Majibu: Kwanini Nyerere hakuvaa sare za CCM?

Majibu: Kwanini Nyerere hakuvaa sare za CCM?

Je Hayati Baba wa Taifa ameshawahi kukemea nyinyiemu na kutishia kurudisha kadi kwasababu kimekengeuka toka kwenye misingi yake? na je hajawahi kusema kuwa katika vyama vyote vilivyoanzishwa alivutiwa zaidi na sera za CDM lakini alisema kuwa hawezi hamia huko kisa kimeanzishwa na hasimu wake Mzee Mtei? kumbuka walikorofishana katika maswala ya kushusha thamani ya shilingi Mzee Mtei alipokuwa gavana
 
Waliosema hivyo ni wanafiki wakubwa wasio penda maendeleo ya taifa letu
mnakosa hoja za msingi mnaanza kuongelea mavazi.

Hivi hoja za msingi ni zipi hasa? Au ndo hizi za kuongelea viongozi wa chadema kuwa na kadi za ccm? Najaribu kufikiri tu.
 
Ni kweli kuwa uelewa wa wananchi umeongezeka kwa kuwa wengi wamepata ELIMU angalau hata ya msingi na sekondari lakini idadi ya wasomi pia hivi sasa ni kubwa maradufu ukilinganisha na siku za nyuma, hii ndio kusema kuwa CCM imefanya kazi yake ipasavyo ya kuandaa sera ya upatikanaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari lakini pia ni kudhihirisha kuwa CCM imeisimamia vyema serikali yake katika kutimiza Ilani yake na Sera zake juu ya Elimu.

Lakini pamoja na Uelewa huo wa watu wetu, ni ukweli usiopingika kuwa wapo wananchi ambao wanaamini katika uzushi huu na propaganda chafu dhidi ya CCM, basi isingelikuwa ni busara kuwaelisha na kuwapa ufahamu wa sawasawa watu hawa..?? nadhani jambo la kusema kwa wananchi ni nini kimefanywa linasemwa sana na viongozi wa chama hasa katibu wa itikadi na uenezi Ndugu NNauye, na hili dogo la kuwaambia hawa wazushi kuwa mmesema jambo lisilo kichwa wala miguu, tunaweza wengine katika sisi kulisema na kulifafanua.

Mwenyezi Mungu atunusuru kama unaongelea wingi wa shule za kata kuwa ndo kuongezeka kwa elimu, hamna kipindi chochote kwenye historia ya nchi hii tulipozalisha wajinga wengi wasojua kusoma na kuandika waloingia sekondari, ni mwaka jana tu walofaulu kwa daraja la 1-3 walikuwa asilimia 11, which means effectively 89% walifeli, inatakiwa km taifa tujichunguze tumekosea wapi ili tuweze kujirudi.
 
KWA karibu wiki nzima iliyopita, wanachama na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakisambaza ujumbe mfupi wa maneno (sms) unaodai kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere hakuwahi kabisa kuvaa sare za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambazo ni suruali nyeusi na shati la rangi ya kijani “kwa sababu alikuwa amekichoka”.

Katika hali hiyo, waongo hao pia walidai alikuwa hazitaki sare hizo kwa sababu alikuwa na kinyongo nacho kwa kwenda kinyume cha malengo na misingi yake, hivyo wapiga kura wa mwaka 2015 wanapaswa waking’oe madarakani na kuiweka Chadema ili kumuenzi.

Nadhani nitumie fursa hii ndogo kutoa ufafanuzi wa jumla kwa wote waliotumiwa meseji hiyo ya kijinga,waliosoma thread mbalimbali zilizojadili hilo ama kuulizwa kwa namna yeyote ile.

Wakati Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM kuanzia Februari 5, 1977 hadi Agosti 16, 1990 alipong’atuka, sare hizo za chama zinazotumika sasa zilikuwa hazijaanza na hata kufikiriwa kwa namna yoyote.

