Majuto: Mchepuko anataka kunipeleka kwa Makonda

Majuto: Mchepuko anataka kunipeleka kwa Makonda

SACO

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2011
Posts
2,877
Reaction score
3,788
Ilikuwa kama utani mwaka 2013 tukiwa kwenye daladala za Kimara - Posta. Nilimtongoza akanitunuku na mimba ya mtoto wa kike ikapatika na akajifungua salama salmini.

Kifupi nimekuwa nikitoa huduma zote kwa huyu mchepuko tokea akiwa mjamzito na nahudumia kwa kutoa kama laki mbili na nusu kila mwezi, lakini haridhiki kabisa anasema fedha haitoshi sababu mtoto anaugua mara kwa mara na mimi nilishamwambia siwezi toa zaidi ya hapo coz hata wife hamjui na nina watoto wengine kwa wife.

Tatizo ni tokea Makonda atangaze kuwa wanawake waliotelekezewa watoto wakatoe taarifa, aisee the whole week am at high risk... nalala kwa shida ni mawazo tu hadi wife kanistukia.. Ni ananitishia kila siku simu haziishi kuwa jumatatu atakuwa wa kwanza kunireport kwa Makonda, na mzaramo huyu kichwa chake antena haipo sawa najua hatanii ataenda tu. Nimejaribu kumtumia rafiki yake amshauri imeshindika.

Jana jioni nimemtumia laki moja, asubuhi hii kanitumia sms... "Unajua kulea wewe? Umenitumia vihela vya mboga hivi huoni wanaume wenzio wanavyotoa? Unajua Mobetto anapewa sh ngapi kwa siku? Kwa taarifa yako hii ni nauli ya tax kesho kwenda kwa Makonda"...

Wakuu hapa nakaribia kuwa chizi sometime najikuta naongea alone. Ushauri tafadhali.
 
Ilikuwa kama utani mwaka 2013 tukiwa kwenye daladala za Kimara _ Posta. Nilimtongoza akanitunuku na mimba ya mtoto wa kike ikapatika na akajifungua salama salmini.
Kifupi nimekuwa nikitoa huduma zote kwa huyu mchepuko tokea akiwa mjamzito na nahudumia kwa kutoa kama laki mbili na nusu kila mwezi, lakini haridhiki kabisa anasema fedha haitoshi sababu mtoto anaugua mara kwa mara na mimi nilishamwambia siwezi toa zaidi ya hapo coz hata wife hamjui na nina watoto wengine kwa wife.

Tatizo ni tokea Makonda atangaze kuwa wanawake waliotelekezewa watoto wakatoe taarifa, aisee the whole week am at high risk... nalala kwa shida ni mawazo tu hadi wife kanistukia.. Ni ananitishia kila siku simu haziishi kuwa jumatatu atakuwa wa kwanza kunireport kwa Makonda, na mzaramo huyu kichwa chake artena haipo sawa najua hatanii ataenda tu, nimejaribu kumtumia rafiki yake amshauri imeshindika. Jana jioni nimemtumia laki moja, asubuhi hii kanitumia sms... "unajua kulea wewe? Umenitumia vihela vya mboga hivi huoni wanaume wenzio wanavyotoa? Unajua Mobeto anapewa sh ngapi kwa siku? Kwa taarifa yako hii ni nauli ya tax kesho kwenda kwa Makonda"... wakuu hapa nakaribia kuwa chizi sometime najikuta naongea alone... Ushauri tafadhali..

Huwezi kuishi na huu utumwa, Kama uoga wako ni kwa Makonda, kwa laki 2 hakuna anachoweza lalamika zaidi, that is enough money. Usikae kwenye huu utumwa, mwambie afanye analotaka basi! Hili nalo litapita kabisa, usiwe mtumwa bila sababu.
 
Laki 2 kwa mwezi.haitoshi?? Au umekuja kutoa kiki kwani akienda utakufa? Kama huna uwezo wa kumpa mil.10 kwa mwezi ufanyaje uibe?? Hata akienda Kuna mahakama zitaangalia kipato chako vs uhalisia...

Nchi hii ina sheria zake haya matamko yatarudi kisheria
 
Mwanangu,acha kuogopa...mwambie nenda kwa Bashite na usipoenda nitakuja kukupiga kwa kunitishia
Lkn tatzo jingine ninaloliona hapo ni kuwa 'huyo mwanamke ni m2 wa viwanja na starehe sana so,hata ukimpa fedha nyingi haziwezi kumtosha
Fanya maamuzi kama mwanaume!
 
Huwezi kuishi na huu utumwa, Kama uoga wako ni kwa Makonda, kwa laki 2 hakuna anachoweza lalamika zaidi, that is enough money. Usikae kwenye huu utumwa, mwambie afanye analotaka basi! Hili nalo litapita kabisa, usiwe mtumwa bila sababu.
Hii issue wife ilikuwa bado kumwambia.. kwani inahitaji utulivu vinginevyo naweza haribu kote
 
Chukua mtoto wewe, hawez kukupeleka hilo ni bit tu
 
Back
Top Bottom