Papaa Kinyani
JF-Expert Member
- Feb 25, 2013
- 1,457
- 699
Naibu Waziri Mpina hongera kwa kazi ya kukagua mito ya Dar es Salaam na kugundua sumu mbalimbali zilizomo ambazo zingeathiri afya za wakazi. Hapa mbezi beach nyuma ya kiwanda cha Interchick kuna ka-mto chenye maji machafu mwaka mzima, kuna raia wanalima mboga mboga nyuma ya kituo cha basi cha jogoo wanatumia maji hayo, tuna wasiwasi kuwa maji hayo si salama kwa mboga hizo. Tunaomba watu wa NEMC mpite na hapo muangalie tafadhali.