Majiko ya nishati ya jua yanakuja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majiko ya nishati ya jua yanakuja

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by TandaleOne, Sep 8, 2010.

 1. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Majiko ya nishati ya jua kutengenezwa Shinyanga Send to a friend Tuesday, 07 September 2010 20:00 digg

  Zulfa Mfinanga, Shinyanga

  MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Yohana Balele ametoa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza majiko yatakayotumia nishati ya jua kwa lengo la kupambana na uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti.

  Dk Balele aliyasema hayo wakati wa ziara ya utambulisho wa majiko hayo iliyofanywa na shirika lisilio la kiserikali la Solar Oven Society Africa katika ukumbi wa hoteli ya Karena mjini hapa.

  Alisema Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa inayonyemelwa kwa karibu na jangwa kutokana na ongezeko kubwa la watu.

  Alisema hali hiyo inasababisha kuwepo kwa shughuli nyingi za kibinadmu kama vile ukataji miti kwa ajili ya utayarishaji wa makazi, ufugaji pamoja na kilimo.

  “Mkoa huu una watu takribani 3 milioni, na kila mwaka watu 100,000 wanaongezeka, pia kuna mifugo zaidi ya 4.5 wakati mkoa una uwezo wa kufuga mifugo 3.8 milioni tu, kwa hiyo hapa tunaona lazima kuwe na uharibifu mkubwa wa mazingira, hivyo nafurahi kusikia tunapata njia mbadala” alisema Dk Balele.

  Alisema ilikuwa vigumu kuwakataza watu kutumia kuni na kuacha kufuga kwa kuwa hakukuwa na njia mbadala na kuongeza kuwa kama teknolojia hiyo itakidhi haja ni wazi kuwa tatizo la uharibifu wa mazingira katika Mkoa wa Shinyanga utakwisha.

  "Ingawa mabadiliko ya tabia ya nchi pia huchangia uharibifu wa mazingira, lakini hili sina pa kulisemea kwa kuwa wewe huwezi kutuwasilishia hoja hii, ila kwa hatua hii ya majiko haya tunaweza kupunguza uharibifu huu",alisisitiza mkuu wa mkoa.

  Awali, akitambulisha mradi huo kaimu mwenyekiti wa Solar Oven Society Africa, Profesa Solomon Mwenda alimwambia mkuu wa mkoa kuwa lengo la kuanzishwa kwa kiwanda hicho ni kupambana na uharibifu wa mazingira unaotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi ikiwa ni pamoja na shughuli za binadamu ambapo mbali la kuokoa mazingira pia mradi huo utatoa ajira kwa wakati wa eneo husika.

  Alisema wilaya zilizotengwa kwa ajili ya majaribio ni wilaya ya Meatu, Longido, Ngorongoro pamoja na wilaya Serengeti kutokana na wilaya hizo kupiga hatua katika utunzaji wa mazingira huku wadau wakubwa ni shule za msingi na sekondari pamoja na vyuo vya elimu nchini.

  "Tutahamasisha wanafunzi kupanda miti baada ya kuwapa elimu juu ya utunzaji wa mazingira ili watumie majiko haya, pia sisi tutajitolea chakula kwa wanafunzi hao" alisema Profesa Mwenda.

  Naye mkurugenzi taasisi ya elimu endelevu Lweikaza Kisoza alisema kuwa uanzishwaji wa mradi huo utasaidia kupambana na umaskini kwani hivi sasa kaya maskini vijijini Tanzania zinatumia kiasi cha asilimia 35 ya kipato cha mwaka kwa ajili ya manunuzi ya nishati ya matumizi ya ndani tu
   
 2. D

  Dick JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ikitekelezwa, ni ukombozi kwa Watanzania pamoja na mazingira yetu.
   
 3. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Kweli ndugu
   
Loading...