Majlis ya Balozi Abbas Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,847
30,189
KUTOKA MAJILIS YA ABBAS SYKES

Kwa kipindi cha zaidi ya miaka thelathini si CCM wala si rafiki yake mpenzi Julius Nyerere alikuwa anafahamu Dossa anaishi vipi na ana hali gani.

Rafiki zake wachache waliokuwa wakimtembelea nyumbani kwake pale Mlandizi walihuzunishwa na hali yake.

Dossa ‘’The Bank,’’ jina la utani alilopewa na rafiki zake kwa ajili ya utajiri wake, mtu aliyekuwa na mali katika miaka ya 1950 alikuwa akiishi katika hali ya ufukara.

Hali hii ya ufukara ilitaka kumkosesha kuhudhuria Mkutano Mkuu wa CCM mwaka 1987 pale Kizota ambapo waasisi wote wa TANU walialikwa pamoja na mabalozi wa Tanzania waliokuwa wanawakilishi nchi nje ya mipaka yake.

Sababu kubwa ilikuwa ni ukosefu wa nguo na viatu vya kuvaa katika hadhara kama hiyo.

Balozi Sykes alinifahamisha kuwa yeye wakati yuko nje ubalozini kila akija Dar es Salaam alikuwa lazima aende nyumbani kwa Dossa Mlandizi kumjulia hali.

Watu hawa baba zao, Kleist Sykes na Aziz Ali walikuwa matajiri, watu maaarufu na marafiki wakubwa.

Dossa aliniambia kuwa yeye ni mkubwa sana kwa Abbas Sykes lakini walianza pamoja darasa la kwanza kwa sababu yeye alichelewa kupelekwa shule na baba yake.

Baba yake alimwambia kuwa yeye hatampeleka shule hadi ahitimu kwanza Qur’an yaani amalize kusoma juzuu zote 30.

Hii ndiyo sababu ya yeye kuchelewa kwenda shule.

Abbas Sykes alinambia, ‘’Nilimwambia Dossa lazima ahudhurie mkutano wa Kizota na nilihakikisha hilo.

Nilimwambia tutaondoka pamoja kwenda Dodoma kwa hiyo nilimnunulia nguo na viatu.’’

Balozi alinieleza maneno haya kwa shida sana na kwa hakika niliona kuwa historia ya Dossa ilikuwa imemuumiza sana.

Kisa cha Dossa kilinikumbusha mkasa wa Ali Migeyo nilioelezewa na Hamza Aziz.

Mimi na Hamza Aziz tulikuwa na Majlis yetu tunakaa wawili tu nje nyumbani kwake tunaangalia Bahari ya Hindi.

Katika Majlis hii nimepokea mengi sana.

Turudi kwa Ali Migeyo.

Ali Migeyo alikuwa katika viongozi shupavu wa TAA dhidi ya ukoloni Kanda ya Ziwa.

Migeyo alipigwa mabomu na Waingereza wakati anahutubia wananchi Kamachumu akafunguliwa kesi na akafungwa jela.

Wakati wa kuunda TANU yeye alikuwa jela anatumikia kifungo na kama isingekuwa kufungwa Migeyo angelihudhuria mkutano wa mwaka wa 1954 wa kuunda TANU.

Baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 Migeyo akawekwa kizuizini na serikali na alitumikia kifungo chake Ukonga Prison.

‘’Siku moja mwaka wa 1965 nikapokea simu kuwa nikamtoe Migeyo jela kwa kuwa ameteuliwa na Rais kuwa mbunge,’’ Hamza Aziz ananihadithia.

‘’Kufika jela nikamkuta Migeyo ndani ya selo yuko nusu uchi hana nguo kavaa matambara.

Nikamweleza Migeyo kuwa nimekuja kumtoa jela na kuwa ameteuliwa na Rais kuwa mbunge.

Nikamwambia lakini kwa hali ile aliyokuwanayo anisubiri nirudi mjini nikamnunulie nguo na viatu.

