Majina ya ‘majiin’

Haya toka kwa jina la JIWE
Ndio maana nikasema yapo mafuta ambayo ukimnusisha mwenye majini basi huyo jini hutoka na unaweza kukaripia kwa kumuudhi kama mfano wa kusema "toka kwa jina la Yesu" hata ukisema toka kwa jina la Jamiiforum yeye hutoka tu kwa sababu ya hayo mafuta.
 
Ni kweli kwa asilimia mia islamic names

Sababu kubwa: Mungu anaelezea lengo la kuumbwa kwetu pale aliposema ktk Qur'an kwamba Hakuwaumba majini na watu "ila wamuabudu"

Uwezo wa viumbe hawa kizungumza kiarabu/mavazi na majina ya kiislam ni mesej tosha kwa watu wa ulimwengu huu Mungu kawafumbia wenye akili wapate kijua dini ya kweli hapa duniani ni ipi
 
Sawa, lakini ukweli ni huo, huwezi kumtoa au kumfukuza kiumbe chenye uwezo kuliko Binaadamu, kiumbe kilichomsaliti Mungu, kwa kumpiga kelele, "kwa jina la Yesu, toka, toka...." inabidi ujiongeze kidogo

Kwa nini usifanye jaribio? Jini ana uwezo much far kuliko binadamu, hilo halina ubishi. Lakini aliye ndani ya Yesu, ni mrithi pamoja na Kristo, amekuwa adopted na hivyo kufanyika mwana wa Mungu, mzaliwa wa pili baada ya Kristo. Yaani situation inakuwa hivi, Yesu anakuwa ni First Born, halafu aliye ndani ya Yesu anakuwa Second Born, yaani wanakuwa sawa tu kama wewe na wadogo zako au kaka zako uliozaliwa nao tumbo moja ulio nao hapo nyumbani kwenu. Kinachotakiwa tu kwa yule ambaye amekuwa adopted, inabidi AAMURU (na si kuomba) kwa Jina la Yesu, ili pepo atoke. Humwombi pepo atoke ila unamwamuru. Sasa inapokuja kwenye kuamuru, hapo ndiyo inaingia hadi hulka yetu sisi ya kibinadamu (ambayo si kosa, japo haichangii au haina uhusiano na pepo kutoka au kutokutoka), kwamba tuna kawaida ya kutoa amri kwa sauti yenye mkwara na ya juu sana, wakati kwa Jina la Yesu, kinachotakiwa ni maneno yenye amri tu hata kama utayatoa kwa sauti ya kawaida na ya upole, pepo lazima ang'oke. Wakati Yesu anaulaani mtini kwa kutokuwa na matunda, aliongea kwa sauti ya kawaida tu, hata namna alivyokuwa anaamuru mapepo yatoke, alikuwa anongea maneno ya amri na kwa sauti ya kawaida tu.
Ni kwamba ukishakuwa adopted na kufanyika mwana wa Mungu, nguvu yote ya Mungu inarithishwa kwako, na unakuwa na uwezo wa kuitumia to an unlimited extent, na kama ukiona kuna vitu bado vinaleta mgogoro pamoja na kuwa uko adopted, jua kuna mahali Mungu anapenda kukuweka uwe sawasawa, ili uwe CHOMBO CHAKE KIPYA, KIKALI CHA KUPULIA. Vinginevyo labda uwe haujasimama kisawasawa na Mungu, uko mguu ndani mguu nje, na hivyo huna uwezo wa kutumia mamlaka zake kwa ukamilifu kama unavyotakiwa, amekunyima uwezo unaostahili kuwa nao.
Muhimu tu ni kuwa huwezi ukamu-invoke Yesu ili utoe pepo. Wana wa Skewa kwenye kitabu cha Matendo ya Mitume, walikuwa wanafanya kitu hiki. Siku moja wakiwa wanajaribu kumtoa pepo, pepo aliwakatalia na akawazidi nguvu na kuwapiga vibaya sana. Wana wa Skewa hawakuwa ndani ya Yesu, hawakuwa na adoption na hivyo walikuwa wanafanya exorcism sawa tu kama vile anavyoweza kufanya Mganga wa Kienyeji. Hakuna nguvu iliyo juu ya Mungu, lakini pia ieleweke wazi kuwa hakuna binadamu aliye nje ya Mungu mwenye nguvu kumzidi Shetani, bado ana upako wa muda aliopewa na Mungu, hakunyang'anywa, ila upako wake uliwekewa tu kikomo.
 
