MAJOR GENERAL QASSEM SOLEIMAN: A Fully Trained Commando na mbabe katika medani ya vita eneo zima la Mashariki ya Kati na Afrika ya Waarabu

NB: Usiibe makala za Infantry Soldier kwenye groups za WhatsApp na Facebook bila idhini yake
View attachment 1313820

Mbabe na mwamba katika medani za kivita katika eneo lote la Mashariki ya kati General Qassem Soleiman ameshamaliza majukumu yake na sasa amepumzika katika ufalme wa Mungu huku harakati zake zikiwa zimeshaonekana Dunia nzima.

Je, huyu mwamba Qassem Soleiman ni nani hadi Dunia itikisike baada ya kifo chake!!?

Hapo mwanzo wale wasiomjua walikuwa wakimbeza sana kuwa si lolote si chochote lakini leo hii wao wenyewe wanakiri kuwa alikuwa ni mwamba kweli, wanakiri kuwa alikuwa ni chuma cha pua. Wanakiri kuwa kwa hakika alikuwa ni KINGPIN.

Yaani athari za kifo chake zimetikisa mpaka mifuko yetu sisi wananchi wa kawaida kwenye mataifa mengine kwa kusababisha ongezeko la bei ya mafuta.

Huyo ndiye General Qassem Soleiman, kiongozi wa IRGC ( The Islamic Revolutionary Guard Corps ) ambalo ni mojawapo katika matawi ya jeshi la Iran linalohusika na ulinzi wa mapinduzi na operation za kijeshi zinazofanyika nje ya Iran ambaye ameuawa jana Januari 02, 2019 karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghada nchini Iraq alipokuwa akijiandaa kwa ajili ya kuondoka Iraq baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi. Gari alilopanda lilishambuliwa na ndege isiyokuwa na rubani (UAV) ya jeshi la Marekani kwa amri ya rais Donald Trump.

Watu wengi wanachanganya baina ya Jeshi la Iran (Artesh) na jeshi la ulinzi wa mapindunzi (SEPAH au IRGC). Ni kwamba IRGC ni tawi tu lililokuwa likiongozwa na huyu mwamba Qassem Soleiman ambaye ni miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu katika jeshi la Iran.

Mkuu wa majeshi ya Iran ni Major General Mohammad Bagheri. Ingawa Major General Qassem Soleiman alikuwa akiripoti moja kwa moja kwa Ayatollah Khamenei lakini mkuu wake wa kazi ni huyo Mohammad Bagheri.

Huyu mwamba katika medani ya vita alizaliwa mwaka 1957 na kujiunga na jeshi la Iran mnamo mwaka 1979. Katika kipindi chote cha utumishi wake jeshini ameshiriki kwenye operation kubwa na ndogo 59 za kijeshi ndani na nje ya Iran.

Miongoni mwa operation kubwa alizoshiriki ni pamoja na vita kati ya Israel na Lebanon ya mwaka 1985-2000 ( South Lebanon conflict (1985–2000) ambapo Israel ilishindwa vita na kuondoa majeshi yake kusini mwa Lebanon, vita kati ya Israel na Lebanon ya mwaka 2006 ( 2006 Israel–Hezbollah War )ambapo kila upande ulijitangazia ushindi, na Vita dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic state huko nchini Iraq na Syria. Pia amekuwa akiratibu na kubuni mipango katika vita vya kiwakala (Proxy war) baina ya Iran na Israel kupitia makundi ya Hamas na Hizbullah.

Mafunzo ya kijeshi na mbinu zake za kivita huko Yemen zimefanikiwa kuisambaratisha Saudi Arabia kwenye uwanja wa vita na kuwafanya Wapiganaji wa Hauthi kuendelea kuiongoza Yemen.

Ndiye aliyefanikisha kumbakiza madarakani Rais Bashar al Assad kwa kupeleka maelfu ya Wapiganaji wa kishia kutoka Iran, Iraq na Afghanistan ili kuliongezea nguvu jeshi la Syria lililokuwa tayari limeshapoteza udhibiti wa ardhi ya Syria ambayo iliangukia mikononi mwa makundi ya waasi yaliyokuwa yakiungwa mkono na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uturuki na Saudi Arabia.

Bila huyu Qassem Soleiman leo hii Israel isingekuwa na Iron dome maana mafunzo yake kwa hamas ndio chanzo cha yale maroketi yanayoichapa Israel kila kukicha.

