Maji yamelowana

Muwekezaji wa pesa nyingi anahitaji guarantee ya mda mrefu Ili na yeye arudishe pesa ya uwekezaji wake na faida maana hajaja kutoa msaada.
 
Haya sasa, mlikuwa mnatutukana, nchi ndio hiyo inapigwa mnada.., ngoja tuone..
 
Watengeneza wafalme wapo kazi kujihakikishia ufalme endelevu..!! Ukiangalia kwa undani hata yule aliyeko pale walipo wao kwa maana ya ukuu wa eneo hilo, alianza kupotea... Lakini akaja dada wa kaka ambaye kaka anaelewana naye sana akarudi himayani..

Ikatokea kisa kinachotaka kulipwa kisasi maana walishaambiwa waliotoka wasisikie kuwasha...!! Kuwashwa ni wakati ukiwa kitini tu..!! Nje ya hapo si ruhusa, ukizingatia simba wa yuda alijiamulia kila kitu kwa aonavyo yeye. Na ndiyo maana yale masandarusi yaliyokuwa yanapelekwa kule alikotokea hayajulikani yal;ikuwa yanapokelewa na nani..!! Na ndiyo maana kesi ilipoamuliwa na Mungu kwa hukumu ile, wale wa eneo alilotoka wakawa na wanaendelea kubisha kila cha sasa..!!

Tusubiri maji yakauke, maana yamelowa chapchapa
 
Mjini kushindikana ni fikra tu na si uhalisia..!! Wapo watakaoamini hilo na wapo watakaoona tofauti na wengine, ukiwemo wewe, waonavyo..!! Maana kila mimi nikifanyacho, wananzengo hutawanyika kwenye makundi kadhaa, lakini makubwa matatu kama vile Rais, makamu wake na waziri mkuu..!!! Kwa wale wa kundi la kwanza, wao watanitazama kwa namna mimi ninavyowaeleza, lakini wale wa makamu wa watanitazamani tofauti na maelezo yangu, na wa wa kwa waziri mkuu wao inategemea tu nini kinajiri mara baada ya wao kujihusisha na mjadala
 
Unataja majina makubwaaaa
 
 
Hapa nimetoka mkavu kabisa, mzee punguza code nasi tupate kuelewa japo kidogo
Mzee Shamte mtoto wa Mohamed Shamte waziri mkuu wa serikali ya Zanzibar iliyopinduliwa alifikiri CCM ni watu hadi kumsaliti baba yake.Anavuna alichopanda.kimsingi Zanzibar inauzwa na Tanzania kwa ujumla,ni swala la muda tu maneno ya Jobo yanatimia.Kule ngorongoro na Loliondo kazi imekwisha anasubiriwa shetani kuhitimisha.
 
Message sent and received very clearly
 
Na ndiyo maana kesi ilipoamuliwa na Mungu kwa hukumu ile, wale wa eneo alilotoka wakawa na wanaendelea kubisha kila cha sasa..!!

Tusubiri maji yakauke, maana yamelowa chapchapa
 
Taifa halina dira kila anaekuja anakuja na yake lazima tuone tofauti!. Walinda mipaka mi huwa nawashangaa hivi unawezaje kulinda pembeni yako nawakati katikati yako inaliwa!..
Ndani kuna watu wanajiita "wasalama". Simaanishi Sungusungu, yaani ni watu wa ndanindani huko deep. Lakini hata huo Usalama wao haujulikani ni Usalama wa nini. Kwa nchi nyingine hawa ndo wangerekebisha kukubali au kukataa madudu ya ndani, kurekebisha au kunyoosha makandokando. Lakini hawa wa kwetu wapo, wapowapo tu ni Bora Sungusungu wa Buchosa wangepewa hii kazi.
 
Mbona ya huko yanaeleweka.
Mwinyi alisema kuwa hivo visiwa havitumiki. Sasa wakaona haja ya kuvifanya viwe productive.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…