Badala yake, suarali hizo nyeusi na shati hilo la kijani lililoshonwa katika sura inayofanana na kombati hasa za mgambo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), zilikuwa ni sare tu za Umoja wa Vijana (UVCCM) na chipukizi wake. Halikuwa vazi la TANU wala la CCM.

Sare zinazotumika sasa ambazo ni suruali au sketi nyeusi pamoja na mashati hayo ya kijani zimeanza kutumika wakati tayari ameng’atuka Uenyekiti wa Taifa wa CCM na kubaki tu mwanachama namba moja aliyekuwa na kadi Na. A 1.

Hata aliposhiriki kwenye vikao kama vya Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) au Mkutano Mkuu wa Taifa pia hakufanya hivyo akiwa mjumbe isipokuwa mgeni mwalikwa ambaye siyo lazima avae sare.

Katika kipindi chote alipokuwa Rais wa chama kilicholeta Uhuru cha Tanganyika African National Union (TANU) na hata Mwenyekiti wa Taifa wa CCM hadi alipong’atuka, wajumbe wa vikao vya chama walikuwa wakishona sare hususan mashati kutokana na vitenge vilivyobuniwa maalum kwa ajili ya tukio husika.

Mfano ulipofanyika Mkutano Mkuu wa Taifa wa uchaguzi mkuu au pengine NEC, Makao Makuu ya Chama yalikuwa yakitoa kitenge maalum na kuwasambazia wajumbe nchi nzima ili kila mmoja ashone shati lake. Hapakuwa na sare hizi nyeusi wala za kijani kama sasa. Zote zilianza wakati Mwenyekiti wa Taifa wa CCM akiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi baada ya mwaka 1992.

Zilianza baada ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa nchi ya vyama vingi vya siasa tofauti na mwanzo ilipokuwa ya mfumo wa chama kimoja ambacho pia kilitajwa kwamba ni CCM.

Zilibuniwa kwa sababu ya kuwatambulisha wana CCM wanapokuwa kwenye vikao vyao wenyewe, mikutano yao na hata vinginevyo ili kuepuka kuingiliwa kwa namna yoyote ile na mtu asiyehusika na shughuli zao.

Mtu anayesema vinginevyo au kumhusisha Mwalimu kukidhi matakwa yake ya kisiasa kwa kutaka kuwadanganya wapiga kura, kumtumia kwa utapeli au kuwataka wapiga kura waje waiweke madarakani Chadema mwaka 2015 kwa madai kuwa CCM ilishatengwa mpaka na mwasisi wake ni mzandiki na juha wa kisiasa.

Chadema wamekuwa wakihaha na kutafuta namna na mbuni mbalimbali za kuungwa mkono hasa katika kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015, kwa kueneza uzushi huu wanaamini kuwa itakuwa ndio kujisafishia njia ya kwenda ikulu, jambo ambalo hakika ni mwendawazimu wa kufikiri, labda mtu asiye fikiri sawasawa ndiye anayeweza kurubuniwa kwa njia hiyo.

Mtu anayetaka kujua ukweli akaingie maktaba yoyote yenye picha za vikao vya TANU au vya CCM vya wakati ambao Mwenyekiti wa Taifa alikuwa Mwalimu Julius Nyerere.

Hapo atakuta kwa mfano, wajumbe waliokuwa ni maofisa wa majeshi kama JWTZ, JKT, Jeshi la Polisi au Jeshi la Magereza kwa sababu kilikuwa kipindi cha mfumo wa chama kimoja tu cha siasa utakuta wamevalia sare zao halisi za kijeshi kama ilivyo nchini China, Korea Kaskazini, Vietnam au Kyuba hadi hivi leo.