Generali Qassem Soleiman amekufa kishujaa huku akiiacha Iran likiwa ni taifa lenye nguvu kubwa kijeshi kuliko mataifa yote ya Mashariki ya kati. Ikumbukwe kuwa mashariki ya kati kuna nchi inaitwa Israel ambayo inasifiwa kuwa ina nguvu kubwa kijeshi lakini nguvu yao inatokana na kubebwa na mataifa makubwa ya Marekani na Ulaya magharibi ikiwa ni pamoja na kusaidiwa hadi bajeti ya ulinzi ya kila mwaka ya ulinzi. Yaani siku hayo mataifa yanayoibeba hiyo nchi yatakaposema hapana, basi hiyo nchi itakosa mahala wa kushika na kuanguka puuu.

General Soleiman amekufa shujaa baada ya kufanikisha malengo ya Iran. Waliomuua wamechelewa kwani wamemuua baada ya kuwa amekwisha kamilisha malengo ya Iran. Nafasi yake katika jeshi la Ulinzi wa mapinduzi ya kiislam (IRGC) imechukuliwa na msaidizi sake Brigedier General Ismail Ghaan. Rest in peace Mwamba, Mbabe na Chuma general Qassem Suleiman.

View attachment 1313823

Jr
 
umesema kwamba Iran ndo anaongoza kijeshi hapo mashariki ya kati na si Israel kwa sababu Israel anasaidiwa na ulaya na marekani ila umesahau kwamba Iran anasaidiwa na urusi na silaha zake zote ni za urusi. so punguza ushabiki na uongee reality

pili aliyefanya assad wa syria akabaki madarakani ni urusi na si hyo iran unayosema ndo inaongoza kijeshi. vita ya syria ilipoanza iran na hezbolah na huyo soleiman waliingia kwa nguvu zao zote ila hadi dakika 45 za mchezo walikua hoi taabani na walikua wameshapoteza nusu ya watu wao na wakarelize hapo hawatoboi watu wanaopigana nao wamejipanga zaidi yao hivo wanahitaji nguvu yenye akili ndani yake(maana wao walienda na manguvu akili wakaziacha) hapo ndo soleiman akaenda moscow kuomba msaada na hapo ndo kipindi cha pili tukaona mabadiliko ya mchezo. sasa hapo aliyeleta ushindi ni solemani au russia? na je hapo nguvu ya iran iko wapi???
 
Umeandika kiushabiki mnoo, na umempamba kuliko uhalisia wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mtu hajapambwa hata tone, katika Uzi huu. Mwaandishi ameacha sifa nyingi Sana za huyu mwamba. Kwanza kabisa ni yeye aliyesafiri mpaka Moscow kumwomba Putin atume jeshi la anga nchini Syria. Huyu mtu pia alikuwa moja ya watu wa mwanzo kushirikiana na marekani kutoa taarifa za intelligence kuhusu kambi za Taliban katika Afghanistan..
Sifa za soleimani, ziliwatisha waisrael huku wakimkosa Mara kadhaa eg alepo 2016.
Mwaka 2017 alimzika mwamba mwingine alokufa Frontline major general election zaheerdin.
Inatosha kuandika kitabu Cha kurasa Mia 3 hivi kueleza action za mbabe KASSEM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kiukweli hujaandika kama mchambuzi! umeandika kama mwananchi wa Irani!
au ndio udini umekujaa!!
tupe faida na hasara zake! mfano marekani faida moja ni taifa lenye nguvu lakn linatumia nguvu zake vibaya kuonea hata wasio stahili
 
View attachment 1313820

Mbabe na mwamba katika medani za kivita katika eneo lote la Mashariki ya kati General Qassem Soleiman ameshamaliza majukumu yake na sasa amepumzika katika ufalme wa Mungu huku harakati zake zikiwa zimeshaonekana Dunia nzima.

Je, huyu mwamba Qassem Soleiman ni nani hadi Dunia itikisike baada ya kifo chake!!?

Hapo mwanzo wale wasiomjua walikuwa wakimbeza sana kuwa si lolote si chochote lakini leo hii wao wenyewe wanakiri kuwa alikuwa ni mwamba kweli, wanakiri kuwa alikuwa ni chuma cha pua. Wanakiri kuwa kwa hakika alikuwa ni KINGPIN.

Yaani athari za kifo chake zimetikisa mpaka mifuko yetu sisi wananchi wa kawaida kwenye mataifa mengine kwa kusababisha ongezeko la bei ya mafuta.

Huyo ndiye General Qassem Soleiman, kiongozi wa IRGC ( The Islamic Revolutionary Guard Corps ) ambalo ni mojawapo katika matawi ya jeshi la Iran linalohusika na ulinzi wa mapinduzi na operation za kijeshi zinazofanyika nje ya Iran ambaye ameuawa jana Januari 02, 2019 karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghada nchini Iraq alipokuwa akijiandaa kwa ajili ya kuondoka Iraq baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi. Gari alilopanda lilishambuliwa na ndege isiyokuwa na rubani (UAV) ya jeshi la Marekani kwa amri ya rais Donald Trump.