Basi nikaondoka hadi mjini kununua nguo ndipo niliporudi Ukonga kumchukua hadi International Hotel nikampangia chumba akae hapo wakati akisubiri kwenda kuapishwa.’’

Uhuru ulikuja na changamoto nyingi sana kuwa ukombozi wa Tanganyika umegeuka kuwa balaa kwa baadhi ya wapigania uhuru.

Turudi kwa Abbas Sykes.

Abbas Sykes alimpitia Dossa na wakaongozana kwenda mkutanoni Kizota.

Wakati Balozi Abbas Sykes ananihadithia uhusiano wake na Dossa tayari nilikuwa nimeshakutananae na kuiona hali yake.

Nilipelekwa kuonana na Dossa na Ally Sykes wakati nafanya utafiti wa kuandika kitabu cha Abdul Sykes.

Ilikuwa mwezi Aprili, 1987 asubuhi kiasi cha saa nne na tulimkuta Dossa Aziz amekaa barazani kwake akiwa amefungulia radio yake akisikiliza BBC.

Mara nilipotambulishwa kwake alinipokea kwa ukarimu mkubwa.

Ukarimu ulikuwa ndani ya damu ya Dossa na akaniambia kuwa akimjua baba yangu vizuri sana toka udogo wao.

Nakumbuka Dossa kunambia kuwa baba yangu alikuwa mtu mpole sana.

Mimi nilikuwa namwangalia huku nikishusha pumzi kwa huzuni.

Katika miaka ya 1930s babu yangu Salum Abdallah alikuwa na nyumba Mtaa wa Mbaruku jirani na nyumba ya Aziz Ali, baba yake Dossa.

Sifa zao zikijulikana na wote.

Mbele ya baraza yake yalikuwepo mabaki ya Landrover ambayo Dossa alimfahamisha mwandishi kuwa gari ile aliitumia na Nyerere katika safari za kutembelea majimbo ya Tanganyika kwa niaba ya TANU wakati wa kudai uhuru.

Mzee Dossa akionyesha kidole mabaki ya gari yake alisema, "Gari hii imetembea sehemu nyingi sana nikimpeleka Nyerere sehemu tofauti za Tanganyika na katika siku za mwanzo mimi mwenyewe ndiye nilikuwa nikiiendesha gari hii hadi pale tulipomwajiri Said Kamtawa kama dereva wa TANU."

Dossa alionyesha dalili zote za kupigwa na maisha.

Katika picha ya pamoja ya waasisi wa TANU kuna watu wawili tu ambao wanaonekana wamevaa suti na tai, hao ni Abdul Sykes na Dossa Aziz.

Hii ilikuwa ishara tosha ya hadhi zao.

Waliobaki wote wamejivalia mavazi yao ya kawaida.

Picha hii imebeba maneno elfu moja.

Dossa aliyeonekana pale kibarazani Mlandizi si yule aliyekuwa kwenye picha ya waasisi wa TANU.

Dossa mtanashati, mtoto wa Mwafrika tajiri, Aziz Ali, Waziri Dossa Aziz aliyetoa mali kuipa TANU ili Nyerere aitumie katika shughuli za kuikomboa nchi alikuwa amechoka akionyesha dalili zote za kusahauliwa na nchi aliyoipigania ijitawale.

Balozi Sykes anasema jioni ile Kizota kwenye chakula cha jioni walichoalikwa wajumbe wa mkutano ule ndiyo baada ya miaka mingi, Nyerere akakutana na Dossa.

Balozi akanambia si wengi katika wale wajumbe walikuwa wanamjua au hata kupata kumuona Dossa ingawa wengi walikuwa wamemsikia kwa ajili ya sifa zake.

Abbas Sykes anasema, ‘’Nyerere alipata mshtuko mkubwa kwa hali aliyomuonanayo Dossa na sikushangaa alipojaribu kueleza hali ya Dossa kwa namna yake kama vile hali ile imesababishwa na yeye Dossa kupenda kuishi shamba.’’

