Majipu ni matokeo ya mfumo ndani ya mfumo, mnyonge lazima akombolewe

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Wale wazee wa zamani kwa maana ya vijana na watoto wa miaka ile ya awamu ya kwanza, waliishi maisha fulani ambayo hayakuwa na makeke, lakini waliyafurahia, hovyo hivyo yalivyokuwa.

Wazee waliaminishwa kwenye maisha ya kijamaa, wakajaribu kadri wawezavyo kuishi bila ya makeke ya kumiliki mali nyingi. Walijaribu kadri wawezavyo kuishi kwa kufuata kanuni za mwana TANU. Wapo wengi walioweza, na wapo wachache ambao moyo wa kutafuta mali uliwajaa kiasi cha kushindwa kuendana na falsafa za kijamaa.

Baada ya fikra za kijamaa kuzidiwa nguvu na masuala ya masharti ya benki ya dunia ili tuweze kupewa fedha na matajiri, taratibu ule moyo wa kijamaa ukaanza kufa. Baada ya kila kitu kuwa ruksa, makucha halisi ya ubunifu wa watu kujitafutia mali, yakaanza kuonekana.

Ukaibuka mfumo ndani ya mfumo wa maisha uliokuwepo kwa muda mrefu tangu nyakati za azimio la Arusha, kitendo cha mfumo mpya dhalimu kuibuka, kikaja na laana ya kila mtu kula kwa uwezo wa nafasi aliyonayo maishani. Hapo ndipo aina nyingi za wizi zikaibuka, mnyonge ambaye hana ukaribu au undugu na mtu mwenye cheo, ndiye aliyeumia kimaisha.

Leo hii waliokula maisha kiasi cha kusahau shida za ndugu zao, wameshajiona kama vile wana kila haki ya kutetea udhalimu wao. Hawa ni wa kupambana nao bila hata ya kuwatazama usoni.

Kina mama mikoani wanajifungua kwa kutumia tochi za simu ya nokia za manesi, halafu bosi fulani anaishi kwa raha kwa sababu tu anao uwezo wa kuongeza sifuri kwenye makaratasi muhimu ya kiofisi. Watoto wanasomea kwenye mchanga, ubao ukiwa umetundikwa kwenye mti wa mwembe, mvua ikianza kunyesha ndio inakuwa kengele ya kwenda nyumbani, halafu kuna watu fulani wanaishi maisha ya mabilionea lakini ni waajiriwa wa serikali!.

Hili suala la kupambana na mfumo ndani ya mfumo ni vita yenye nia ya kusambaza utajiri wa nchi uweze kuwafikia wale walioathirika na uwepo wa mfumo ndani ya mfumo ulioanzishwa ukiwa na lengo bora kabisa. Hii ni vita ambayo jamii yenye nia njema haipaswi kuchoka kuipigana, iwe usiku iwe mchana.
 
Imenigusa
Na ni wazi Rais wetu ameonyeshwa kuwa na nia dhabiti kushughulikia mfumo huu wa kijinga wa kujilipa million 45 na kufanya kikao cha bodi marekani akati hio pesa ingetumika kujenga madawati kila Mwezi madawati 10000 leo hii tatizo la madawati tusingekuwa kuwa nalo
 
Kweli mkuu! Ttatizo langu sijawahi kuwa na imani na Serikali ya CCM, but i will be happy if JPM will prove me wrong. Let see 2020 matokeo ya juhudi zake!
 
Kweli mkuu! Ttatizo langu sijawahi kuwa na imani na Serikali ya CCM, but i will be happy if JPM will prove me wrong. Let see 2020 matokeo ya juhudi zake!
Nahifadhi MAWAZO NA UTASHI WANGU MPAKA NIONE ATALISHUGHULIKIA VIPI SUALA LA KATIBA MPYA
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Mtumbua majipu amekuwa mwiba kwa Lumumba
Dawa inayoponya ni ile chungu, utotoni tulikuwa tunaogopa sana kupigwa sindano ili tupone malaria. Lakini matokeo ya sindano yalikuwa ni ya haraka zaidi kuliko hata vidonge vya masaa. JPM anaipiga sindano CCM, na atapitisha chekeche zito sana ili akisafishe chama kiweze kurudi kwenye misingi iliyokusudiwa na waasisi.
 
Kweli mkuu! Ttatizo langu sijawahi kuwa na imani na Serikali ya CCM, but i will be happy if JPM will prove me wrong. Let see 2020 matokeo ya juhudi zake!
Mkuu , hii ni serikali ya JPM, siyo ya CCM. Maana CCM wenyewe hawaelewani na hawamwelewi JPM. Picha halisi litaonekana akipewa uenyekiti.
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Back
Top Bottom