Wachache kati yao ni pamoja na Jenerali Mirisho Hagai Sarakikya, hayati Jenerali Abdallah Twalipo, Jenerali David Musuguri, hayati Jenerali Mwita Kyaro, hayati Luteni Jenerali Silas Mayunga, hayati Meja Jenerali Mwita Marwa na kadhalika.

Mbali na CCM kutokuwa na sare katika kipindi hicho chote, hata Chadema yenyewe licha ya kuanzishwa na Mzee Edwin Mtei tangu mwaka 1992, lakini ni majuzi tu wakati Mwenyekiti wa Taifa wa sasa, Freeman Mbowe alipokuwa akigombea urais mwaka 2005 ndipo alipokuja na mavazi ya khaki na kutangaza kwamba hatayavua “mpaka kieleweke”.

Hakusema kwamba yanakuwa sare za chama hicho lakini ilipofika mwaka 2010 ndipo idadi kubwa ya wanachama wakayafanya kuwa maalum kwa ajili hiyo.

Leo kwa mfano mtu akiuliza kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema aliyetangulia kabla ya Mbowe, hayati Bob Makani amewahi kuvaa sare hizo za khaki jibu lake ni “hapana”, lakini haimaanishi kwamba alikuwa hakipendi chama hicho isipokuwa vinginevyo.

Mbali na Makani, hakuna pia picha yoyote inayomuonyesha mwasisi wa Chadema, Mzee Edwin Mtei akiongoza kikao chochote cha Kamati Kuu, Baraza Kuu la Taifa, Mkutano Mkuu wa Taifa au pengine akihutubia popote wakati wote alipokuwa Mwenyekiti wa Taifa huku akiwa na kombati hizo za khaki.

Narudia tena kuwa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere hakuwahi kuvaa sare hizo za CCM zinazotumika sasa siyo kwa sababu alikuwa hakipendi chama chake na kudai hivyo ni ujinga wa kufikiri.

Nadhani japo sare hizo zilianza kutumika 1992 na kwa kuwa alikuwa ni mwanachama wa CCM bado angeweza kuzivaa endapo angependa kufanya hivyo kwa hata leo tunaona baadhi ya viongozi wastaafu wa CCM kama mkapa wanapoalikwa kwenye vikao vya chama wanavaa lakini kwa nini yeye hakuvaa labda ilitokana na mtazamo wake aliokuwa nao yeye hakuangalia chama kama chama bali aliangalia taifa kama taifa na hata alipozungumza hakuzungumza kutetea chama bali alizungumza kwa maslahi ya nchi kwa hiyo, hiyo yaweza kuwa moja ya sababu
 
Ni kweli kuwa uelewa wa wananchi umeongezeka kwa kuwa wengi wamepata ELIMU angalau hata ya msingi na sekondari lakini idadi ya wasomi pia hivi sasa ni kubwa maradufu ukilinganisha na siku za nyuma, hii ndio kusema kuwa CCM imefanya kazi yake ipasavyo ya kuandaa sera ya upatikanaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari lakini pia ni kudhihirisha kuwa CCM imeisimamia vyema serikali yake katika kutimiza Ilani yake na Sera zake juu ya Elimu.

Lakini pamoja na Uelewa huo wa watu wetu, ni ukweli usiopingika kuwa wapo wananchi ambao wanaamini katika uzushi huu na propaganda chafu dhidi ya CCM, basi isingelikuwa ni busara kuwaelisha na kuwapa ufahamu wa sawasawa watu hawa..?? nadhani jambo la kusema kwa wananchi ni nini kimefanywa linasemwa sana na viongozi wa chama hasa katibu wa itikadi na uenezi Ndugu NNauye, na hili dogo la kuwaambia hawa wazushi kuwa mmesema jambo lisilo kichwa wala miguu, tunaweza wengine katika sisi kulisema na kulifafanua.

