Majukumu yanazidi kipato, nahitaji kazi jamani kuongeza kipato

Sea Beast

JF-Expert Member
Aug 5, 2022
1,888
4,054
Habari
Natafuta kazi yeyote ambayo nitapata kipato japo hata 10,000 kwasiku maana majukumu yamenizidi wazazi hawapo vizuri kiuchumi na mzazi wa kiume(Baba wa Familia) alifariki inanilazimu kusaidia Home kidogo masuala ya kula, shule madogo na majukumu ya hapa na pale

Kipato nachopata kidogo sana hata kwa kukutumia mimi mwenyewe na Sina mshahara ninalipwa kwa kamisheni at least mwaka jana tulikuwa tunapata kamisheni mzuri kidogo ambayo unafanya mambo yako na nyumbani unasaidia ila sasahivi kwakeli tunapata pesa ya usafiri tu na kujiunga bando kichwa kinauma nahitaji kukamilisha malengo yangu na pia nyumbani familia Hali duni sisi ndio watoto wakubwa Bimkubwa hali ngumu anatuangalia tusaidiesaidie familia kichwa mpaka kinauma.

Naomba mtu yeyote anayeweza kunipa kazi au kuniunganisha na Kazi sehemu ya at least kupata 10,000 kwasiku au 300,000 kwa Mwezi maana sasahivi changamoto kipato aisee wanaotokea familia zetu wanajua hii changamoto.

Ujuzi na Skills nilizo nazo

1)Teaching Skills

Ninaweza kufundisha secondary masomo Kama Geography na History, pia program yeyote inayohusu kufundisha.

2) Computer Basics i.e Ms Word
Ninauwezo wa kufundishika program/system zozote za taasisi au Kampuni na nikaweza kufanya kazi katika ofisi husika.

Naweza kufanya kazi yeyote nipo DSM

_________________
Ningependa uzi huu uwafikie wengi nitakuwa nafanya Door to Door (Personal) kwa kutag watu randomly ili kuonesha umuhimu wa mtu na kuonesha msisitizo wa hitaji na umuhimu
 
Jiajiri kwenye betting!
Ukibet Full Time baada ya dakika 90 unapata chako!

Ukibeti magoli hata yakipatikana ndani ya dakika 10 unapata chako.

Hatusubiri mshahara mwisho wa mwezi wala mwisho wa wiki, ni ndani ya dakika 90 unakuwa umeshajua hatima yako.
 
Sio mcuatiliaji wa mpila hivyo itakuwa ngumu kwangu ku-master game maana nawaona hata wanaozijua timu na mashabiki ndakindaki wanapoteza Sana je Mimi.
 
Nimezaliwa na kukulia DSM Mzee hatuna mashamba
Mzee ishu ya uchumi ni janga la wengi na Hakuna matumaini,pana jamaa yangu watoto wake wanalamba hadi kisu na kutafuna kitunguu njaa sometimes nikipata elf 5 au 10 nampa angalau wasife njaa.
Mwenye nyumba anataka kodi watoto wanalia njaa.
Hali tete,pana mwingine akila leo kesho anapiga desh hadi kesho kutwa ana vyeti procurement, transport and logistics,ni mtaalamu wa clearing and forward hana mtaji hana Kazi kaandika barua zaidi ya elf 3.
Nchi imestaki hii.
 
Habari
Natafuta kazi yeyote ambayo nitapata kipato japo hata 10,000 kwasiku maana majukumu yamenizidi wazazi hawapo vizuri kiuchumi na mzazi wa kiume(Baba wa Familia) alifariki inanilazimu kusaidia Home kidogo masuala ya kula, shule madogo na majukumu ya hapa na pale

Kipato nachopata kidogo sana hata kwa kukutumia mimi mwenyewe na Sina mshahara ninalipwa kwa kamisheni at least mwaka jana tulikuwa tunapata kamisheni mzuri kidogo ambayo unafanya mambo yako na nyumbani unasaidia ila sasahivi kwakeli tunapata pesa ya usafiri tu na kujiunga bando kichwa kinauma nahitaji kukamilisha malengo yangu na pia nyumbani familia Hali duni sisi ndio watoto wakubwa Bimkubwa hali ngumu anatuangalia tusaidiesaidie familia kichwa mpaka kinauma.

