Maji ya kipindi cha Nuhu kutengeneza Safina yalienda wapi?

KenBayona

New Member
Mar 26, 2017
1
7
Kwa muda sasa najaribu kujiuliza hili swala kwamba Bahari ilikuwepo tangu kuumbwa kwa hii dunia ila maji yalioangamiza kizazi cha enzi za Nuhu yalipotelea wapi katika uso wa dunia au ndio kusema kina cha bahari kiliongezeka?

Mwenye uelewa juu ya hili naomba anisaidie.
 
Kama unadhani kuna gharika ilitokea jiulize maswali haya.
1. Maji yalitoka wapi na yalikwenda wapi baada ya gharika.
2. Wanyama walikuwa wanakula nini ndani ya safina.
3. Nani alianza kuwasambaza tena wanyama baada ya safina kwenda maeneo mbalimbali ya dunia.
4. Kuna wanyama ambao hawawezi ishi kabisa mashariki ya kati kama polar bears nuhu aliwezaje ishi nao.
5. Zaidi ya species million 8 zilitoshaje kwenye safina ndogo kuliko hata titanic.
6. Kwanini formation ya miamba hai suggest uwepo wa gharika hata nusu dunia tu.
 
kama unadhani kuna gharika ilitokea jiulize maswali haya.
1. maji yalitoka wapi na yalikwenda wapi baada ya gharika
2. wanyama walikuwa wanakula nini ndani ya safina
3. nani alianza kuwasambaza tena wanyama baada ya safina kwenda maeneo mbalimbali ya dunia
4. kuna wanyama ambao hawawezi ishi kabisa mashariki ya kati kama polar bears nuhu aliwezaje ishi nao
nitaongeza mengine badae
Kwani binadamu tulioenea dunia nzima nani alitusambaza?
 
Kuna muda ambao huwez kupata majibu sahihi ya maisha walioishi zaman sana,,,kuna maswali ambapo akili haiwez kufikia kifikra..so hutapa jib lililonyooka
 
Mbona kuna maji barid na maji chumvi wakati maji yote yalijichanganya!! na kama maji yote yalikuwa ya chumvi, Nuhu and co walikunywa nni?
 
nita kujibu kwa kisayansi.asilimia 80 ya dunia imetawaliwa na maji .hata takwimu za viumbe vingi vya kila aina vipo kwenye maji.wanasayansi wanadai kama sehemu zile mbili kusini na kaskazini ambazo ni antarctica na mwenzake ni kama mabara ambayo huesabiwa na barafu yenye maji mengi kama yakiweza kuyayuka.
 
kama unadhani kuna gharika ilitokea jiulize maswali haya.
1. maji yalitoka wapi na yalikwenda wapi baada ya gharika
2. wanyama walikuwa wanakula nini ndani ya safina
3. nani alianza kuwasambaza tena wanyama baada ya safina kwenda maeneo mbalimbali ya dunia
4. kuna wanyama ambao hawawezi ishi kabisa mashariki ya kati kama polar bears nuhu aliwezaje ishi nao
nitaongeza mengine badae
Ukitaka kujua uwezo wa watu kufikiri wewe soma tu mada kama hizi ndipo utaweza kushangaa sana....

Mtu anahoji jambo lililotokea miaka maelfu huko utadhani limetokea mwaka jana. hivi ni kweli hatujui kabisa kuwa kulikuwa na tofauti kubwa sana ya kimazingira na hali ya hewa kipindi kile na leo?

Hata hivyo,unapohoji na kujibu masuala ya ki-Biblia unapaswa ufikirie kwa namna ambayo siyo sawa na hii ambayo unaifikiria kwenye aisha ya kawaida kwasababu kuna mambo yaliyoko kwenye biblia ambayo hayawezekaniki kwa namna ya kawaida kwasababu mtendaji hafungwi na kanuni zinazokufunga wewe....

Sasa kama mtu anahoji namna wanyama wanaoishi kwenye mazingira fulani kuweza kuishi kwenye safina ambayo haina mazingira hayo huyo ni moja kwa moja anafungwa na kanuni ambazo aliyewafanya wanyama hao wakaishi kwenye safina hafungwi nazo....

Hilo ni sawa na kuhoji walichokuwa wanakula wanyama siku zote,yaani ni kichekesho kikubwa kabisa....

Hujui tu kuwa kuna mwanamama mmoja alitumia unga kidogo sana aliokuwa nao bila kuisha kwa siku mingi tu,jambo ambalo haliwezekaniki kwa akili zako za kawaida ambazo kwa kiwango kikubwa zimejengwa na mazingira na jamii yako na hivyo kuzifanya kuwa ziyo zako.....

Tunashindwa kuelewa hata mambo madogo kama haya,inasikitisha sana....
 
Back
Top Bottom