Makabidhiano salama kwenye Maisha

Makabidhiano salama kwenye Maisha

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,252
Reaction score
79,804
MAKABIDHIANO SALAMA KWENYE MAISHA

Anaandika, Robert Heriel

Andiko hili laweza somwa na mtu yeyote. Halibagui mtu yeyote yule.

Leo nitaangazia jambo muhimu sana ambalo wakati mwingine baadhi yetu hatizingatii.

Je umewahi kusikia mtu akisema; amekabidhiwa Mkoba?
Kwa watoto wa siku hizi huenda neno hilo Likawa geni masikioni mwao lakini kwa watu wa miaka ya tisini Kurudi nyuma wengi wetu tunalifahamu.

Tunalifahamu kutokana na umuhimu wake Katika zama zetu lakini pia hata sasa umuhimu wake upo licha ya kuwa hauuonekani.
Maisha ya mwanadamu yanahitaji Makabidhiano ili yawe mazuri na salama. pasipo makabidhiano maisha ya mwanadamu hugeuka kama maisha ya mnyama.
Ni maisha hatari yasiyo na usalama ndani yake

Kwenye koo au jamii zisizo Na makabidhiano hujikuta wakitanga tanga huku na huko kama vikaragosi vinavyopeperushwa na upepo.
Makabidhiano ni kitendo au mfumo wa kupewa mtu au kitu au jambo kiwe chini ya uangalizi na uongozi wa mtu au chombo fulani.

Kitu au mtu ambaye hajakabidhiwa usalama wake ni mdogo na mwisho wake hauwagi mzuri.

Aina kuu za Makabidhiano
1. Makabidhiano ya Kifamilia
2. Makabidhiano ya kiuchumi
3. Makabidhiano ya Kiroho
4. Makabidhiano ya Kisiasa
5. Makabidhiano ya Kifikra

1. MAKABIDHIANO YA KIFAMILIA
Hii ni ile hali au kitendo cha kupewa mamlaka ya kuongeza, kuratibu na kusimamia familia, au ukoo.
Familia makini na koo Bora lazima ziwe na utaratibu wa Makabidhiano. Ili familia iwe na nguvu lazima awepo wa kuiongoza anayefahamika.

Baba ndiye mwenye mamlaka ya kukabidhi familia mikono salama. Kikawaida Baba huikabidhi familia mikononi mwa Mama(mke wake) pale aondokapo au afapo. Pia Kwenye jamii nyingi duniani Anayekabidhiwa familia ni mtoto wa kwanza wa kiume.
Huyo atapewa mamlaka yote ya kuongoza na kuwasimamia ndugu zake.

Kibiblia tunamuona Yesu Kristo akifanya Makabidhiano ya kifamilia kwa Ndugu yake Yohana, akimwambia amtazame Mama yake(Mariamu) sio kwamba Baba(Mume wa Mariam)hakuwepo hasha! Alikuwepo lakini Yesu kama mtoto wa kwanza kwenye familia ya Yusufu anatekeleza wajibu wake wa kumteua Yohana kama Mwangalizi wa Mama yake siku akiwa hayupo.
Tutaona baadaye sababu zinazozingatiwa kwenye kumkabidhi mtu mkoba.

Familia isipofanya Makabidhiano tena ya hadharani kamwe haiwezi kuwa na umoja na heshima miongoni mwa ndugu.

Mtu anapokabidhiwa Familia labda ni Kaka au Dada mkubwa(kwa familia zenye wanawake watupu) mbele ya kila mmoja; akitokea mmoja akakaidi sauti ya mkabidhiwa(Mteule) maana yake amekaidi mpaka sauti ya Baba.

Yaani Baba yako akiikabidhi familia kwa ndugu yako kisha Baba yako akafa; basi jua kuwa Baba yako anaishi kupitia ndugu yako aliyekabidhiwa, usipotii sauti yake na kumdharau basi moja kwa moja umemdharau Baba yako, matokeo yake ni laana.

Lengo kuu la Makabidhiano ni usalama na kutimiza Malengo na ndoto zilizokwisha kuwekwa. Maboresho chanya hayazuiliwi
Familia isiyokuwa na mkabidhiwa huingia katika hatari nyingi mno.

Kama vile hatari za kimaadili na kuanguka kwa familia au ukoo huo.