Umenichanganya Mkuu, kwani nani hasa Yesu nani Kristo?!
 
Umenichanganya Mkuu, kwani nani hasa Yesu nani Kristo?!

Ni yule anayekupenda kuliko viumbe wote ambao umewahi kuwaona au kuwasikia, ila wewe mwenyewe hujui. Anapatikana Kanisani, nakushauri ukamtafute huko. Humu kwenye forum tunatofautina itikadi, hatuwezi kumjadili humu kwa kina, except kwamba tunaweza kupeana tu zile basics ambazo kila mmoja anaweza kuzi-accommodate
 
Kanisani nikamtafute nani Yesu au Kristo?? Yupi mmoja wao?
 
Usichokijua ni sawa na usiku wa kiza kinene. Fungua kamusi zote za Kiarabu halafu angalia maana ya neno Jinn (Kamusi kubwa za Kiarabu mojawapo ni Akrane). Neno jinn lina maana nyingi mojawapo ni, nyoka wakaao milimani, vijidudu vidogo vikaavyo kwenye takataka au bakteria, watu wakubwa kama viongozi wasiionekana mara kwa mara, n.k. Vyote , hivyo vimeitwa majinni. Hata aya inayozungumzia Majinni inaelezea kisa cha wafanyabiashara wa Kiyahudi wa kabila la Nasibin waliokutana na Mtume s.a.w akiwa anatoka Taif na akazungumza nao kuhusu Islam na kuwasomea aya zake.
Na ndio maana Quran mpaka tutakufa itabaki kwenye Asili yake ya Kiarabu. Ingekuwa inatafsiriwa na kupoteza uhalisia wake ungeweza kuwapotosha wengi sana hapa.

Tangulini Jini maana yake ni mtu mwenye hadhi kubwa.
 
Shekh! Kwa maelezo laini ni kwamba 'Majiin' wote ni 'waisilam' na wanaweza kumwingia yeyote muislam pia mkristo?
 
Sasa hivi wewe unafuga Mangapi muheshimiwa? Vipi huyo wa bibi nani kabaki nae
 
mnajidanganya, hakuna uchawi wala mambo ya kijini kama haya, ni story tu za hapa na pale na uzushi..
 
hahaha wajinga ndiyo waliwao.
Huyo Nabii Na Mashaka Naye!!
 
Kwani Lucifer na Yesebeli ni nani!? Hayo ni majina tu ya Majini kama vile Asha na Fatuma
Ahah tofautisha Ni vitu viwili tofauti
Majini Ni rank ya chini KABISA
Mapepo na majini,
Mapepo yapo Juu kwa majini!
 
dini ya uislamu ukisoma sana kuna steji unaweza kuijua dunia sana kuliko wakristo .
wakristo wazungu wametuficha vingi ili tusielewe kama wao ndo maana kuna siri nyingi.
majini yapo ya kila aina na elimu yake ni kubwa sana walio bahatika kupata.
Katika uislam majini ni kama mtu tu na hata ndani ya msaafu wamepewa sura moja kwenye Quran
 
Ahah tofautisha Ni vitu viwili tofauti
Majini Ni rank ya chini KABISA
Mapepo na majini,
Mapepo yapo Juu kwa majini!
Nani mapepo, nani Majini, unajichanganya Mkuu

Mungu kaumba, Malaika, Majini na Binaadamu pamoja na Wanyama..

Pepo, Ruhani ni miongoni mwa Majini sema wao wameokoka, ni wacha Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…