Majina ya ‘majiin’

Chief uliwahi kusikia jina linalojitambulisha kwa jina kama joseph, Aloyce au martha?

Bila kujali kuwa huyo aliyeingiwa na huyo 'pepo' ni mkristo, muislam au mpagani
 
Isikusumbue ndugu,ni sawa tu na kukuta mbwa kapewa jina kama, Maurice, john nk.
Haimaanishi kuwa hao mbwa nao ni wakristo ni majina tu.
Hainisumbui boss bali ni kaz ya akili siwezi kuizuia. Je uliwahi kuckia jini linaitwa isack?
 
Mara nyingine shetani hujifanya malaika wa nuru
 
Kuitwa Mkiristo ni kawaida sana kazi ipo kuwa na imani ya kweli isiyo changanyika, huyo mbibi ni mlozi aka mchawi
 
Suleiman wa quran ni tofauti sana na wa biblia
 
Kuitwa Mkiristo ni kawaida sana kazi ipo kuwa na imani ya kweli isiyo changanyika, huyo mbibi ni mlozi aka mchawi
Hapana yule Bibi alikuwa sio mchawi, Ukristo ni dini ya Kubuni, hakuna Hata sehemu moja katika Biblia Yesu kasema aabudiwe, au dini (gospel) anayoihubiri iitwe Kristo

Kristo neno La Kigiririki lenye maana "Aliepakwa Mafuta", Biblia vile vile ni neno la Kigiriki lenye maana Maktaba au mkusanyiko wa Vitabu
 
Hakika Quran haikuwacha kitu hata dawa na kinga hupatikana kwenye Quran. Masheikh wengi hutumia surat za Quran mfano suratul kursi ina kinga kubwa sana. Sasa sijui upande wa wakristo wao inakuwaje


Nangatukaa
TUNATUMIA JINA LA YESU
 
Aahah Laiti Ungejua!
Watu wanapambana na Lucifer na Yezebeli.
Sembuse Jini???
Sawa, lakini ukweli ni huo, huwezi kumtoa au kumfukuza kiumbe chenye uwezo kuliko Binaadamu, kiumbe kilichomsaliti Mungu, kwa kumpiga kelele, "kwa jina la Yesu, toka, toka...." inabidi ujiongeze kidogo
 
Sawa lakini je unaijua tofauti baina ya majini na masheitani?
Labda kwa kukuweka sawa nahitaji tofauti hapo kwanza
Majini ni viumbe vilivyoumbwa na Mungu, viumbe hivi havionekani, vinaishi duniani, vinaishi katika jamii tafauti,pamoja na Binaadamu, vina makabila tafauti, vina Miji yao nk

kwa ufupi Hawa viumbe ni sawa na Binaadamu, wanaishi katika mfumo kama tunavyoishi Binaadamu, wako Majini wazuri na wabaya, Gini akiwa kaasi, akiwa Muovu huitwa SHETANI..

MASHETANI ndio wanatumiwa na baadhi ya Binaadamu kufanya mambo Maovu..
 
Nakubali majini yana majina yao...zebaq,jupta,subiani,makata,pruto,na kuna jini kikongwe kabisa anaishi ktk MBAAZI anaitwa qdaz.
 
Aahah Laiti Ungejua!
Watu wanapambana na Lucifer na Yezebeli.
Sembuse Jini???
Kuna siku kwenye tv nilikuwa namuangalia nabii mmoja anatowa watu mapepo basi akaja kijana ndio ana jini na anasema ni Lucifer,ila kilichonifurahisha zaidi ni kiingereza chake huyo Lucifer maana alikuwa anaongea kiingereza ila kilikuwa cha kutafuta maneno. Nikaona huyu Lucifer anatakiwa akapigwe msasa na Ras simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…