Nyerere katika mazungumzo mepesi kwenye meza ya chakula alisema kuwa Dossa akipenda sana maisha ya kuishi shamba toka siku zile za kupigania uhuru, ‘’Mara nyingi sana Dossa akinishawishi tutafute mashamba tulime.’’

Abbas Sykes akanambia, ‘’Nyerere alikuwa najaribu kuileza hali ya Dossa na yeye kujiweka mbali na umasikini wa Dossa.’’

Haukupita muda mrefu Mwalimu akamnunulia Dossa gari na hiyo gari ikapelekwa nyumbani kwake Mlandizi.

Nilifarajika sana siku niko mjini nilipomuona Dossa Aziz akiendesha gari katika barabara za Dar es Salaam.

Siku moja nilikwenda kumtembelea Abbas Sykes.

Ukumbi wa Abbas Sykes umepambika vyema na ukiwa kwenye ukumbi wake unaiona Bahari ya Hindi kwa uzuri kabisa na upepo mzuri unakupiga.

Lakini kitu cha mvuto ni kitambaa cheusi cha Al Kaaba ambacho kakiweka katika fremu kubwa pale ukumbini.

Balozi Sykes akanieleza kuwa ameingia hadi ndani ya Kaaba na aliyemfanyia itifaki hiyo alikuwa Balozi Abdallah Sued wakati alipokuwa balozi wa Tanzania Saudi Arabia).

Hapo ukumbini kama ni msomaji wa magazeti utapambana na kila aina la chapisho kuanzia magazeti ya ndani hadi ya nje ya nchi.

Siku ile jicho langu liliangukia kwenye video inayoitwa, ''High Society,'' ni senema ya zamani sana katika miaka ya 1950.

Katika film ile kuna wachezaji nyota wa senema na wanamuziki wa wakati ule kama Bing Crosby.
Huyu alikuwa muimbaji mahiri sana.

Mwingine ni mpiga muziki wa jazz Louis Armstrong ambae alikuja Tanganyika mwaka wa 1960 na akapiga Ilala Stadium, yuko na Frank Sinatra ambae na yeye alikuwa mwimbaji maarufu na mcheza senema.

Kwa kitambo kirefu niliishika ile video na nikawa kama imenitoa pale.

Balozi Sykes alililiona lile akanambia, ''Mohamed mimi na baba yako tulitoka Kipata kwenda Avalon Cinema kwa miguu kuangalia film hiyo.''

Hii ilikuwa mwaka wa 1956.
Baba zangu hawa walikuwa vijana sana.

Miaka 90 si miaka midogo na Balozi Sykes ana mengi aliyoshuhudia.
Yapo yaliyokuwa anapenda kunihadithia na yapo nilihisi hakuwa anapenda sana kuyaeleza kwani yalimtia machungu kama vile yalivyonisikitisha mimi msikilizaji.

Nakumbuka siku aliponihadithia kwa ufupi tu historia ya Ramadhani Mashado Plantan juhudi zake katika kuunda TANU na sababu zilizomfanya atoke TANU mwaka wa 1958 na kuunda All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT).

Balozi anasema siku moja Tanganyika ishakuwa huru alikwenda kumsalimia Mashado Plantan nyumbani kwake Mtaa wa Lindi (sasa Mtaa wa Tatu bint Mzee) na hakuweza kujizuia alitokwa na machozi baada ya kuona ile hali aliyomkutanayo na alipokuwa akinieleza habari hii nilimuona akitoa kitambaa na kufuta machozi.

Mimi nilitosheka hata kama Balozi alikuwa kimya hakutaka kunieleza zaidi kwa nini alibubujikwa na machozi.

