Majibu rahisi kwa maswali magumu

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Swali la kwanza: Wanafunzi kuandika matusi na bongo fleva kwenye mitihani ya kumaliza kidato cha nne
Jibu: Wafungulie mashitaka kwa kutukana na wachunguzwe akili zao..... really??

Swali la pili:
Maandamano ya wananchi (Songea) kupinga mauji ya holela ya raia wasio na hatia
Jibu: Ushirikina na wanasiasa ..... really?

Haya ni mambo machache ambayo yanaonyesha jinsi tulivyo wazembe wa kufikiri ama kwa makusudi ama kwa kutaka kufunika udhaifu wetu katika kutatua changamoto zetu kama taifa.

Mambo haya mawili ukiyatazama kwa juu juu yanaonekana kama matukio yasiyo na uhusiano lakini ukiyamulika kwa karibu utaona kuwa yanafanana na yanasitahili majibu ya haraka kuliko hizi kanyaboya zinazotolewa na "viongozi" wetu.

Wahusika wakuu kwenye matukio yote mawili ni vijana wa umri ambao wanatakiwa wawe na matumaini na kesho yao lakini kutokana na siasa zetu uchwara na ukosefu wa uwajibikaji vijana hawa hawana matumaini na kesho yao.

Vijana walioandika bongo fleva na matusi kwenye mitihani yao huenda walifanya hivyo kutokana na kukosa cha kuandika kwani vitu walivyokuwa wanaulizwa hawajawahi kufundishwa na hivyo ama wangeliweza kuondoka bila kuandika chochote ama kutuma ujumbe kwa wahusika (ambacho walifanya) kuwa mitihani ile haina maana yoyote kwao kwa sababu wametelekezwa na mfumo wa elimu uliopo.
Kwa upande mwingine maandamano ya jana Songea - wahusika wengi ni vijana wa umri chini ya miaka 40 na ambao ni nguvu kazi ya jamii yoyote ile, hawa wanastahili wawe wanazalisha lakini kutokana na kuwa tumeamua kuwa taifa la wachuuzi tumewalazimisha vijana hawa ama kukosa kazi ama kuwa na kazi kidogo kiasi kwamba ni rahisi mno kuwashawishi kuingia kwenye maandamano ama zogo lolote kwani hawana cha kufanya na pia hawana cha kupoteza.

Badala ya kuyatafutia majibu stahili "viongozi" wetu wanahangaika na dalili huku ugonjwa ukisambaa kwa kasi na si muda mrefu taifa hili litakoma kuwa kisiwa cha amani.

Ukichukua dhuluma ukajumlisha na ukosefu wa ajira matokeo yake ni vurugu na fujo zisizo mithilika!

Mtani upo hapo lakini?
 
Back
Top Bottom