Naomba mtu yeyote anayeweza kunipa kazi au kuniunganisha na Kazi sehemu ya at least kupata 10,000 kwasiku au 300,000 kwa Mwezi maana sasahivi changamoto kipato aisee wanaotokea familia zetu wanajua hii changamoto.

Ujuzi na Skills nilizo nazo

1)Teaching Skills

Ninaweza kufundisha secondary masomo Kama Geography na History, pia program yeyote inayohusu kufundisha.

2) Computer Basics i.e Ms Word
Ninauwezo wa kufundishika program/system zozote za taasisi au Kampuni na nikaweza kufanya kazi katika ofisi husika.

Naweza kufanya kazi yeyote nipo DSM

_________________
Ningependa uzi huu uwafikie wengi nitakuwa nafanya Door to Door (Personal) kwa kutag watu randomly ili kuonesha umuhimu wa mtu na kuonesha msisitizo wa hitaji na umuhimu
its so sad champ, nikisoma maelezo yako utafikiri tumewahi onana kwenye harakati za kutafuta kazi za viwandani kwa mhindi. jah bless man mtaa umetuzimia data kabisa
 
Mzee ishu ya uchumi ni janga la wengi na Hakuna matumaini,pana jamaa yangu watoto wake wanalamba hadi kisu na kutafuna kitunguu njaa sometimes nikipata elf 5 au 10 nampa angalau wasife njaa.
Mwenye nyumba anataka kodi watoto wanalia njaa.
Hali tete,pana mwingine akila leo kesho anapiga desh hadi kesho kutwa ana vyeti procurement, transport and logistics,ni mtaalamu wa clearing and forward hana mtaji hana Kazi kaandika barua zaidi ya elf 3.
Nchi imestaki hii.
Niliiona hii stori mzee ni changamoto aise, ila kwa jamaa hapo wa logistics amejaribu kwenye Kampuni ndogo za usafirishaji maana naona huku town kwenye jengo zima zimejazana Kampuni za logistics mpaka nawaza kuwa na hii carrier
 
Je una umri gani?unaweza kufanya kazi za mikono eg usafi wa nyumba na kuangalia garden full time na kulala hapo hapo?malipo ni kwa wiki
 
Mzee ishu ya uchumi ni janga la wengi na Hakuna matumaini,pana jamaa yangu watoto wake wanalamba hadi kisu na kutafuna kitunguu njaa sometimes nikipata elf 5 au 10 nampa angalau wasife njaa.
Mwenye nyumba anataka kodi watoto wanalia njaa.
Hali tete,pana mwingine akila leo kesho anapiga desh hadi kesho kutwa ana vyeti procurement, transport and logistics,ni mtaalamu wa clearing and forward hana mtaji hana Kazi kaandika barua zaidi ya elf 3.
Nchi imestaki hii.
Huyo jamaa wa clearing ameshawahi kufanya kazi hizo(uzoefu)na yuko mkoa gani??
 
Mungu atusimamie makabwela...ki ukweli wengi tunapitia changamoto hasa...imagine msosi tu shida,hapo ndio unajua ile kaul ya kua uyaone haikua masikhara!tupambane tu ndg zangu huenda siku moja tutafanikiwa angalau kumudu the basic needs
 
Huyo jamaa wa clearing ameshawahi kufanya kazi hizo(uzoefu)na yuko mkoa gani??
Kama una nafasi ya kumsaidia jamaa kupata kazi fanya hivyo hata mimi napitia kipindi kigumu sana cha kushukuru hakuna anaenitegemea so maisha nayamudu nikipata nikikosa fresh tu vilevile sina madeni
 
Back
Top Bottom