Wakati wa ukoloni Mashado Plantan alikuwa na gazeti Zuhra ambalo ndilo lilikuwa gazeti la kwanza kuandika harakati za Waafrika wa Tanganyika dhidi ya ukoloni na TANU ilipoasisiwa likawa gazeti la kwanza kumtangaza Nyerere na kujenga haiba yake kwa wananchi.

Labda tutasoma sababu ya machozi haya katika kumbukumbu zake alizokuwa anaandika.

Sheikh Mohammed naomba umalizie thawabu zako kwa kutupatia maelezo ya hizo picha, kwani unatupatia historia nzuri ya nchi yetu kwa sisi ambao kipindi hicho kilikuwa kable yetu.
 
Mzee Mohamed Said.
Ingawa mara nyingi nimemukosoa sana lakini siachi kusoma maandiko yako.

Kuna kitu kikubwa sana ninakiona kwenye maandiko yako.

Jambo kubwa ambalo siku zote nakushauri lakini seems hauna radhi nalo ni kuandika vitabu. Usijaze juzuu nyingi andika vitabu ambavyo sisi wa hali ya chini tuvinunue na kuelimika.

Kuna mengi sana yanakeherehesha masikio lakini yana uhalali wa kusikilizwa. Hizi political betrayal huwa zinaishia gizani. Tunapaswa kuelewa njia halisi zilizopitwa na wale woote waliojitolea sisi tuwe huru. Inawezekana serikali na historians wengi wamefocus kwenye eneo moja na siyo maeneo yote ya njia za Uhuru.

Alale pema mzee Abdul Sykes.
 
Kipaji...
Huacha caption makusudi kujua kama wasomaji watatambua picha.

Huyo ni Dossa.
Dosa nilikuwa namfahamu,utotoni miaka ya mwishoni ya 80 nilikuwa namuona nyumbani kwake Mlandizi amekaa barazani anakunywa chai,kila tukipita tulikuwa tunamuona yupo na chupa za chai.
Kuna shule ya sekondari Mlandizi inaitwa Dossa Azizi.
 
Nikiwa mpenzi mkubwa wa historia, kitu huwa najiuliza.. kwanini watu muhimu kama huyu Dossa Aziz na wenzake walikuja kutelekezwa na serikali, especially Nyerere? Maana kama ni Dossa naamini katika kadi za waanzilishi wa TANU, kadi yake ilikuwa ni miongoni mwa kadi zile 7 za awali. Lakin unakuja kukuta watu waliokuja kula maisha kipindi cha Nyerere ni kina George Kahama. Wakati hawakuweka chochote kwenye uhuru..
 
Mzee Mohamed Said.
Ingawa mara nyingi nimemukosoa sana lakini siachi kusoma maandiko yako.

Kuna kitu kikubwa sana ninakiona kwenye maandiko yako.

Jambo kubwa ambalo siku zote nakushauri lakini seems hauna radhi nalo ni kuandika vitabu. Usijaze juzuu nyingi andika vitabu ambavyo sisi wa hali ya chini tuvinunue na kuelimika.

Kuna mengi sana yanakeherehesha masikio lakini yana uhalali wa kusikilizwa. Hizi political betrayal huwa zinaishia gizani. Tunapaswa kuelewa njia halisi zilizopitwa na wale woote waliojitolea sisi tuwe huru. Inawezekana serikali na historians wengi wamefocus kwenye eneo moja na siyo maeneo yote ya njia za Uhuru.

Alale pema mzee Abdul Sykes.
Msanii
Nimeandika vitabu 10.
 
Msanii
Nimeandika vitabu 10.
Basi punguza uchoyo uwe unavinadi kwenye posts zako ili wenye ufahamu wavinunue.

Haya mambo usipoyaandika vyema kwenye vitabu sidhani kama atatokea mtu kuja kuandika.

Ni vizuri uliishi hii historia na hata una uwezo wa kutafiti. We need to know all sides za history ili tujitambue who are we really
 
Msanii,
Nimekusikia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom