Gamlemilwe
JF-Expert Member
- May 26, 2013
- 290
- 200
Leo tarehe 15.06.2017 Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI imeulizwa Bungeni juu ya kusitishwa kwa uhamisho wa watumishi wa umma kwa kipindi kirefu sasa. Muulizaji wa swali ameeleza kwamba kitendo hicho cha kusitisha uhamisho kimeleta adha na madhara makubwa hususani kwa wanandoa ambao imeshindikana kwa mume au mke kumfuata mwenzi wake.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Wizara ya OR- TAMISEMI Mhe. Jaffo ameeleza kwamba ni kweli uhamisho wa watumishi wa umma ulisimamisha kupisha zoezi la uhakiki wa watumishi wa umma. Hivyo ameeleza kwamba serikali iko katika hatua za mwisho kukamilisha baadhi ya taratibu na baada ya kukamilisha wataruhusu uhamisho kuendelea.