~ Majuto - Ufalme wa Tandu ~ A novel...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
......Rais hakupoteza muda, alilakiwa hapo na Kanali Khaki ambaye alimpa maelezo mafupi na kumuelekeza ambako miili ya Marehemu ilikuwa bado imelazwa ikiwa imefunikwa na kanga na shuka. Alimwambia pia kuwa wamefanikiwa kupata watu wengine wanne wakiwa bado hai, na matumaini ya kuwapata wengine bado yapo endapo msaada wa Afrika ya Kusini utafika mapema. Rais alisikiliza kwa makini huku akitingisha kichwa chake. Hakutaka kuingilia shughuli za uokoaji, na aliamua kwenda chini ya mwembe ambako ndiko kulikuwa na makao makuu ya shughuli hizo. Akiwa njiani kuvuka barabara kwenda kwenye eneo hilo la chini ya mwembe, makumi ya watu walimzunguka huku wakitaka kupeana naye mkono wa pole. Macho yake yalikuwa yamevimba na uso wake umebadilika rangi kwa majonzi na machozi. Hakusalimiana na wengi, na alipofika chini ya ule mwembe, aliwaambia wasaidizi wake kuwa angependa kuzungumza na wananchi kwa kifupi. Mmoja wa wasaidizi wake ambaye alikuwa ni mmoja wa watoto wa kigogo wa chama alizungumza kwenye simu ya upepo na kumtaka dereva mmoja wa gari lenye spika alilete eneo hilo. Dakika kumi baadaye gari aina ya Toyota lenye spika nne zilizochomewa juu zikiangalia pande nne za ulimwengu liliegeshwa. Rais Kikwete alifumba macho kwa dakika chache huku akijiandaa kuzungumza na wananchi. Wakati anajiandaa upande wa pili wa barabara shughuli za utafutaji na uokoaji ziliendelea. Alipofumbua macho yake, alielekea lilikoegeshwa gari. Watu walizunguka karibu huku kamera, vinasa sauti vya vyombo vya habari vikielekezwa aliko. Watu walivuta pumzi kumsubiri Rais wao azungumze......


(Hiyo ni sehemu tu ya kisa kinachoendelea cha kusisimua kinachohusu hali halisi ya ulimwengu, usaliti, mapenzi, siasa, na ulafi... kinaendelea kila wiki katika Gumzo... kama hujasoma.. hujui umepitwa na nini..! Hadi sasa kisa hicho kinangojewa kila wiki na mamia ya Watanzania kila kona duniani!)

Anza kusoma kisa hicho hapa:

http://www.phpbbcity.com/forum/viewtopic.php?t=277&start=0&mforum=baraza
 
Back
Top Bottom