Majina ya watoto (Vikembe) wa wanyama/viumbe...

Asamwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2012
Messages
2,917
Points
2,000

Asamwa

JF-Expert Member
Joined Apr 13, 2012
2,917 2,000
Kuna ripoti fulani nilikuwa nasoma nikakutana na neno "vifaranga" ikimaanisha samaki wachanga. Ni sawa samaki wachanga kuitwa vifaranga?

Majina mengine ya watoto (vikembe) wa wanyama mbalimbali ni kama ifuatavyo:

Ng'ombe......Ndama
Nzige...kimatu/maige/tunutu/matumatu/funutu
Ndege....Kinda
Kipepeo/nondo....kiwavi
Nzi......Buu
Farasi....Kitekli
Mamba...... Kigwena
Nyangumi..... Kinyangunya
Fisi.... Kikuto/bakaya
Ngamia..... Nirigi/nirihi
Paka.......kinyaunyau/kipusi
Ndovu.... Kidanga
Mbweha.... Nyamawa
Nyani...... Kigunge
Kondoo..... Kibebe/katama
Mbuzi.....Kibui/kibuli/kimeme
Farasi na punda.... Nyumbu
Punda.... Kiongwe/kihongwe
Mbu....kiluwiluwi
Chura.... kiluwiluwi
Kuku..... Kifaranga
Papa.... Kinengwe
Nyuki.... Jana
Simba..... Shibli
Sungura.....Kitungule
Kwanga/wibari.... " "
Samaki.... Chengo/kichengo
Chui.... Chongole/kisui
Mbwa..... Kilebu/kidue/kibwa
Nyoka...... Kinyemere
Njiwa..... Kipura
Wazazi wenye rangi tofauti.... Chotara/suriama

Naomba michango yenu mingine.
 

Nteko Vano

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Messages
435
Points
0

Nteko Vano

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2012
435 0
Kuna ripoti fulani nilikuwa nasoma nikakutana na neno "vifaranga" ikimaanisha samaki wachanga. Ni sawa samaki wachanga kuitwa vifaranga? Naomba michango yenu.
Ndio lugha inayotumika- vifaranga. Kwa kiingereza wanaita fish fingerlings or seed kwa samaki hawa wa kawaida. Ikiwa prawns watasema postlarvae na itabadilika kutokana na aina ya samaki.
 

naumbu

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Messages
4,640
Points
2,000

naumbu

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2010
4,640 2,000
Kuna ripoti fulani nilikuwa nasoma nikakutana na neno "vifaranga" ikimaanisha samaki wachanga. Ni sawa samaki wachanga kuitwa vifaranga? Naomba michango yenu.
samaki mchanga kule kwetu ina maana nyingine so jiandae kwa majibu usiyotarajia
 

chabuso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Messages
5,435
Points
2,000

chabuso

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2013
5,435 2,000
Kifaranga ni mtoto wa kuku/bata/ndege kwa ufupi viumbe jamii ya ndege watoto wao wanaitwa vifanga,vinaanguliwa kutoka kwenye mayai
Ndama ni mtoto wa ngo'mbe
Mtoto wa samaki anaitwa mtoto wa samaki
Mtoto wa mbwa anaitwa mtoto wa mbwa
Mtoto wa binadamu anaitwa mtoto wa binadamu
Hicho ndio kiswahili
 

Fofader

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2011
Messages
855
Points
225

Fofader

JF-Expert Member
Joined Sep 28, 2011
855 225
Kifaranga ni mtoto wa kuku/bata/ndege kwa ufupi viumbe jamii ya ndege watoto wao wanaitwa vifanga,vinaanguliwa kutoka kwenye mayai
Ndama ni mtoto wa ngo'mbe
Mtoto wa samaki anaitwa mtoto wa samaki
Mtoto wa mbwa anaitwa mtoto wa mbwa
Mtoto wa binadamu anaitwa mtoto wa binadamu
Hicho ndio kiswahili
Na kinda utaelezeaje?

Sent from my GT-P7500 using Tapatalk HD
 

chabuso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Messages
5,435
Points
2,000

chabuso

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2013
5,435 2,000
Mkuu mtoto wa kibua anaitwaje?
Kibua ni jamii ya samaki
mtoto wa kibua anaitwa kibua
mtoto wa tasi anaitwa tasi
mtoto wa nguru anaitwa nguru
mtoto wa pweza......
mtoto wa jodari.....
mtoto wa ngisi......
mtoto wa mkundaji.....
mtoto wa koana....
mtoto wa changu.....
mtoto wa nduwaro....
mtoto wa kasa.....
mtoto wa taa......
mtoto wa kolekole....
mtoto wa sumbururu.....
kaka unawajua hao samaki ;)
 

124 Ali

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2010
Messages
7,475
Points
2,000

124 Ali

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2010
7,475 2,000
Kifaranga ni mtoto wa kuku/bata/ndege kwa ufupi viumbe jamii ya ndege watoto wao wanaitwa vifanga,vinaanguliwa kutoka kwenye mayai
Ndama ni mtoto wa ngo'mbe
Mtoto wa samaki anaitwa mtoto wa samaki
Mtoto wa mbwa anaitwa mtoto wa mbwa
Mtoto wa binadamu anaitwa mtoto wa binadamu
Hicho ndio kiswahili
Mtoto wa mbwa anaitwa mtoto wa mbwa-kijibwa
Mtoto wa binadamu anaitwa mtoto wa binadamu-mwana/kichanga
 

chabuso

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Messages
5,435
Points
2,000

chabuso

JF-Expert Member
Joined Feb 18, 2013
5,435 2,000
Kinda ni hatua ya pili ya kifaranga katika ukuaji,hapa some how ana uwezo wa kujitambua/nakujisaidia sio helpless kama alipokuwa kifaranga.
Usifananishe kiswahili na lugha nyingine,watu wengi wanafananisha grama ya kiswahili na kingereza
kuwezi kumwita mtoto wa kuku kinda la kuku
wala huwezi kumwita kinda la ndege kifaranga cha ndege

hicho kitakuwa sio kiswahili itakuwa lugha iliyofanana na kiswahili lakini watu watakufahamu nini umekusudia
 

Forum statistics

Threads 1,389,755
Members 528,022
Posts 34,033,706
Top