Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linaendelea kuwahoji maofisa kadhaa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuhusiana na tuhuma za kuruhusu usafirishaji wa twiga wanne kwenda Uarabuni bila kibali.
Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Lucas Ngh'oboko, aliiambia NIPASHE kuwa uchunguzi huo unaendelea, lakini alisema kuwa twiga hao walitokea mkoani Arusha.
"Maofisa hao wa KIA walikiuka taratibu. Tunachunguza kuona nini kilitokea," alisema Ngh'oboko. Alisema maofisa wa polisi wako kazini kupitia nyaraka na vibali, ambavyo wanaendelea kuvitafuta.
Kamanda huyo alisema taarifa zikikamilika, polisi watatoa taarifa.