the ultimatum
JF-Expert Member
- Dec 16, 2012
- 419
- 142
Leo tar 28/08/2013 katika kikao cha bunge session ya asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu wabunge watatu walisimama kuomba mwongozo wa spika. Wabunge hao ni Christopher Ole Sendeka, Hezekiah Wenje na mbunge mmoja wa jinsia ya kike sikuweza kumfahamu ni nani. Ole Sendeka aliomba mwongozo wa spika juu ya majibu yaliyotolewa jana na William Lukuvi bungeni kuhusu kutokuwataja wahusika wa biashara ya madawa ya kulevya ambapo alidai na wabunge nao wapo. Sendeka alitaka ama waziri afute kauli au awataje wahusika wa biashara hiyo kwani kutokuwataja kusingeleta taswira nzuri kwa wabunge mbele ya wananchi kwani baadhi yao akiwemo yeye Ole Sendeka hafahamu hata madawa ya kulevya yanafananaje. Mbunge wa pili (Mwanamke) nae alitaka muongozo wa majibu ya maswali yake aliyopewa leo bungeni. Hezekiah Wenje alitaka mwongozo juu ya maswali aliyouliza Mwigulu Nchemba leo bungeni. Aliomba mwongozo juu ya shutuma alizotoa bungeni kwa mwenyekiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe na katibu wake Dr. Willibroad Slaa kwamba kwa mauaji yaliyotokea Morogoro, Arusha na kwingineko kama mahakama ingekuwa inatenda haki basi ingewashitaki Mbowe na Slaa kwani wanahusika..Wenje aliongeza, makada wa CCM mkoani mwanza walimchinja kwa chain saw kiongozi wa CHADEMA na watuhumiwa walikamatwa lakini walitoroka mikononi mwa polisi wakiwa wamefungwa pingu na kwamba wangeweza kusema walitumwa na nani kufanya mauaji yale. Akijibu kwa kifupi sana, Job Ndugai alisema "Kutokana na muda nitaruhusu majibu ya hoja moja tu" Kisha akasimama William Lukuvi kujibu mwongozo wa Ole Sendeka wa madawa ya kulevya na wabunge. Baada ya hapo katibu wa bunge akatoa utaratibu wa hoja ya AZIMIO na bunge likatumia takribani dakika 45 kutoa pongezi kwa mbunge Anne Makinda aliyechaguliwa kuwa rais wa mabunge ya Afrika ambapo baadaye wabunge watatu walisimama kuchangia hoja. Wabunge hao ni Anna Abdallah, Hamadi Rashidi na Prof. Mark Mwandosya ambao wote walimsifia Anne Makinda
Kutokana na hoja ya muda bungeni aliyoitoa Ndugai nahoji yafuatayo:-
1. Kama kipindi cha maswali na majibu bungeni kinapaswa kuisha saa nne asubuhi, yaani muda wa saa moja tangu saa tatu asubuhi. Kulikuwa na sababu gani kwa jana na leo kuzidisha muda wa maswali na majibu?
2. Kama swala ni muda Ndugai aliona shida gani kuomba majibu yajibiwe kwa kifupi?
3. Kwa hoja ya muda inapingana na baadhi ya kanuni za bunge ambazo zinarushu kuongeza muda kwa baadhi ya hoja hasa za serikali. Ingawa kanuni hizo zisingetumika hapa lakini zinaonesha ni vipi muda sio kikwazo katika mijadala bungeni kwani hicho ndicho kilichowapeleka wabunge bungeni
4. Kama swala ni muda kulikuwa na sababu gani kutumia takribani dakika 45 kajadili katika kile walichokiita AZIMIO ambapo kwa muda wote huo walikuwa wanatoa pongezi kwa Anne Makinda kwa kuchaguliwa kuwa rais wa mabunge ya Afrika.