Mama na Baba wakishafariki na asiwepo ndugu aliyekabidhiwa watoto ni rahisi kwa familia kuharibika kimaadili
Watoto watafanya mabaya pasipo kuogopa yeyote wala pasipo kuona aibu kwani Hakuna aliyepewa mamlaka ya kuwaongoza.
Kwa zamani mtu kabla Hajafa ilikuwa lazima aite watoto wake wote kisha awape Wosia na mashauri ya muhimu baadaye Humchagua mtu mmoja ambaye atampa mamlaka yote kuwaongoza watoto wake. Ikiwemo mamlaka ya kubariki na kulaani ambayo ni mamlaka ya juu kabisa aliyonayo mzazi.

Hivyo watoto humuheshimu mtu huyo baada ya Baba au Mama yao kufa.
Watoto wa siku hizi wamekosa adabu kwa sababu wengi wao hawajakabidhiwa kwa mtu. Ukimuonya atakuambia kwani wewe ni nani kwake hapo utabaki umeaibika.

Niishie hapa japo yapo mengi yakusema

2. MAKABIDHIANO YA KIROHO
Binadamu yeyote huongozwa na Roho. Kwenye roho zipo falme za kiroho ambazo huitwa miungu; ingawaje Mungu ni mmoja lakini haiondoi ukweli kuwa ipo miungu mingi mingine kama sivyo asingalituambia kuwa tusiabudu miungu mingine ila yeye pekee.

Je roho na maisha yako yamekabidhiwa kwa Mungu yupi?
Wazazi na wazee wetu hufanya mengi wawapo Kwenye maisha ya ujana ili kufanikiwa na kujikimu kwenye maisha. Wapo ambao walifanya maagano na miungu na kusalimisha vizazi vyao kwa miungu hiyo.
Lazima ujue wewe maisha yako yalikabidhiwa kwa mungu yupi, waulize wazazi wako kama wapo watakujibu; muhimu waulize kwa hekima na nidhamu. Kama wazazi Hawapo basi uliza wazee wa ukoo
Maisha yako yanaendeshwa na miungu au Mungu kati yapo, hivyo unavyohangaika na maisha lazima ujue hilo.
Lazima awepo mtu kwenye ukoo aliyekabidhiwa kuendesha mambo ya kiroho.
Mzazi makini kabla hajaondoka Dunia lazima awaambie watoto wake mahali sahihi Pakuabudu na kiongozi wa dini atakayewasimamia watoto wake
Yesu amchagua Petro na kimkabidhi wanafunzi wake. Alimwambia; Chunga Kondoo zangu
Yesu anajua umuhimu kwa kundi kuwa Na kiongozi wa kuwaongoza.

3. MAKABIDHIANO YA KIUCHUMI
Haya ni Makabidhiano yanayohusu Mali, pesa na urithi mwingine wowote kama miradi
Familia bora na koo makini hukabidhi Mali kulingana na akili, mtazamo, umri na jinsia ya watoto.

Mkabidhi mtoto mali anayostahili kukabidhiwa, mpe mali anayoweza kuiongoza.

Waisrael walipokuwa wakiingia Kanaani walikabidhiwa Mali na ardhi kulingana na makabila yao kimuonekano, kimaumbile na kiakili. Makabila yenye nguvu walikabidhiwa ardhi ya mipakani. Hata hivyo Kabila la Lawi halikupewa Mali ya ardhi isipokuwa urithi wa kiroho kwa kupewa Zaka na Sadaka.
4. MAKABIDHIANO YA KISIASA
Haya huhusu utawala na uongozi kwa ujumla wake. Iwe uongozi wa kiserikali, kijamii, Kimila, kifamilia, kidini nk
Makabidhiano haya ni muhimu kwani huhusu usalama wa baadaye.

Mfano wa Makabidhiano ya Kisiasa
Musa Vs Joshua
Daudi Vs Suleiman
Eliza Vs Elisha Nk
Hata hivyo Makabidhiano huweza pia kufanywa kwa njia ya demokrasia kwa zama hizi

5. MAKABIDHIANO YA KIMAARIFA
Haya ni Makabidhiano ya Elimu, ujuzi, telnolojia, ufahamu, hekima, falsafa nk
Afrika tunatatizo kubwa katika kipengele hiki.
Wapo wazee hufariki wakiwa na ujuzi au maarifa fulani.
Wapo wenye maarifa ya kutengeneza zana mbalimbali, wapo wenye kujua mitishamba ya dawa, wapo waliokufa wakiwa na uwezo usiosemeka

Mfano wa makabidhiano ya maarifa
Aristotle Vs Plato
Plato Vs Socrate kama sijachanganya
Yesu Vs Petro
Elia Vs Elisha
Hao walihamisha Elimu zao kwa wanafunzi wao

Kwa leo tuishie hapa.
Ulikuwa nami

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Morogoro
 
Back
Top Bottom