wameingizwa kwenye kamati ya kampeni ya watu 32)


Butiku akasema" Mwalimu alipenda ccm imeguke,isiwe mwiko watu kuondoka ndani ya ccm kama wanaona hawakubaliani na utaratibu( hapa inamaana waliohama hawakubaliani na utaratibu,waliobaki wamekubaliana nao)

Alienda mbali kwa hasira kusema" kosa walilofanya ni kubaki ndani ya ccm kwa muda miaka yote wakati hawakubaliani na chama( hapa alimaanisha ccm haina kanuni za kuwajibisha kwa mwanachama anayeonekana kuvunja maadili hivyo huachwa ajiondokee mwenyewe)


Aliendelea kusema" Mtandao wa watu 10,waliohama chama wamo,watu hawa wanasema kuna mizengwe,hawataki utaratibu,wanataka holela,wajuaji,tunawachelewesha kutajirika,watoke chadema wapokeeni"

Kwa hoja hii inamaana waliotoka ndio wanataka utajiri ila waliobaki si matajiri

Mzee butiku atuambie ni mwanachama yupi wa ccm anayezingatia utaratibu? ( hasa kura za maoni)

Je,ccm ilipokuwa inavunja Azimio la Arusha kule Zanzibar waliohama nani alikuwa M/ kiti wa kikao?

Je,imekuwaje wanaccm,waandishi wa habari leo kusimama kuwasema( Lowassa kuwa fisadi huku matajiri wakioingiza nchi kwenye mikataba ya aibu wakifumbiwa macho?)


Mzee Butiku na wanaccm watuambie,chama hiki kikongwe ni wapi kimewahi kuwawajibisha wamamtandao,au ccm ni kichaka cha kufichia wezi?

Mkakati wa kujivua gamba kwa nini ulikwama?

Ninachojua,ccm wanajua kukiuka kanuni na sheria,ndio walioua Katiba ya warioba,ndio hawataki mikataba ya gesi na Madini kuwekwa wazi hawa haaajatuambia Mabasi ya UDA ni ya nani nk!

Siamini Magufuli ndio Mwarobaini wa wezi wa Fedha za halmashauri wakati anaingia huko ccm ikiwa imefuta maadili ya Azimio la Arusha!

Siamini kama Lowassa utajiri wake unatiliwa shaka kuwa wakifisadi huku;

* wakati inamsema ni fisadi baada ya kujiuzuru 2008 hakuna hata kesi moja waliyomfungulia?🔴

* baada ya Kujiuzuru,Kikwete alienda kumnadi Lowassa Monduli kuwa Mgombea Ubunge!🔴

* Baada ya kuingia Bungeni,alichaguliwa kuwa M/ kiti wa kamati ya Mambo ya nje ( huku si mtu safi!🔴

* baadaye akachaguliwa kuwa M/ kiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama,( huku chama hiki hiki kinachosema si msafi,anakumbatia matajiri akina Manji,Rostam,Ns Mengi kikamwamini nafasi hii!)

Makada wa ccm waambieni watanzania pamoja na mikakati ya kupandikiza chama cha Act wazalendo kwa Gharama kubwa huku bara kuua Chadema na ADC kule zanzibar na Hamad Rashid kuua Cuf,

Mtueleze,ccm nini msimamo wake kwa makada kinaowaona ndani ya chama hawafai?

Kwa nini kimeanza yaleyale ya Mrema kilipoona hatima yake inapotea?

Ikiwa ccm inaweza kumvumilia Lowassa,kinawezaje kuacha kuvumilia Rushwa za uchaguzi,kinashindwaje kuwavumilia wezi wa fedha za halmashauri,kinashindwaje kuvumilia wauza unga,kinashindwaje kuvumilia walioua viwanda vyetu,kinashindwaje kuvumilia walioua ATC,kinashindwaje kumvumilia jamaa wa chenji ya RADA na wenzake?

Watanzania,tunahitaji kujua kuwa" Tunawatu wametujengea Utumwa wa Fikra kuwa wao ndio kila kitu,wanajua kuliko watanzania,wanaloamini wao na wanawataka watanzania kuwa fikra zao ndio sahihi"!!


Fikiri nje ya boksi
 
Yan mwaka huu ccm lazima uiadhibu kwa kipigo cha mbwa mwizi, wametutesa kwa muda mrefu, wameiba kwa muda wa miaka 54, wamefuga mijizi na mila rushwa kwa muda mrefu. wamefanya chama ni cha kifalme, mtoto kumrithi baba na kueana vyeo kirafiki, kindugu na kiukoo! sasa haya yote na mengine mengi mwisho wake OCt 25
 
Naona we pohamba ndio walewale ccm ishawapa mlungula kuwadanganya watu kuwa uchaguzi hautakuwa huru ili tusipige kura, umefel hapo hatudanganyiki (we need change) tumeichoka ccm ya mafisadi.
 
Naona we pohamba ndio walewale ccm ishawapa mlungula kuwadanganya watu kuwa uchaguzi hautakuwa huru ili tusipige kura, umefel hapo hatudanganyiki (we need change) tumeichoka ccm ya mafisadi.
Je, mafisadi wa escrow wamehamia chama gani?
 
Back
Top Bottom