Mkuu Miaka 50 tangu uhuru bado tunaongelea mambo ya elimu? naamini hilo suala ni la lazima na sio la kutambia majukwaani, hembu tutazame nchi ambazo tulipaata nazo samba samba uhuru leo zipo wapi na linganisha na TANZANIA, wanafunzi bado wanakaa chini, elimu ni ya kuunga unga, hembu tazama shule za kata halafu tuseme ukweli elimu bora ipo wapi hapo?

Nakubaliana na wewe kuwa propaganda zingine ni lazima zijibiwe kwani ndio siasa lakini isiwe tunaacha kutolea ufafanuzi mambo ya msingi tunajikita kwenye hoja dhaifu eti kwasababu zinajibika kirahisi.

Nimebahatika kusafiri sana katika Mikoa kadhaa katika Nchi hii, nafika mpaka huko vijijini maisha yaliyopo huko kwa kiongozi anayejali wananchi wake wala asingekubali waishi vile, hembu tazama viongozi walivyojilimbikizia mali, hembu tazama mtu anapoukwaa uwaziri gafla maisha yake yanavyobadilika, sijui kama ushawahi kufika hata Amana hospital ukajionea mama zetu walivyolala chini wakisubiri kwenda kujifungua, ndugu Miaka 50 ya uhuru hata vitanda hospitalini hakuna na bado munasema CCM iongoze hii Nchi tena! napata mashaka.
 
Hivi lile VAZI LA TAIFA limefikia wapi? (though to me was a childish idea).

Nchimbi aliunda TUME YA VAZI La taifa na ikazunguka mikoa yote ya Tanzania kutafuta maoni. We want to know matokea ya TUME hiyo maana imeteketeza pesa za walalahoi wa Tanzania. Au ulikuwa ni mradi wa Nchimbi? baada ya kuhamia Internal affairs umekufa?

Huyu Nyerere mimi ninaona tunamtukutza sana (No disrespect to him). Nyerere kwamba hakuwahi kuvaa sare za CCM, so what? Inanikumbusha kauli ya Mkapa kwamba Vicent Nyerere sio ukoo wa Nyerere kwasababu Nyerere hakuwahi (Mkapa) kunitambulisha hata siku moja.

Hizo ndiyo light touch politics za Tanzania.

Mkuu nimekusoma vizuri sana....loud and clear.
Politics za nchi hii zimekuwa to lite.
Mtu anaandika page nne eti anakanusha Nyerere kuvaa au kutovaa sare za chama.

Hiyo ndio politics yenyewe ya Tanzania na hususani CCM, eti fulani ana kadi ya CCm hajairudisha....kwahiyo?

Zipo hoja za msingi za kutolea ufafanuzi. Ni ujuha tu unawasumbua hawa.
Kwanini wasije kueleza mabilioni ya JK yalitoka kwenye source ipi na mafanikio yake yakoje.
Was it meant to be a revolving fund? Does it revolve?

Tusikie mikakati ya kufanya mageuzi ya mfumo wa elimu.....Tumemsikia Kitila Mkumbo amesema education system hii inatakiwa kufanyiwa kubadilishwa. Waje hawa watetezi kusema isibadilishwe na watupe sababu za msingi.
Kama wanafunzi zaidi ya 500 wanafaulu kwenda sekondari lakini hawajui kusoma wala kuandika. Waje hapa hawa watetezi, watuambie ubora wa elimu hii upo wapi na haya matokeo ni propaganda au ni fact.

Watu wazima wanajadili sarawili na skati na blauzi.
Insanity is a talent to some of them.
 
Haya yanayozushwa na tuhuma za "namna hii" zinazoelekezwa CCM kila uchao ni ushahidi tosha kuwa CHADEMA wamekosa sera na hoja za msingi za kuwavuta watanzania katika Chama Chao hivyo kujikita katika hoja dhaifu na zisizo na mashiko za namna hii, lakini kwa kuwa ni tuhuma na mara zote tuhuma ikiachwa bila kujibiwa watu huwa wanaiamini tuhuma hiyo na kuisadiki.