Watu wengi wanachanganya baina ya Jeshi la Iran (Artesh) na jeshi la ulinzi wa mapindunzi (SEPAH au IRGC). Ni kwamba IRGC ni tawi tu lililokuwa likiongozwa na huyu mwamba Qassem Soleiman ambaye ni miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu katika jeshi la Iran.

Mkuu wa majeshi ya Iran ni Major General Mohammad Bagheri. Ingawa Major General Qassem Soleiman alikuwa akiripoti moja kwa moja kwa Ayatollah Khamenei lakini mkuu wake wa kazi ni huyo Mohammad Bagheri.

Huyu mwamba katika medani ya vita alizaliwa mwaka 1957 na kujiunga na jeshi la Iran mnamo mwaka 1979. Katika kipindi chote cha utumishi wake jeshini ameshiriki kwenye operation kubwa na ndogo 59 za kijeshi ndani na nje ya Iran.

Miongoni mwa operation kubwa alizoshiriki ni pamoja na vita kati ya Israel na Lebanon ya mwaka 1985-2000 ( South Lebanon conflict (1985–2000) ambapo Israel ilishindwa vita na kuondoa majeshi yake kusini mwa Lebanon, vita kati ya Israel na Lebanon ya mwaka 2006 ( 2006 Israel–Hezbollah War )ambapo kila upande ulijitangazia ushindi, na Vita dhidi ya kundi la kigaidi la Islamic state huko nchini Iraq na Syria. Pia amekuwa akiratibu na kubuni mipango katika vita vya kiwakala (Proxy war) baina ya Iran na Israel kupitia makundi ya Hamas na Hizbullah.

Mafunzo ya kijeshi na mbinu zake za kivita huko Yemen zimefanikiwa kuisambaratisha Saudi Arabia kwenye uwanja wa vita na kuwafanya Wapiganaji wa Hauthi kuendelea kuiongoza Yemen.

Ndiye aliyefanikisha kumbakiza madarakani Rais Bashar al Assad kwa kupeleka maelfu ya Wapiganaji wa kishia kutoka Iran, Iraq na Afghanistan ili kuliongezea nguvu jeshi la Syria lililokuwa tayari limeshapoteza udhibiti wa ardhi ya Syria ambayo iliangukia mikononi mwa makundi ya waasi yaliyokuwa yakiungwa mkono na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uturuki na Saudi Arabia.

Bila huyu Qassem Soleiman leo hii Israel isingekuwa na Iron dome maana mafunzo yake kwa hamas ndio chanzo cha yale maroketi yanayoichapa Israel kila kukicha.

Generali Qassem Soleiman amekufa kishujaa huku akiiacha Iran likiwa ni taifa lenye nguvu kubwa kijeshi kuliko mataifa yote ya Mashariki ya kati. Ikumbukwe kuwa mashariki ya kati kuna nchi inaitwa Israel ambayo inasifiwa kuwa ina nguvu kubwa kijeshi lakini nguvu yao inatokana na kubebwa na mataifa makubwa ya Marekani na Ulaya magharibi ikiwa ni pamoja na kusaidiwa hadi bajeti ya ulinzi ya kila mwaka ya ulinzi. Yaani siku hayo mataifa yanayoibeba hiyo nchi yatakaposema hapana, basi hiyo nchi itakosa mahala wa kushika na kuanguka puuu.

General Soleiman amekufa shujaa baada ya kufanikisha malengo ya Iran. Waliomuua wamechelewa kwani wamemuua baada ya kuwa amekwisha kamilisha malengo ya Iran. Nafasi yake katika jeshi la Ulinzi wa mapinduzi ya kiislam (IRGC) imechukuliwa na msaidizi sake Brigedier General Ismail Ghaan. Rest in peace Mwamba, Mbabe na Chuma general Qassem Suleiman.

View attachment 1313823

NB: Usiibe makala za Infantry Soldier kwenye groups za WhatsApp na Facebook bila idhini yake
walimuonea huruma sema alipogusa read line wakala kichwa. Marekan waliona nivyema wale kichwa kulipizia dam ya contractor ambaye inasemekana alikuwa mtu muhim sana ktk jeshi la marekan. Upendo wa marekan kwa huyu contractor ambaye inasemekana alkuwa brain behind USA waliona bora wammalize ajuwe hata yeye walimstai kwa muda wakiheshm sheria zaka mataifa. Niyeye alie toa amri yakumaliza yule contractor na kuvmia ubaloz wa USA.
 
Back
Top Bottom