Majibu ya Zitto juu ya shutma za kuhujumu CHADEMA

Kwanini DR Slaa hajibu shutuma za ufisadi zilizoanikwa na TUNTEMEKE?
Kwa sababu anajua Tuntemeke ni Freshthinking aka Zitto Kabwe aka matunguri na kama hujui tukukumbushe kwamba watu Kama akina DR Slaa huwezi kuwazzunguka wana watu wengi nyuma yao
 
There is a polish for everything that takes away rust; and the polish for the heart is the remembrance of Allah.

Chadema imeundwa na watu wengi toka huko mwanzo lakini ukweli usiofichika kuwa Dr na Zito ndio mihimili mikuu ndani ya chama hicho.

Hivyo kama kuna watu wangependa kuona chadema kina futika basi njia nyepesi ni kuweka kambi kwa watu hao wamwili kwa kuwa kila mmoja ana watu wake wanaomuamini na kumfata.

Hivyo wanaopiga kelele kuwa zkk aondoke au ni muongo au ana uchu wa madaraka ni ujinga tuu wa fikira kwa kuwa hata kama hamtaki leo ila ipo siku itafika chaguo lao atakuwa huyo kijana.

Nafikiri vijana wa Dr wanaumizwa sana na uwezo wa zkk hivyo wanatumika vibaya lakini na fahamu hii watu wengi watakuwa hawapendi kuona au kusikia lakini ukweli zkk ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana pale chadema.

kama hawataki au vipi lakini ukweli ndio huu, wapiga kelele wote wamesahau kuwa kijana huyu ndio pekee alikuwa anapita kila jimbo kupigia wenzake debe wakati wa uchanguzi ulio pita nani alifanya hivyo hata mwenyekiti wa chama bwana mbowe alijifungia hai.

go zkk ur the best na fahamu sanane hatakama anasema yeye ni mkweli na analinda chama ila alikukuta na ataondoka atakuacha hapo hao ni vijana wanao penda kuota kuaminika bila kujiaminisha

Mh Zitto alishajibu shutuma za kina saa8 na wenzake siku nyingi sana kama ifuatavyo:

1) Vipi madai kuwa unatumwa na CCM ili kupunguza nguvu ya CHADEMA? Kama si kweli unadhani kwanini watu wanakuona kama pandikizi ndani ya CHADEMA?

‘Baadhi ya watu wanapandikiza chuki hizi kwa sababu zao wenyewe. Hawanisumbui maana najua ni kikundi kidogo cha watu wachache wenye malengo yao ovu. Wajue tu kwamba hawawezi kuwadanganya Watanzania ambao wanafanya maamuzi yao sio tokana na propaganda ila kutokana na matendo ya kila mmoja.

Onyo: Watu hao hawawezi kummaliza Zitto kisiasa bila kuiathiri CHADEMA maana the imaage of Zitto is so intimately intertwined with CHADEMA that you couldn’t attack Zitto without jeopardizing the image of Chadema, and vice versa.
Wanaoeneza sumu hii hawana nia njema wala mapenzi na CHADEMA. Hawaelewi siasa. Wanafurahisha maadui wa CHADEMA. Maadui wanawachochea kwa kuwapa habari za uwongo na wao wanadhani watammaliza Zitto. Huwezi kummaliza Zitto bila kuiathiri CHADEMA. Hawatafanikiwa.’

2) Ni kweli kuwa una mkakati wa kuhamia CCM kabla ya 2015?
‘Sijawahi wala kufikiria kuhamia CCM. Kama nilivyosema hapo awali, sijawahi kuwa mwanachama wa chama kingine chochote tofauti na CHADEMA. Namwomba mungu kuwa niondoke duniani nikiwa chama hiki hiki. Siamini katika kuhama vyama. Ninaamini katika mfumo imara wa vyama vingi nchini. Ninaamini katika demokrasia pana.’

3) Vipi tetesi kuwa wewe na Kafulila mmeanzisha chama na una mkakati wa kutimkia huko?

‘Swali hili na lililotangulia yanaonyesha kuwa hizi kweli ni tetesi tu. Sasa kama unasema nina mkakati wa kuhamia CCM. Tena kuna tetesi nimeanzisha chama na nataka kuhamia huko, sasa mimi nina vyama vingapi nitakavyohamia?

