Majukumu yamenielemea

Tony Yeyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Posts
733
Reaction score
568
Habar Zenu

Mwenzunu nimejikuta kwenye wimbi la mawazo Baada ya kuelemewa na majukumu. Baada ya Kupata kibarua nimejikuta napokea simu nyingi kuhusu Matatizo ya kifamilia

Nimejitahidi sana kutatua Matatizo Kwa kadri ya uwezo wangu lakini mambo yanazidi kuwa magumu.

Ukiachana na kuhudumia familia Yangu lakini shida za Ndugu zimekuwa haziishi

Zinapokaribia tarehe za mwisho wa mwezi najikuta sina raha Kabisa maana napigiwa simu nyingi za shida na kuombwa pesa tu

Naombeni mbinu ya kukabiliana na changamoto hizi
 
Ukiwaendekeza ndugu hufiki kokote na mwisho wa siku wao ndio wanakuteta kwamba una kazi ila hauna maendeleo,katika mshahara tenga kiasi fulani cha kusaidia ndugu wa karibu au muhimu zaidi mfano wadogo zako wa damu ndio uwape kipaumbele au wazazi,shida zikizidi kiasi waambie hauna,kiasi kinachobaki fanya maendeleo yako binafsi.kinyume cha hapo utafanyia kazi shida za watu na hilo sio lengo maana mwisho wa siku utakuwa hujafanya kitu ktk maisha yako
 
Wewe ndio una suluhisho sahihi. Hapa unaweza shauriwa vibaya ukapata laana kwa kushindwa kusimama katika yale unayopaswa kutenda.

Kuna jamaa alifanikiwa akajenga nyumba kubwa sana mama yake akamuhusia kuishi na nduguze mama alipokufa jamaa akauza ile nyumba na kusambaza ndugu zake ili wajitegemee. Wengi waliangaika sana baada ya kusambazwa ila jamaa naye ali suffer kinoma maana hata ile nyumba aliiuza tena mwishowe wanaye wote walikufa pia sasa kabakia na kijana mmoja naye choka mbaya sana.

Hivyo suala la ndugu ni la kuangalia sana.
 
Kuna mkulungwa mmoja kaandika Uzi mzuri Sana kuhusiana na waliopata kazi na nini wanatakiwa wafanye,ametoa mawazo mazuri Sana,ikiwemo vile vile kuepuka mikopo ktk hizi taasisi za kifedha ndogo ndogo hizi,nakushauri utafute

Kutoka kwangu nikwambie hivi,Saidia ndugu kutokana na uwezo wako,usipitilize utapata presha, swali la msingi kabla ya wewe kupata kazi waliendesha vipi Maisha?

Usihofu maneno Yao,Saidia pale inapowezekana na inaposhindikana sema pia, tumia lugha nzuri Tu na kuwapiga sound,unaweza kujitoa Sana kwao ukashinda kufanya mambo yako ya msingi,na ndio hao hao baadae wanakuja kukusema tena '' alikuwa na kazi Yule lkn kashindwa kufanya mambo ya maana'' lkn wamesahau kuwa ulitumia hela nyingi kuwasaidia wao.
 
Wabongo shida sana nilipokua naenda kuishi majuu nilisikia tu huyu tunampa mwaka anarudi na ni miaka mingi enzi hizo kwenda majuu unefight sana..

Kisa nisichokisahau ni miaka 4 mbele niliporudi likizo kusalimia nikakutana na mama mmoja cha kwanza ilikua ni salam cha pili ikawa kuomba pesa nilimjibu tu kuwa sina pesa.

Nilikuja kuambiwa na bi mkubwa kua wimbo ukawa ninaringa nimeenda nje sasa nishabeba tamaduni za nje.

Hii iliendelea hata kwenyr issue zisizo na maana yaani watu wanafanya kisherehe kidogo tu hata siwajui wanataka niwape pesa.

Hadi wa leo kanuni yangu ni natoa hela nikiamua na nitachangia msiba na sio harusi.

NB:Ni mwiko mimi kuniweka kwenye group la mambo ya harusi na wanalijua hili
 

Umasikini wa ukooo, ndugu, familia na jamaa hautaisha kwa kuwapa hela. Bahati mbaya sana na wewe umasikini unakuhusu in the next few years if you do not change course immediately. I mean immediately!

Huwezi kumsaidia mtu kuinuka huku umekaa. Lazima usimame vizuri ukiwa na balance la sivyo utaanguka. Ninachomaanisha ni kwamba, matatizo hayo yalikuwepo hata kabla ya wewe kupata kibarua na yataendelea kuwepo hata ukijitahidi kiasi gani.

Focus kwenye kuondoa umasikini wa familia yako kwanza. Watunze wazazi wako kama bado wapo. Wengine ni watu baki. Jiimarishe kiuchumi kwa kuwekeza kwenye vitegauchumi vya muda mrefu.

Ukiendekeza matatizo ya ndugu, amini nakuambia, umasikini wa milele unakuhusu.

Bahati nzuri utakapofilisika ndo utagundua walikuwa na malengo maalumu. Hao hao ndo watashangilia umasikini wako, tena watakutolea mfano ulivyokuwa mjinga.
 

Asante Mkuu
 
Waambie wakuache ujipange kwanza,usipokua makini utaishia kusaidia watu tu.

Jiulize,Ulipokua hauna kazi nani alikua anawasaidia?

Be selfish at sometimes
 
Kabla ya wewe kupata hicho kibarua, hayo matatizo yalikuwa wapi? Au ni nani alikuwa anayatatua?
 
Nadhani wengi wa members wa hapa JF wenye kazi wanakutana na matatizo kama haya ikiwemo mimi. Tofauti yetu na wewe ni kuwa sisi hatusaidii watu kupita uwezo wetu na ndugu zetu wanapoomba msaada tunawaambia bila kupepesa macho kuwa hatuna uwezo wa kuwasaidia kwa sababu tumebeba majukumu mengi hivyo fedha hatuna. Na wala hatuji JF kulialia kuwa tunasumbuliwa na ndugu zetu kwa sababu tunajua hilo ni jambo la kawaida kwa jamii za kiafrika. Sasa wewe jitie kijogoo uendelee kujifanya una uwezo wa kusikiliza na kumfurahisha kila mtu. Kwa kifupi dawa siyo kuja kulialia hapa bali ni kuwaambia watu ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…