Wananchama wa CCM, wanao wajibu wa kufafanua na kutoa ufahamu kwa watu juu ya tuhuma mbalimbali zinazoikabili CCM kwa kadri ya Ufahamu wao.
Sas we n. A. P. e kwa akili yakoa unaona umeonea la maana? Nyie magamba manaushawishi gani kwa wananchi zaidi ya ununuzi wa kura? Kuhonga wananchi kapelo, sukari, chunvi, kanga ndo ushawishi? Jaribuni kuwa haya. Cdm ulisha sikia wamehonga mtz yoyote ili wachaguliwe? Jiandaeni kuwa wapinzani wazuri chama cha mabepande ambacho kiko radhi kutoa hata uhai wa mtu ili mladi kiendelee kutawala.
 
Too low! Kisheta? Poyoyo? Mburura? Mwenye akili timamu hawezi kujibu kipuuzi namna hii!
 
Haya yanayozushwa na tuhuma za "namna hii" zinazoelekezwa CCM kila uchao ni ushahidi tosha kuwa CHADEMA wamekosa sera na hoja za msingi za kuwavuta watanzania katika Chama Chao hivyo kujikita katika hoja dhaifu na zisizo na mashiko za namna hii, lakini kwa kuwa ni tuhuma na mara zote tuhuma ikiachwa bila kujibiwa watu huwa wanaiamini tuhuma hiyo na kuisadiki.

Wananchama wa CCM, wanao wajibu wa kufafanua na kutoa ufahamu kwa watu juu ya tuhuma mbalimbali zinazoikabili CCM kwa kadri ya Ufahamu wao.
Nape = "Dr Slaa ana kadi ya CCM".
Dr Slaa = "Kadi ya CCM ninayo nimeifanya kumbukumbu".
Nape = "Nampongeza Dr Slaa kwa kukiri".
Hebu tujiulize hii ina TIJA gani kwetu wananchi?
 
Mwalimu RIP.CCM na Mwenyekiti wake tupeni jibu kwa nini TANZANIA NI maskini TAJIRI?kwa nini maji safi na salama,elimu ya awali(kindergatten hadi form six) afya ya msingi(kunawa mikono kabla ya kula,kuchemsha maji,kuvaa viatu,kula chakula bora, kulala vizuri,) ni kitu haiwezekaniki eti?MWALIMU ALICHOVAA AU KULA AU RAFIKI ZAKE AU IMANI YAKE YA DINI AU UADILIFU siyo mada muhimu kwenu-maana MANIFESTO/ILANI yenu haiseemi mnamuunga mkono MWALIMU.KWA NINI MMEKUWA CHAMA CHA MAFISADI wala si MAPINDUZI?Haya ya propaganda za CDM sisi tutajua kuchambua mkishajibu kiu zetu jamani NAPE na mawakala wako JF!
 
Kweli naona CCM wameamua kutekeleza agizo la mwenyekiti wao kujibu kila kinachoongelewa kuhusu CCM, jibuni na hoja ufisadi,wizi wa epa,kagoda,meremeta na jinsi vigogo wa serikali wanavyotorosha twiga wetu kwenda arabuni, pia hela mlizoficha uswis yapo mengi ya kujibu muhimu zaidi ya kutetea nguo zenu za kijani.......Tanzania tuna shida ya huduma bora na maisha mazuri sio sare zenu jamani.......kha!

