Ili jiji likubalike ni jiji hata kama halina mataa ya kuongoza magari mitaa lazima iwe na vibao vya majina ya mitaa.
Bongo sijui kuna matatizo gani. Hata mtaa wenye makao makuu ya halmashauri ya mji unaweza usiwe na kibao cha jina la mtaa.
Majina ya mitaa yanaweza kuwekwa kwa maana maalumu. Na si lazima yawe magumu. Majina ya mitaa ya downtown Washington DC yako hivi upande mmoja ni 1, 2, 3, 4, 5 ..... na upande wa pili yanaorodhesha majimbo yote hamsini ya Marekani kwa kufuata alphabeti. Utakuta mitaa kama New York, Georgia, Connecticut, New Hampshire, New Jersey nk. Ni kama katikati ya jiji la Dar kuwe na mitaa ya Iringa, Arusha, Morogoro nk.
Hata halmashauri ya jiji ikijipanga kuweka vibao vya mitaa vinang'olewa sijui na mafundi wa majiko au watu wa skrepa yaani tabu tupu.
Bila ya kuwa na majina ya mitaa watu wataendelea kwenda posta kuchukua barua mpaka lini. Wataendelea kuchukua vifurushi vya mizigo stendi ya basi kwa makondakta mpaka lini.
Lini Bongo watu wataagiza vitu online kama mitaa haina majina?
Lini wabongo watu wataendesha magari kwa kutumia GPS bila ya majina ya mitaa.
Wabunge na vyama vya maendeleo mnatakiwa kupiga madebe vitu vya aina hii ambavyo vinawagusa wananchi moja kwa moja.
"Madongo yataendelea mpaka kieleweke".