Majina ya mitaa na namba za nyumba

Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
2,000
Ili jiji likubalike ni jiji hata kama halina mataa ya kuongoza magari mitaa lazima iwe na vibao vya majina ya mitaa.

Bongo sijui kuna matatizo gani. Hata mtaa wenye makao makuu ya halmashauri ya mji unaweza usiwe na kibao cha jina la mtaa.

Majina ya mitaa yanaweza kuwekwa kwa maana maalumu. Na si lazima yawe magumu. Majina ya mitaa ya downtown Washington DC yako hivi upande mmoja ni 1, 2, 3, 4, 5 ..... na upande wa pili yanaorodhesha majimbo yote hamsini ya Marekani kwa kufuata alphabeti. Utakuta mitaa kama New York, Georgia, Connecticut, New Hampshire, New Jersey nk. Ni kama katikati ya jiji la Dar kuwe na mitaa ya Iringa, Arusha, Morogoro nk.

Hata halmashauri ya jiji ikijipanga kuweka vibao vya mitaa vinang'olewa sijui na mafundi wa majiko au watu wa skrepa yaani tabu tupu.

Bila ya kuwa na majina ya mitaa watu wataendelea kwenda posta kuchukua barua mpaka lini. Wataendelea kuchukua vifurushi vya mizigo stendi ya basi kwa makondakta mpaka lini.

Lini Bongo watu wataagiza vitu online kama mitaa haina majina?

Lini wabongo watu wataendesha magari kwa kutumia GPS bila ya majina ya mitaa.

Wabunge na vyama vya maendeleo mnatakiwa kupiga madebe vitu vya aina hii ambavyo vinawagusa wananchi moja kwa moja.
21ce65c03d810d3625ba65d896daf1dc.jpg

"Madongo yataendelea mpaka kieleweke".
 
Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
2,000
Haina haja ya kuwa na mjomba Marekani siku hizi. Dunia imekuwa kijiji unaingia online unaagizia maziwa ya mwanao kutoka California. Sasa utaagiza vipi kama anuani yako ina neno moja tu Tabata.
 
Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
43,876
2,000
Mkuu huo mfumo shirika la posta na TCRA waliwahi kuutangaza ila sijui umefikia wapi
 
Mwelewa

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,352
2,000
Wazo zuri.

Mitaa kuwa na majina na kutambulika rasmi inarahisisha mawasiliano.
Rahisi kupokea vifurushi kutoka kokote duniani.

Anwani ya mtaa/nyumba unayoishi inafahamika kwa uwazi tu. Hivyo huduma inakufikia haraka na kwaurahisi.

Nakumbuka rafiki yangu anatoka Cape Town kabla ya flight inaonyesha aliulizwa anwani/number ya nyumba ninayoishi Dar es salaam (well, binafsi siishi Dar. Nilifikia kwa rafiki)

Teh teh napokea simu naulizwa number ya nyumba na mimi namuuliza mwenyeji wangu anacheka ananiambia hiyo mambo hakuna. Na nyumba ni bora kabisa.

Well haikuwa issue sana. Mgeni alifika.
Lakini kama mitaa tunayoishi ingetambulishwa rasmi kwa majina inapendeza zaidi.

Muhimu pia kwa usalama.

Mambo yanakuwa kwenye mpangilio sio shaghalabaghala aaaaarughh
 
Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
2,000
Hii yote ni kwa sababu wabunge wanaacha kupigania ya mitaani kwao wanakowakilisha wanapigania ya serikali kuu.
 
Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
2,000
Kuna magari siku hizi yanafanyiwa majaribio. Hayatumii dereva. Unalipa online gari linakuja linakuchukua linakupeleka unapoenda. Ukifika unateremka gari linakuambia have a nice day. Sasa bila ya mitaa gari la hivyo litafika lini Tanzania.
 
saburi kilonzo

New Member
May 6, 2017
4
45
Wazo zuri.

Mitaa kuwa na majina na kutambulika rasmi inarahisisha mawasiliano.
Rahisi kupokea vifurushi kutoka kokote duniani.

Anwani ya mtaa/nyumba unayoishi inafahamika kwa uwazi tu. Hivyo huduma inakufikia haraka na kwaurahisi.

Nakumbuka rafiki yangu anatoka Cape Town kabla ya flight inaonyesha aliulizwa anwani/number ya nyumba ninayoishi Dar es salaam (well, binafsi siishi Dar. Nilifikia kwa rafiki)

Teh teh napokea simu naulizwa number ya nyumba na mimi namuuliza mwenyeji wangu anacheka ananiambia hiyo mambo hakuna. Na nyumba ni bora kabisa.

Well haikuwa issue sana. Mgeni alifika.
Lakini kama mitaa tunayoishi ingetambulishwa rasmi kwa majina inapendeza zaidi.

Muhimu pia kwa usalama.

Mambo yanakuwa kwenye mpangilio sio shaghalabaghala aaaaarughh
Posta wanatakiwa wajue dunia imebadilika, kuwekwa vibao vya kutambulisha mitaa ni jambo la muhimu sana.
Wamesema muda mrefu lkn utakelezaji hakuna, nchi hii sijui nani kailoga
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
6,363
2,000
Kuna magari siku hizi yanafanyiwa majaribio. Hayatumii dereva. Unalipa online gari linakuja linakuchukua linakupeleka unapoenda. Ukifika unateremka gari linakuambia have a nice day. Sasa bila ya mitaa gari la hivyo litafika lini Tanzania.
2446553_IMG_9582.jpg

2446554_IMG_9583.jpg

NDINDA
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom