~ Majuto - Ufalme wa Tandu ~ A novel...


Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,023
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,023 280
......Rais hakupoteza muda, alilakiwa hapo na Kanali Khaki ambaye alimpa maelezo mafupi na kumuelekeza ambako miili ya Marehemu ilikuwa bado imelazwa ikiwa imefunikwa na kanga na shuka. Alimwambia pia kuwa wamefanikiwa kupata watu wengine wanne wakiwa bado hai, na matumaini ya kuwapata wengine bado yapo endapo msaada wa Afrika ya Kusini utafika mapema. Rais alisikiliza kwa makini huku akitingisha kichwa chake. Hakutaka kuingilia shughuli za uokoaji, na aliamua kwenda chini ya mwembe ambako ndiko kulikuwa na makao makuu ya shughuli hizo. Akiwa njiani kuvuka barabara kwenda kwenye eneo hilo la chini ya mwembe, makumi ya watu walimzunguka huku wakitaka kupeana naye mkono wa pole. Macho yake yalikuwa yamevimba na uso wake umebadilika rangi kwa majonzi na machozi. Hakusalimiana na wengi, na alipofika chini ya ule mwembe, aliwaambia wasaidizi wake kuwa angependa kuzungumza na wananchi kwa kifupi. Mmoja wa wasaidizi wake ambaye alikuwa ni mmoja wa watoto wa kigogo wa chama alizungumza kwenye simu ya upepo na kumtaka dereva mmoja wa gari lenye spika alilete eneo hilo. Dakika kumi baadaye gari aina ya Toyota lenye spika nne zilizochomewa juu zikiangalia pande nne za ulimwengu liliegeshwa. Rais Kikwete alifumba macho kwa dakika chache huku akijiandaa kuzungumza na wananchi. Wakati anajiandaa upande wa pili wa barabara shughuli za utafutaji na uokoaji ziliendelea. Alipofumbua macho yake, alielekea lilikoegeshwa gari. Watu walizunguka karibu huku kamera, vinasa sauti vya vyombo vya habari vikielekezwa aliko. Watu walivuta pumzi kumsubiri Rais wao azungumze......


(Hiyo ni sehemu tu ya kisa kinachoendelea cha kusisimua kinachohusu hali halisi ya ulimwengu, usaliti, mapenzi, siasa, na ulafi... kinaendelea kila wiki katika Gumzo... kama hujasoma.. hujui umepitwa na nini..! Hadi sasa kisa hicho kinangojewa kila wiki na mamia ya Watanzania kila kona duniani!)

Anza kusoma kisa hicho hapa:

http://www.phpbbcity.com/forum/viewtopic.php?t=277&start=0&mforum=baraza
 
C

Comrade Mfate

Member
Joined
Sep 26, 2006
Messages
9
Likes
0
Points
0
C

Comrade Mfate

Member
Joined Sep 26, 2006
9 0 0
Hongera mtunzi ukumaliza sema nami niteleta bonge la stori
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,023
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,023 280
Haya mazee
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,872
Likes
8,023
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,872 8,023 280
Happiness.. nini tatizo... kisa kitaendelea leo...usikose
 
C

chige

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
8,032
Likes
15,199
Points
280
C

chige

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
8,032 15,199 280
Nakumbuka siku alipotoa machapisho kuhusu Meremeta! Nkumbuka jinsi kulivyokuwa na demand ya kutaka lile chapisho ingawaje mtu ulitakiwa uchangie kidogo!!!

Sijui leo hii akitoa chapisho ni wangapi watalikimbilia kama ilivyokuwa zama zile!!
 

Forum statistics

Threads 1,235,528
Members 474,641
Posts 29,225,752