Majuto afunguka tangazo la airtel

Majuto afunguka tangazo la airtel

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
951

​



[FONT=Arial, Verdana]KUTOKANA na malalamiko ya baadhi ya mashabiki na hali ya kutofahamu juu ya sababu inayosababisha kuendelea kuonyeshwa kwa tangazo la kampuni ya simu ya mkononi Airtel lilikouwa limerekodiwa na marehemu Sharomilionea, King Majuto afafanua sababu zinazosababisha tangazo hilo kuendelea kuwa hewani kwa kipindi hiki[/FONT]

[FONT=Arial, Verdana]Akizungumza kwa njia ya simu Amri Athumani a.k.a King Majuto alisema kuwa mkataba bado unaendelea kuwepo na ndio maana bado tangazo hilo linaendelea kuchezwa katika vyombo vya habari[/FONT]

[FONT=Arial, Verdana]Alisema kuwa mbali na mkataba huo pia mama yake mzazi na marehemu Sharomilionea ameomba tangazo hilo liendelee kupigwa ili kwa kipindi cha mwezi mmoja ili aweze kupata fedha za kujikimu kimaisha kwa kipindi hiki ambacho mwanaye ndiye alikuwa msaada mkubwa kwake[/FONT]

[FONT=Arial, Verdana]"Tangazo hilo linapigwa kwa makubaliano ya mama yake mzazi ili aweze kupata fedha za kujikwimu , na ameruhusu lipigwe kwa kipindi cha mwezi mmoja na ndio maana unaona linachezwa hilo tangazo katika vyombo vya habari" alisema King Majuto[/FONT]

[FONT=Arial, Verdana]Mbali na hayo alipouulizwa mwanasheria wa kujitegemea Mwemezi Makumba juu ya uhalali wa kuendelea kulicheza tangazo hilo yeye alieleza kuwa,kama taratibu zote zilifuatwa na kukamilika katika mkataba huo ni halali kuendelea kucheza tangazo hilo huku mafao pamoja na stahiki zote za marehemu zikilipwa kwa mrithi wake[/FONT]

[FONT=Arial, Verdana]Alisema kuwa kulingana na taratibu za mkataba kukamilika mtu anapokufa na mkataba haufi, bali unaendelea kwa kushirikisha warithi wa marehemu[/FONT]

[FONT=Arial, Verdana]Aliongezea kuwa mkataba unaweza kufa kama taratibu za mkataba huyo haujakamilika kisheria

[/FONT]
http://pro-24.blogspot.com/2012/12/majuto-afunguka-tangazo-la-airtel.html[FONT=Arial, Verdana]

[/FONT]
 
Sioni tatizo, ngoja tuendelee kumuona kijana mwenzetu Sharo-milionea japo hatukonaye.
 
Sasa hakuna utata tena maana ufafanuzi wa King Majuto umeeleweka.
 
Nami nimeelewa sasa maana la kanumba liliachwa kuchezwa fasta
 
Ahaaaaaa... Kumbeeee!! Mtanzania akielewa jambo lililokuwa linamsumbua lazima alie Kama Ndama
 
sioni tatizo la tangazo kuendelea kuwepo silioni... tatizo wabongo ni waoga wavifo na mambo yanayohusu marehemu sana......
 
Yaani tunathamini fedha kuliko marehemu!! Hizi fedha mbona hatuendi nazo? Kwani Sharo aliondoka nazo? Mie naona si haki kuendelea kulionyesha irrespective of any reason!!!

​



KUTOKANA na malalamiko ya baadhi ya mashabiki na hali ya kutofahamu juu ya sababu inayosababisha kuendelea kuonyeshwa kwa tangazo la kampuni ya simu ya mkononi Airtel lilikouwa limerekodiwa na marehemu Sharomilionea, King Majuto afafanua sababu zinazosababisha tangazo hilo kuendelea kuwa hewani kwa kipindi hiki

Akizungumza kwa njia ya simu Amri Athumani a.k.a King Majuto alisema kuwa mkataba bado unaendelea kuwepo na ndio maana bado tangazo hilo linaendelea kuchezwa katika vyombo vya habari

Alisema kuwa mbali na mkataba huo pia mama yake mzazi na marehemu Sharomilionea ameomba tangazo hilo liendelee kupigwa ili kwa kipindi cha mwezi mmoja ili aweze kupata fedha za kujikimu kimaisha kwa kipindi hiki ambacho mwanaye ndiye alikuwa msaada mkubwa kwake

"Tangazo hilo linapigwa kwa makubaliano ya mama yake mzazi ili aweze kupata fedha za kujikwimu , na ameruhusu lipigwe kwa kipindi cha mwezi mmoja na ndio maana unaona linachezwa hilo tangazo katika vyombo vya habari" alisema King Majuto

Mbali na hayo alipouulizwa mwanasheria wa kujitegemea Mwemezi Makumba juu ya uhalali wa kuendelea kulicheza tangazo hilo yeye alieleza kuwa,kama taratibu zote zilifuatwa na kukamilika katika mkataba huo ni halali kuendelea kucheza tangazo hilo huku mafao pamoja na stahiki zote za marehemu zikilipwa kwa mrithi wake

Alisema kuwa kulingana na taratibu za mkataba kukamilika mtu anapokufa na mkataba haufi, bali unaendelea kwa kushirikisha warithi wa marehemu

Aliongezea kuwa mkataba unaweza kufa kama taratibu za mkataba huyo haujakamilika kisheria

http://pro-24.blogspot.com/2012/12/majuto-afunguka-tangazo-la-airtel.html

 
kwa ulimwengu wa sasa siyo ajabu, kama sikosei mwanamuziki alieingiza mapato makubwa usa mwaka juzi na jana alikuwa ni mjj baada ya kifo chake.tatizo sijui kama sharo aliandika will ie mirathi mapema!!!!siunajua wabongo bwana kwa kuchakachua
 
Yaani tunathamini fedha kuliko marehemu!! Hizi fedha mbona hatuendi nazo? Kwani Sharo aliondoka nazo? Mie naona si haki kuendelea kulionyesha irrespective of any reason!!!

Sasa Mpelekee Mama yake Marehemu hela ya kula ili ulistopishe tangazo.
 
Acheni umasai. Kwani kuna shida gani kuendelea kuonyesha matangazo ya marehemu? Mbona movie za kanumba tunaangalia na miziki ya kina bob marley tunaisikiliza? Acheni uswahili, wa kulalama angekuwa mamake mzazi. Huu unafiki wa kujifanya tunaheshimu na kuthamini watu baada ya kufa hata haupendezi!
 
Back
Top Bottom