Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Sifa kubwa ya kiongozi wa umma ni uwajibikaji wa kisiasa. Mwalimu Nyerere aliwahi kusema Kiongozi wa umma hata akituhumiwa tu inatosha kumpumzisha wakati ukitafuta ushahidi.
Kiongozi wa umma ni tofauti na mtumishi wa umma. Mtumishi wa umma unatafuta ushahidi kwanza ndipo unamuwajibisha, Lakini kiongozi wa umma unamuwajibisha kwanza kisiasa then ushahidi baadae.
Sifa ya Uwajibilkaji ndiyo iliyomfanya Mfalme Herode kumtimua mkewe alipotuhumiwa kuchepuka (miaka zaidi ya 2000 iliyopita). Sifa ya uwajibikaji ndiyo iliyomfanya Ali Hassan Mwinyi kujiuzulu nafasi yake ya Waziri wa mambo ya ndani baada yawafungwa kufia gerezani (japo yeye hakuhusika). Pia sifa ya uwajibikaji ndiyo iliyomfanya Ursula von der Leyen kujiuzulu nafasi yake kama Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani baada ya kutuhumiwa kucopy research yake ya PhD.
Watu wote hawa WALIWAJIBIKA kwa tuhuma tu. Hawakusubiri tuhuma hizo kudhibitishwa. Na hawakusubiri kuundwa Tume itakayosema walihusika au lah. Waliwajibika kisiasa. Uongozi wa kidemokrasia lazima ujenge mazingira mazuri ya viongozi kuwajibika hata kama ni kwa tuhuma tu.
Lakini uongozi wa Magufuli umekuwa vice-versa. Watumishi wa umma wanawajibishwa kwa tuhuma tu, lakini viongozi wa kisiasa wakituhumiwa hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi yao.
Wapo madaktari, Walimu, Wahasibu, Na watumishi wa kada nyingine serikalini ambao wamefukuzwa kazi kwa tuhuma tu na hawakupewa nafasi ya kujitetea (contrary to the principle of natural Justice). Lakini viongozi wa kisiasa wakituhumiwa wanaachwa tu na kupeta. Hili ni doa ktk serikali ya Magufuli.
Ikiwa Magufuli ana nia ya dhati ya kuleta mabadiliko nchini, basi namshauri awaondoe katika baraza lake mawaziri watatu ambao wana tuhuma nzito na hazivumiliki (serious allegetions).!
1. Sospeter MUHONGO,
Huyu ametuhumiwa kwenye kashfa ya mita za mafuta bandarini. Tuhuma zake ni nzito kwa sababu zilitolewa na Mtendaj Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Vipimo nchini Bi.Magdalena Chuwa mbele ya Waziri mkuu.
Ktk maelezo yake Chuwa alisema Waziri Muhongo alijua kuwa mita hazifanyi kazi lakini hakuchukua hayua yoyote hadi siku moja kabla ya ujio wa waziri mkuu ndipo akamtumia text kiongozi huyo wa WMA ili awashe mita hizo. Hizi ni tuhuma zinazopaswa kumuweka Muhongo pembeni kwa maslahi ya taifa.
2. JENESTA MHAGAMA,
Huyu ana tuhuma mbili. Ya Kwanza alifanya uteuzi wa Mkurugenzi mkuu wa NSSF kinyume na sheria maana sio jukumu lake kuteua wakuu sa mashirika ya hifadhi ya jamii. Aliingilia majukumu ya Rais. Mamlaka ya uteuzi ya wakuu wa Mashirika ya hifadhi za jamii kwa mujibu wa sheria ni Rais (Social security regulatory authority act 2008). Anaweza kuteua ikiwa tu Rais atampa ruhusa maalumu.
Pili, aliteua mtu asiye raia wa Tanzania. Dr.Carina Wangwe ni raia wa Uganda. Press release ya SSRA leo imedhibitisha kuwa Dr.Wangwe ni raia wa Uganda aliyeolewa na Mtanzania. Hivyo akaomba Uraia wa Tanzania mwaka 2001. So kwa sasa ni mtanzania.
Lakini katika nafasi nyeti kama Mkurugenzi Mkuu wa NSSF huwezi kumuweka raia wa Kuomba. Uma uhakika gani kama aliomba Uraia kwa maslahi ya nchi yake aliyozaliwa? Kwanini tumuamini kiasi cha kumpa ukuu wa NSSF? Ina maana hakuna Mtanzania wa kuzaliwa mwenye sifa hizo?
Howif kama Dr.wangwe anatumika kwa maslahi ya Uganda? Ina maana nchi hii imekosa raia wa kuzaliwa wenye kuweza kushika nafasi hiyo hadi apewe mtu mwenye uraia wa kuomba? Kuna baadhi ya nafasi ktk nchi zinapaswa kuwa za raia wa kuzaliwa tu.
Mtu amekana Uraia wa Uganda kisa kaolewa na Mtanzania. Vp kama hiyo ndoa ikivunjika akaolewa na Mjerumani si atakana uraia wa Tanzania pia? Kwa vyovyote vile Jenesta Mhagama anapaswa kupumzishwa kwa maslahi ya umma.
3. JANUARY MAKAMBA,
Huyu ametuhumiwa kufanya utapeli kwa kushirikiana na dada yake Mwamvita Makamba. Anadaiwa kumtapeli mfanyabiashara mmoja wa Italia kiasi cha dola molioni 1 sawa na Shilingi bilioni 2 na milioni 300 za kitanzania, ili amfanyie mpango wa kupata tenda ya kujenga bandari ya Bagamoyo.
Inadaiwa pia kuwa hii si mara ya kwanza kwa Makamba kufanya utapeli wa aina hii. Aliyetoa tuhuma hizo anasema January kwa kushirikiana na dada yake "wamewaliza wengi". Wengine wameamua kusema kama huyo muitaliano na wengine wameamua kukaa kimya na "kufa kiume".
Madai haya ni mazito maana yameambatanishwa na vielelezo kama email, sms na voice note ambazo mlalamikaji alikua akiwarekodi January na dada yake bila wao kujua.
Hata kama madai haya si ya kweli lakini ni LAZIMA January akae pembeni kwa maslahi ya umma. Hawezi kuendelea kuwa kiongozi huku akiwa na tuhuma kubwa kiasi hiki. Ni aibu na fedheha kwa nchi.
Mwambieni Magufuli awapumzishe hawa watatu kwa hatua za awali ili kurudisha imani yake kwa wananchi maana imeanza kupotea.
Alamsiki.!