Majuto: Sitatongoza mtandaoni tena

Pole sana mkuu, sio JF tuu hata Facebook hukooo. Hahaha umenikumbusha mbali sana. Tulikua na demu mmoja ofisini, dah kituko, kajichubua balaa, shapeless, pasi ya umeme. Ila sasa picha zilizopo FB aah hatari lazima unateee, pozi za kufa mtu, anatumia Camera360 tena. Ukiongea naye kwenye simu ndio anakumaliza kabisa daaahh!!! Na ukicheki profile ana friends karibia 500 na wengi ni vidume. Naamini wengi aliwaumiza maana alikua dada poa flani pia.


Tuache hizi mambo aloo
 
Hahahaaa. Itafika tu Mtani ila kuisogeza karibu ngoja nimuombe ruhusa Sesten Zakazaka kama akikubali Mtani basi tunapanga tu. 😜😜😜😜😜

😂😂😂😂😂 lol.
Utaleta maombi rasmi yakiwa na maelezo yakina halafu itawekwa mizani kuangalia uzito wa sababu, viwango vya usalama na kama suala la kutekana sio tu halitakuwepo wala kwenye mipango na fikra halijapangwa....hii ni pamoja na kuzingatia hutaruhusiwa kutembea peke yako kwenda kwenye huo mualiko aua hata gym😉 Hajar
 
Wanaume wa mikoani ndio maana dada zenu wanaomba nauli ya kuja Dar sababu boda boda hawazijui wanaziona kwenye TV
 
Ndo hivyo mkuu , jina, mada zake pamoja na avatar vilinifanya ni usiku mzima nisilale nikiingonjea siku ya kuonana na mrembo matata, ila niliyekutana nae sina budi kutubu na kumrudia mola wangu au nikomae na wa huku uswazi kwetu.
Mkali ungeuchuna tu, wala ilikuwa haina haja ya kuja kumsema hapa maana maji ukiyavulia nguo lazima uyaoge. Lakini kubwa zaidi hata ukikuta kitu ambacho ni tofauti na mategemeo yako usikimbilie kumletea shombo humu ndani, huwa haipendezi. Kuna kipindi ukija kukua hutawaangalia watu kwa sura zao wala maumbile na utakuja fahamu kwanini nasema hivi....
 
Hahahaaaaa. Nimejikuta nakuelewa tu Sesten nitafanya hivyo.

Ila pia nimecheka hivi mie na gym wapi na wapi jamaani. 🙈🙈🙈🙈
 
Hizi ndio thread pendwa huku MMU na chitchat. Siku moja tu unaweza kukuta ina pages hata 50! Ukisoma maandishi utaona watu wanajidai kumponda mleta mada kwanini kaja kusimulia huku au kwanini anakosoa uumbaji wa Mungu, ila ukisoma katikati ya mistari utaona wengi wanainjoi sana the whole drama na wanatamani huyo 'aliedhalilishwa' hapa atajwe wamjue sasa sijui wakishamjua inasaidia nini.
 
Hahahahaaaa, ulitegemeaje mkuu… yaani unaachaje kumpenda uliyemuona kwa macho mpaka uweke nguvu nyingi kwa mtu usiyemjua…. Wabongo ni waigizaji kwa kila jambo, teteteteeeh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…