****!! Umevurugwa, kajipange upya uje uandike tena. Kumbuka ukweli utabakia kuwa ukweli no matter what
 
Nyerere alikuwa yupo ki-taifa zaidi kuliko ki-chama.
 
kichwa chako naona unafugia nywele gamba wewe!kadanganye huko chimwaga....hujui lolote zaidi ya uzandiki na ujuha
 
Baba wa taifa alijua kuwa ipo siku chama kingine(CDM)kitakuja ongoza tanzania na ndio maana alitumia sare rasmi ili wana nchi wajue mbadala wa Ccm
 
Hujui unachoongea TandaleOne,
Kifupi tu ni kua Mwalimu alikua na falsafa za "TAIFA KWANZA, CHAMA BAADAE".
Huo unaoongea hapo ni uongo, uzandiki, ujuha na uzushi tu.
HIVI WEWE NI RAIA WA NCHI HII? unaposema Falsafa ya TAIFA KWANZA CHAMA BAADAYE unamdanganya nani? Yaani mkutano wa kizota ugharimie bilion kumi na tano wakati vyuo vya ualimu havitoshi kuelimisha walimu? yaani watoto wa Dar Es Salaam wanakalia mawe darsani wakati mktano wa NEC unaghalimia milion 400? watu mtwara wanatembea uchi hawana nguo wakati kiongozi wa chama na magari matatu ya kumsaidia kazi ?

Hiyo Flasafa unayoitamka wewe inatumika zaidi katika nchi za westerm europe , India, Israel, Philipin4ena marekani kuliko kokote hapa duniani
 
Mbona kwenye kinyanganyiro cha kumpachika mkapa mwalimu alikuwepo?na mbona wanachama tulivaa sare hizo?bado swali lipo pale pale!!kwa nini hakuwahi kuvaa sare hizo?ziwe kitenge,kofia,overall au chochote?ukweli ni kuwa sare za chama zilikuwepo enzi za mwalimu ila hakuwahi kuzivaa!!!hizo blaa blaa nyingine hazina kichwa wala miguu,cha msingi tujiulize kwa nini hakuvaa basi!!hizo porojo za Tanu na Taa sijui jwtz sijui jenerali nani haziwezi kubadili ukweli!!ngoja nikutumie hela ya kangara moja uzimulie hangover ndiyo inayokusababisha umwage povu hapa,kwanza hoja yenyewe haina maana hata chembe,kama alivaa au hakuvaa haitusaidii chochote,tungejadili mabilioni ya uswis au ile ya misumari badala ya vipuri na jinsi gen mboma anavyotafuna tanesco hapo tungekuwa tunatenda haki,ccm mmekifanya chama cha porojo na wizi tuuu,wakati mwalimu alikijenga kwa misingi ya utaifa!!kwenda kule.
umenena vema mkuu.
 
Baba wa taifa alijua kuwa ipo siku chama kingine(CDM)kitakuja ongoza tanzania na ndio maana alitumia sare rasmi ili wana nchi wajue mbadala wa Ccm

Mathayo 23

9 Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.
 
Haya yanayozushwa na tuhuma za "namna hii" zinazoelekezwa CCM kila uchao ni ushahidi tosha kuwa CHADEMA wamekosa sera na hoja za msingi za kuwavuta watanzania katika Chama Chao hivyo kujikita katika hoja dhaifu na zisizo na mashiko za namna hii, lakini kwa kuwa ni tuhuma na mara zote tuhuma ikiachwa bila kujibiwa watu huwa wanaiamini tuhuma hiyo na kuisadiki.

Wananchama wa CCM, wanao wajibu wa kufafanua na kutoa ufahamu kwa watu juu ya tuhuma mbalimbali zinazoikabili CCM kwa kadri ya Ufahamu wao.

Sawa, nakubaliana nawe!.. SIFONGO kataja hoja "dhaifu" za CHADEMA dhidi ya magamba, kama vile: Wizi wa EPA, Kagoda agriculture, meremeta, mabilioni ya uswisi, wizi wa wanyamapori kupitia uwanja wa ndege wa KIA!.. Wizi huu wote ni kazi ya CCM.

Je, wizi huu ni uzushi? kama ni uzushi mbona hata viongozi wa CCM wanakiri kutokea? BASI TUPE UKWELI!.. MBONA UNAKWEPA?
 
Back
Top Bottom