Sijawahi hata kufikiria kuanzisha chama cha siasa. Chama changu ni CHADEMA na sitaondoka CHADEMA.
Kinachonisikitisha ni kwamba kuna viongozi wa CHADEMA wamekula sumu hii na bila woga wanaisema kana kwamba ni kweli.

It is very unfortunate Kiongozi wa chama makini kama CHADEMA kuamini ujinga na kuingia kwenye mitego kama hii.
Nataka ijulikane wazi kabisa kwamba, CCM haitachoka kutugawa. Haitachoka kupandikiza chuki miongoni mwetu. Wameshajua udhaifu upo wapi na wahenga walisema kamba hukatikia?’

Source: JF, 22 Nov 2012

Inaonekana wazi maadui wa Zitto wamekata tamaa na sasa wanaamua kumprovoke ili asuse na ahame CDM. Zitto, move on mungu atosha kuwa shahidi baina yao na wewe na siku zote penye ukweli uongo hujitenga.

i trust no witch, this guy is practicing witchery, he said so proudly. we are fed up with him to hell with zitto matunguri.
 
There is a polish for everything that takes away rust; and the polish for the heart is the remembrance of Allah.

Chadema imeundwa na watu wengi toka huko mwanzo lakini ukweli usiofichika kuwa Dr na Zito ndio mihimili mikuu ndani ya chama hicho.

Hivyo kama kuna watu wangependa kuona chadema kina futika basi njia nyepesi ni kuweka kambi kwa watu hao wamwili kwa kuwa kila mmoja ana watu wake wanaomuamini na kumfata.

Hivyo wanaopiga kelele kuwa zkk aondoke au ni muongo au ana uchu wa madaraka ni ujinga tuu wa fikira kwa kuwa hata kama hamtaki leo ila ipo siku itafika chaguo lao atakuwa huyo kijana.

Nafikiri vijana wa Dr wanaumizwa sana na uwezo wa zkk hivyo wanatumika vibaya lakini na fahamu hii watu wengi watakuwa hawapendi kuona au kusikia lakini ukweli zkk ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana pale chadema.

kama hawataki au vipi lakini ukweli ndio huu, wapiga kelele wote wamesahau kuwa kijana huyu ndio pekee alikuwa anapita kila jimbo kupigia wenzake debe wakati wa uchanguzi ulio pita nani alifanya hivyo hata mwenyekiti wa chama bwana mbowe alijifungia hai.

go zkk ur the best na fahamu sanane hatakama anasema yeye ni mkweli na analinda chama ila alikukuta na ataondoka atakuacha hapo hao ni vijana wanao penda kuota kuaminika bila kujiaminisha

Zitto ni mchawi kirusi mzandiki hawezi kuhujumu chama akajidai anajenga chama he has to go simple as that
 
Kwanini DR Slaa hajibu shutuma za ufisadi zilizoanikwa na TUNTEMEKE?

Dr.ajipange kuandaa mikakati na namna ya kueneza chama kwa watanzania wenye njaa,kiu,na hamu ya mabadiliko,masalia ni size ya wazalendo,na wananchi tunaohtaj mabadiliko,mbona hawana kitu kabisa sjui hata waliwezaje kuwa viongoz,wapuuzwe kabisa.ZZk,U can fool some people for some time,bt u can't fool all the people all the time(Reg.bob marley)we need changes and not rat killers(aka.Dumuzi)huwez saka uongoz kwa gharama ya kukiua chama.subira yavuta heri,why 2015?acha tuonje mabadiliko hayo mengine yafuate.
 
Jamani nilishasema hapo wali; ZITTO HASAFISHIKI HATA KWA JIKI...... Usaliti hajaanza leo huyu toka shule.... This is the most qualified OPPORTUNIST. To hell with him.... Chadema bado itasimama hata bila yeye kw taarifa yenu.
 
i trust no witch, this guy is practicing witchery, he said so proudly. we are fed up with him to hell with zitto matunguri.

Utasusa peke yako. Hiyo bad name waliitwa mpaka mitume itakuwa Zitto. Zitto go on doing better things for your country. Achana na vidudu mtu hivi vinavyokalia majungu badala ya maendeleo.
 
Jamani nilishasema hapo wali; ZITTO HASAFISHIKI HATA KWA JIKI...... Usaliti hajaanza leo huyu toka shule.... This is the most qualified OPPORTUNIST. To hell with him.... Chadema bado itasimama hata bila yeye kw taarifa yenu.

