namparu
Member
- Jul 6, 2014
- 38
- 15
Mh. Mbowe amewataja Marais wastaafu kikwete na mkapa, pamoja na katibu mkuu sefue kua ndio majipu hatari zaidi.
Binafsi nimejaribu kutafakari zaidi ya hapo na nashangaa mh. Magufuli kushindwa kugusa sehemu ambazo watanzania wamekuwa wakikutaja kwa kirefu kuwa ndiko hasa kunakorudisha nchi nyuma.
Maeneo hayo ni pamoja na madini na maliasili. Uporaji wa maliasili zetu, mikataba mibovu ya madini na mengine mengi nani yuko nyuma ya haya yote na kwanini mh. Magufuli hawezi kugusa huku.
Binafsi siamini kama tunaweza kutoka hapa tulipo bila kugusa pamoja na mengine hayo niliotaja hapo juu.
Namuomba mh. Magufuli atuambie kwanini hajaweza kufikia majipu hayo na kama hajui kinachoendelea juu ya mikataba ya madini yetu yanayoendelea kuisha bila faida kwa taifa pamoja na tembo wanaoendelea kuteketea.
Mh. Angalia pia suala la madawa ya kulevya!