Maji ya Ndanda yapigwa marufuku mkoani Mtwara

Maji ya Ndanda yapigwa marufuku mkoani Mtwara

Watz acheni uvivu wa kufikiri, BWANA AFYA ni mtaalam maamuzi yake yasibezwe

serikali ya ccm kupitia mkemia mkuu iliwahi kuchoma unga wa bakhresa wakidai kuwa haufai kwa matumizi ya binadamu,the outcome,walipelekwa mahakamani serikali ikashindwa kesi bakhresa akalipwa mabilioni..endelea kuwaamini hao unaoita wataalamu(wengi wao siku hizi ni wanasiasa,wanatumika kisiasa na kibiashara).
 
mbona maji ya bakhresa machafu sana? yanavumbi
 
Yale maji ni mazuri ever in tz,alafu yana nembo ya Tbs tangu kiwanda kianze uzalishaji.,ubora huo ulitokea wapi.
Mbali na mengi,nahisi na jamaa wa pride mtwara nao wanahusika ktk fitina kwani ni mmoja wa share holders wa kiwanda kingine cha maji(brand name nimesahau)

Ni Makonde water Spring, wameyapigia debe sana lakini wapi yamefulia mbaya hamna mtu anayekunywa...kila mtu ni ndanda tu...bei karibu na bure na yana radha halisi ya Spring!! Hata wakataze siezi acha kuyanywa hayo maji
 
Huku rukwa kuna maji dew drop ni best all over the country
 
Ni Makonde water Spring, wameyapigia debe sana lakini wapi yamefulia mbaya hamna mtu anayekunywa...kila mtu ni ndanda tu...bei karibu na bure na yana radha halisi ya Spring!! Hata wakataze siezi acha kuyanywa hayo maji

Mkuu fitina imeanzia hapo ila nashangaa watu wanavyomtaja Bakharesa/Mengi katika sakata hili.
 
Dah inaweza kuwa moja ya sababu mbali na fitina za biashara,kwa lindi huu mchezo ni umeshamiri sana
Nimezunguka Tanzania. Maji Mengi yanachumvi. Maji ambayo ni mazuri na ni baridi ni(kwa test yangu mimi binafsi): Ndanda Springs-Mtwara, Kilimanjaro- Kilimanjaro,Rungwe- Mbeya, Ruwenzori- Nilikunywa Mwanza( niliambiwa yanatoka Uganda sina uhakika). Kuna maji fulani yapo Dodoma( nadhani FURAHA).Kosa la Ndanda ni kuwaachia wahuni wachukue.chupa zao hasa pale Stendi ya Basi Lindi, bila jamaa kunitonya ningekunywa tope, yaani wauzaji wadogo wanachukua chupa za maji ya Ndanda wanaweka maji ya Bomba halafu wanauza eti ni Ndanda. Nashangaa wenyewe Ndanda wanakaa kimya badala ya kuwachukulia hatua wanakaa kimya. Ngoja wale ban ndo watakuwa makini kufuatilia bidhaa zao
 
huo uchafu labda tulivyokuwa tukiogelea kwenye mto mwena/ndanda.. enzi hzo tupo ndanda high school
 
Back
Top Bottom