Hivi semeni ukweli kwa nini mnamchukia Zitto? Dr Slaa mbona anashutumiwa kwa kashfa za ufisadi hamumwambii atoe maelezo, au mnababaishia hapa kwa Zitto ili yapite?
 
Dr.ajipange kuandaa mikakati na namna ya kueneza chama kwa watanzania wenye Dumuzi)huwez saka uongoz kwa gharama ya kukiua chama.subira yavuta heri,why 2015?acha tuonje mabadiliko hayo mengine yafuate.

Na Zitto pia ana majukumu mengi ya kufanya na ya maaana kwa taifa hili, Freshthinking and others will deal with you vichwa maji hata hamfikirii. Hamuwezi hata kuficha chuki zenu binafsi!
 
Hapa mimi kama kichwa kimejam hivi wakuu.
Kina ben saa8 walitumika na zitto kumhujumu slaa
ben saa8 akatumwa na slaa kumpa sumu zitto
lakini zitto anasema hamjui ben hta kwa sura. Nani mbaya hapa?
 
Kwa sababu anajua Tuntemeke ni Freshthinking aka Zitto Kabwe aka matunguri na kama hujui tukukumbushe kwamba watu Kama akina DR Slaa huwezi kuwazzunguka wana watu wengi nyuma yao

Tunataka kiongozi ambaye akisema anachukizwa na rushwa na ufisadi, tuone kweli hata matendo na macho yake tukimwangalia yanaonyeshe hivyo, na awe tayari kuyasimamia yale anayoyaamini. aamini kwenye nguvu ya umma na sio katika kuugawa umma kama wanavyofanya wazee wa manyanga.
 
Hapa mimi kama kichwa kimejam hivi wakuu.
Kina ben saa8 walitumika na zitto kumhujumu slaa
ben saa8 akatumwa na slaa kumpa sumu zitto
lakini zitto anasema hamjui ben hta kwa sura. Nani mbaya hapa?

Pitia post ya Ben, yeye mwenyewe alikiri kwamba hajawi kuonana na Zitto katika maisha yake. Kwa mwenye akli hivi hajiulizi Zitto ni mjinga kiasi gani amuamini mtu ambaye hata kwa sura hamjui?
 
Tunataka kiongozi ambaye akisema anachukizwa na rushwa na ufisadi, tuone kweli hata matendo na macho yake tukimwangalia yanaonyeshe hivyo, na awe tayari kuyasimamia yale anayoyaamini. aamini kwenye nguvu ya umma na sio katika kuugawa umma kama wanavyofanya wazee wa manyanga.

Zitto anapambana na hivyo ulivyovitaja kweupe. Wengine ni maneno tu! Hajawahi kuchukua posho za vikao lakini wengine wanachukua, ametangaza mali zake laini wengine wanasua sua. Ila kwa vile yeye ameonesha ambition ya kuwa rais siku moja, wale wasiojiamini wanamuona tishio na kuanza kumpikia majungu. Its too late, time will tell na mtaumbuka tu.
 
Pitia post ya Ben, yeye mwenyewe alikiri kwamba hajawi kuonana na Zitto katika maisha yake. Kwa mwenye akli hivi hajiulizi Zitto ni mjinga kiasi gani amuamini mtu ambaye hata kwa sura hamjui?
Nimejaribu kupitia post nyingi za Ben Saanane hakuna mahali amesema hayo maneno yako hapo juu, zaidi anasema anafahamiana vizuri sana tena kwa karibu sana kisiasa na Zitto.

Kitu pekee ambacho Ben Saanane amekiri ni kuwa hakwenda kwa waganga wa Zitto kuapishwa ili asimsaliti Zitto.
 
Kweli zzk amewekeza sana kwa watetezi. Ila naamini hasafishiki kirahisi hivi. Dawa yake ni kutubu na kubadili tabia sasa
 
Nimejaribu kupitia post nyingi za Ben Saanane hakuna mahali amesema hayo maneno yako hapo juu, zaidi anasema anafahamiana vizuri sana tena kwa karibu sana kisiasa na Zitto.

Kitu pekee ambacho Ben Saanane amekiri ni kuwa hakwenda kwa waganga wa Zitto kuapishwa ili asimsaliti Zitto.

Njia ya muongo ni fupi sana. Nenda katika post za BEN ukikuta kuna anaposema alishawahi kuonana na Zitto uweke hapa. Sehemu zote anasema alikuwa akiwasiliana naye.... so many times. Wapi alishawahi kuonana naye na wapi?
 
Back
Top Bottom